KISA KILICHONITOA MACHOZI MTWARA MJINI.(Edited) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KISA KILICHONITOA MACHOZI MTWARA MJINI.(Edited)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sizinga, Oct 17, 2010.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kwa wale wakazi wa Mtwara,mtakuwa mnaijua vizuri ile barabara itokayo pale Ligula Hospitali inashuka chini kuelekea kwa Jionee, Cocobeach,TTC mpaka kiyangu, hii ni barabara kubwa na ina nzuri kwani ina kiwangi kizuri cha lami. Ukifika pale kwa jionee kuna junction, ile barabara inayoelekea CHUNO, na hapa ndipo kisa hiki kimelalia.

  Hii barabara ilikuwa ipo kwenye service, labda inawezekana ukweli kwamba kipindi hiki cha uchaguzi mara nyingi barabara za huku mtwara nyingi zinafanyiwa marekebisho. Sasa Muhandisi wa hii barabara(Contractor) ni kijana flani wa makamu(miaka 35-40) simfamu kwa jina ila tu nikimwona mwona na wafanyakazi wengine wa barabara hii wakijishughulisha kuweka lami hii barabara.

  Hivi majuzi huyu bwana, alitokea kumpenda(sidhani kama ni kumpenda au ni hulka ya mwili) mdada flani(jina nalihifadhi) ambae amepanga nyumba flani inatazama na hii barabara. ifahamike kwamba huyu dada alikaa zaidi ya miaka miwili hospitali na ni mwasirika wa VVU, na still anaendelea kutumia ARV kusogeza siku mbele, na hapo mtaani watu wote kama sio wengi wanamfamu vizuri tu huyu dada. Ikumbukwe kipindi cha nyuma miaka ya 2000 huyu dada kutokana na uzuri wake alikuwa 'matawi ya juu' sana!

  Huyu Contractor bila kujua hilo(ni mkazi wa Dar) akaja siku hiyo pale kwake akamtongoza wakakubaliana, akalala nae.

  Siku ya pili huyu bwana akaja tena, akanunua soda, akaket mduleni akaanza kunywa. Bahati nzuri mama mwenye nyumba siku hiyo alikuwepo pale na huu 'mchongo' alikuwa keshaupata. Basi yule mama nae akaenda kukaa na yule baba pale mduleni, na 'akamchana live' kwamba ulyefanya nae ngono jana ni muathirika ana UKIMWI......

  Ngoja niwaambieni..huyu dada ni ''muuaji'' kiufupi,alicheza sana kipindi cha 'balehe' yake,labda kwa sababu ya uzuri wake. Wakati yupo hospitali manesi walikuwa wakisema aliruhusu kuingiliwa nje ya maumbile na kusababisha kupigwa 'bomba' na ikafikia hatua kwamba sehemu kubwa ya viungo vyake vya ndani(utumbo) vimeshaharibika, na isitoshe miguu yake imeshapoteza nguvu(haina balance), ni juzi tu alianguka kwenye ngazi za kupandia bafuni na kusababisha mguu wake mmoja kuvunjika na tayari keshawekwa kopa(POP).

  Na yule daktari aliyemtibu huo mguu alikuja kumuangalia pale home kwake na baadae aliwaambia wapangaji wengine kwamba eti wakati anamweka kopa alikuwa anamtega kumshikashika' wakati yeye(dokta) ndiye aliyekuwaw anasupply ARV kwa huyoo dada. Isitoshe siku moja mtoto kiume wa mama mwenye nyumba aliitwa chumbani kwa huyu dada ili amkrekebishie TV yake,akampa na bia moja, jamaa akawa anakunywa, bia ilipofika nusu yule dada akaanza kumtega kumkumbatia n.k. Jamaa kuona hivyo akaruka na kuondoka zake. Baada ya masa kadhaa kupita jamaa akarudi amelewa na akaanza kumtusi yule dada ikawa kama kuna ugomvi hivi....so huyu dada anafanya makusudi kuwafata wanaume ilhali anajua yeye ni mgonjwa. Sina uhakika kama huyu Contractor alimtongoza au huyu dem alimtega na jamaa akaingia kichwakichwa...

  Yule baba alivunja ile soda aliyekuwa anakunywa palepale, akaanza kulia na kutoa michozi huku akisema kwa uchungu kwamba alikuwa hakujua hilo, mbaya zaidi alisema kwamba kabla ya kukutana nae alienda duka la jirani kununua Condomz, lakini yule dada alikataa katakata kutumia kondom nna jamaa akaziweka kando....kikubwa zaidi wakati analia akisikika akisema kwamba ana mke na watoto, na hajui atamwambia nini mke wake akirudi huko Dar.

  Baada ya siku mbili kupita tangu ule mkasa niliona magari ya mchanga yakija na kuanza kusomba zile changarawe ambazo ilibidi zitumike kwenye ile barabara na mpaka sasa hivi hii barabara ina changarawe zenye vumbi na ule uji wa lami haujawekwa bado, nilijaribu kuwauliza wale jamaa wakiopaikiza changanrawe kulikoni walisema yule contractor kaenda Dar es salaam..sasa sikujua kwamba mkataba kaukatisha au ilikuaw vp wameiacha hii barabara na vumbi lake...Hiki ni kisa cha kweli na kimeniskitisha sana .(http://erwinsizinga.blogspot.com)
   
 2. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Tusikurupuke kutongoza au tusiwe wepesi kutegeka jamani tutakufa hivi hivi
  Aids inaua.Tuheshimu ndoa zetu jamani
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hivi hii thread si ipo tayari humu au ni nini kinaendelea......mmenimix
   
 4. E

  Elam Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  pole sana kwa uyo mjomba lakini ni fundisho kwetu sisi wengine kuto kurukia kila ua kama nyuki wa kienyeji,bila kujua maua mengine hayana asali bali ni sumu....aksante kwa kutupatia mfano hai..
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Ipo ila hii imekuwa ''edited''...imegusia majibu ya wale waliokuwa wanauliza kwenye ile thread ya kwanza..........
   
 6. Nchi Kavu

  Nchi Kavu JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 3,519
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Dah! Na huyo mhandisi mh! Ntu kutoka dar kufika ntwala kuntia demu hujui historia yake. Sasa ndo ivo kujuta, bha!!
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wapo wanaume wengi sana wenye tabbia kama ya huyo mkandarasi... wengi weanakuwa vipofu linapokuja suala la ngono. Inabidi wajifunze kuanzia sasa kuwa uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mbao
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo wewe ndio nyani<abiziani>?
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hapana
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sawa mkuu, ila si vibaya hata ukiwa na ID mbili, ndio uhuru wenyewe huo!
   
 11. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Ni vema AKAPIME Kujua kama hana Ukimwi Kabla halafu baada ya miezi mitatu acheki .Tena siku hizi Chance ya Kuambukizwa kwa tendo moja si kubwa kihivyo
   
 12. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  hahahahaha umenikumbusha mbali sana!!:biggrin1::biggrin1:
   
 13. Engineer2

  Engineer2 Senior Member

  #13
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani alibakwa? si alifanya kwa hiari yake mwenyewe? na nani kakuambia kuwa wenye VVU hawana haki ya ngono? issue hapa ni safe sex, kama alienda kavu kavu imekula kwake, akapime aanze arv
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,460
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Ni suala la nature kuizidi common sense...inawapata wengi tu na si suala la kudhihaki
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mi sijaelewa naombeni mwongozo: Kuingiliwa Nje ya maumbile ndo nini??
   
Loading...