Kisa cha Waziri Ngeleja na Mlinzi kwenye ATM

Wadau popote mlipo kama kuna mtu anayeweza kupata kujua hatima ya mjakazi wa waziri ngeleja hata familia yake hatuletee taarifa, wenzetu wanasheria tunaomba mpe huyu mwajibikaji kazi kwa haki msaada wa hali ya juu mimi binafsi niko tayari kutoa kiasi cha pesa ambacho sitakisema naomba tuangalie kama tuna uwezekano wa kumsaidia huyu mtu kwa hali na mali .kiburi cha ngeleja kimeshafanyiwa maziko ni kwamba yeye hajapata fahamu. Mkono mtupu haulambwi. MANENO MATUPU HAYAVUNJI MFUPA

Tuta, kukusahihisha huyu jamaa hakuwa mjakazi wa Ngeleja bali ni askari wa kampuni fulani ya ulinzi, cha kufahamu hapa ni kuwa kama jamaa bado ana kazi ili msaada zaidi uweze kuangaliwa kama atasaidiwaje kisheria, ukisema achangiwe je una uhakika kuwa na yeye mwenyewe atakubali kufanyiwa hivyo? nadhani swala zima la sheria za kazi ndio msaada pekee utakaoweza kumsaidia zaidi
 
These half God-Ministers of ours!.

Expecting everyone to know you is something very stupid...for what special thing that you have done to this country, that deserves the recognition of your parabolic-belly by the whole state?...

Is it being friend to the landlord?...POOR YOU!
 
Ngeleja ni waziri kama MISIFA TU!! anayo sidhani kama amekosa sehemu za kutafutia SIFA mpaka aende kwenye ATM kutafuta MISIFA sema tu huyo MLINZI alitaka kwenda kuwaonyeshea wale waliokuwa wakisubiri kwenye ATM kuwa yeye anajua lkn alipaswa kuwa mstaimilivu maana mtu yeyote mwenye ATM CARD automatically anakuwa na ufahamu hivyo anajua nini anafanya.

NGELEJA ni WAZIRI bwana anajulikana sana na dunia na anastaili heshima maana huyo ni kiongozi hii ni biblicaly maaana maanadiko yanasema muheshimu kiongozi wako sasa wewe unakuwa hauna nidhamu kwa mkuu wako unaakili kweli?

Na mlinzi kazi yake ni usalama kama kuna mwizi yeye ni kazi kuzuia mwizi asiibe ATM na sio mtu kachukuwa muda mrefu kwenye ATM.

Just imagine ukitoka kwenye ATM uku ukiwa umechukuwa muda mwingi alafu ukakuta foleni kubwa nje how do you feel? Je ni SIFA? NGELEJA hakuafanya hivyo, ni moto wa mlinzi wakuchukulia kila mtu poa ndio umemponza.

Hamjawahi kwenda kwenye ofisi za watu mlinzi anakuuliza: "unataka kumwona boss shida yako nini?" ukimjibu shida binafsi anakwambia mfuate nyumbani!!!:confused:

mambo mengine tuwe tunaacha hao walinzi sometimes wao wanapokuwa walinzi wa benk wanajihisi kuwa na wao wanamamlaka ya Kufanya chochote.
Simlaumu Ngeleja.

Hilo litakuwa ni fundisho kwa walinzi wengine wenye nyodo na waonevu wa rahia wa KAWAIDA

Sasa heshima itakuwepo sababu watakuwa wakiogopa kuwa huyu mtu kwenye ATM anaweza kuwa waziri hivyo nidhamu itakuwepo Kwa watu wa kawaida pia.
.
 
Unamhukumu mlinzi huyu usiyemjua wala kupata nafasi ya kukutana naye kwa mujibu wa mazoea yako na walinzi yaliyopita.

Unfair, unjust.

The bigwigs need to respect some common courtesy like the rest of us.

Hii iko deep sana mazee... proper!!
 
tuta, kukusahihisha huyu jamaa hakuwa mjakazi wa ngeleja bali ni askari wa kampuni fulani ya ulinzi, cha kufahamu hapa ni kuwa kama jamaa bado ana kazi ili msaada zaidi uweze kuangaliwa kama atasaidiwaje kisheria, ukisema achangiwe je una uhakika kuwa na yeye mwenyewe atakubali kufanyiwa hivyo? Nadhani swala zima la sheria za kazi ndio msaada pekee utakaoweza kumsaidia zaidi
naelewa mkuu ujakazi nimeitumia kama zama za kale wafalme walivyokuwa wanawatumisha na kuanyanyasa watumwa au wafanyakazi .nikimaanisha ngeleja ndio mfalme au mkuu fulani ambaye kama humjui yeye ni nani .wakati unatekeleza wajibu wako utakiona cha mtemakunde kuhusu msaada kama raisi wako anakusaidia kukuombea wewe misaada mwananchi utapata waPi ujasiri wa kukataa msaada?
 
ngeleja ni waziri kama misifa tu!! Anayo sidhani kama amekosa sehemu za kutafutia sifa mpaka aende kwenye atm kutafuta misifa sema tu huyo mlinzi alitaka kwenda kuwaonyeshea wale waliokuwa wakisubiri kwenye atm kuwa yeye anajua lkn alipaswa kuwa mstaimilivu maana mtu yeyote mwenye atm card automatically anakuwa na ufahamu hivyo anajua nini anafanya.

Ngeleja ni waziri bwana anajulikana sana na dunia na anastaili heshima maana huyo ni kiongozi hii ni biblicaly maaana maanadiko yanasema muheshimu kiongozi wako sasa wewe unakuwa hauna nidhamu kwa mkuu wako unaakili kweli?

Na mlinzi kazi yake ni usalama kama kuna mwizi yeye ni kazi kuzuia mwizi asiibe atm na sio mtu kachukuwa muda mrefu kwenye atm.

Just imagine ukitoka kwenye atm uku ukiwa umechukuwa muda mwingi alafu ukakuta foleni kubwa nje how do you feel? Je ni sifa? Ngeleja hakuafanya hivyo, ni moto wa mlinzi wakuchukulia kila mtu poa ndio umemponza.

Hamjawahi kwenda kwenye ofisi za watu mlinzi anakuuliza: "unataka kumwona boss shida yako nini?" ukimjibu shida binafsi anakwambia mfuate nyumbani!!!:confused:

Mambo mengine tuwe tunaacha hao walinzi sometimes wao wanapokuwa walinzi wa benk wanajihisi kuwa na wao wanamamlaka ya kufanya chochote.
Simlaumu ngeleja.

Hilo litakuwa ni fundisho kwa walinzi wengine wenye nyodo na waonevu wa rahia wa kawaida

sasa heshima itakuwepo sababu watakuwa wakiogopa kuwa huyu mtu kwenye atm anaweza kuwa waziri hivyo nidhamu itakuwepo kwa watu wa kawaida pia.
.

ni vyema umjionyesha wazi kuwa we ni kibaraka wa ngeleja!
 
Waswahili walisema 'Aliyejuu mngoje chini' [Kwani atashuka tu] Lakini vijana wa siku hizi wanasema 'Alyejuu mfuate huko huko[Kitaeleweka]
Mimi ninaamini kabisa kuwa mlinzi huyo kosa lake ni kumuambia mkubwa apishe wenzake [hata hivyo siyo ustaarabu kuongea na simu kwenye kibanda cha ATM wakati kuna wateja wengine nao wanangojea huduma hiyo] Huyo waziri hakuwa mstaarabu kabisa na hiyo hadhi yake anatembea nayo lakini aelewe kwa wastaarabu amejiabisha mwenyewe. Ninaamini kabisa ajira ya huyo mlinzi iko mashakani na ushahidi pekee ni footage ya camera lakini kwa sababu itampiga chini mheshimiwa inawezekana isioneshwe kabisa.
Ushauri kwa mlinzi- Akiona anaadhibiwa na mwajiri kutokana na uoga wao basi aende akalalamike kwa afisa kazi na asisitize footage ya tukio kama ndiyo ushahidi wake.
HAKI YA MTU HAIPOTEI KWANI HATA KAMA VYOMBO VYA DOLA VITAMDIDIMIZA LAKINI LAANA YA DHAMBI YA UONEVU WA NAMNA HII MARA NYINGI HUMUATHIRI MTENDA BILA YEYE KUTAMBUA CHANZO.
 
Ngeleja ni waziri kama MISIFA TU!! anayo sidhani kama amekosa sehemu za kutafutia SIFA mpaka aende kwenye ATM kutafuta MISIFA sema tu huyo MLINZI alitaka kwenda kuwaonyeshea wale waliokuwa wakisubiri kwenye ATM kuwa yeye anajua lkn alipaswa kuwa mstaimilivu maana mtu yeyote mwenye ATM CARD automatically anakuwa na ufahamu hivyo anajua nini anafanya.

NGELEJA ni WAZIRI bwana anajulikana sana na dunia na anastaili heshima maana huyo ni kiongozi hii ni biblicaly maaana maanadiko yanasema muheshimu kiongozi wako sasa wewe unakuwa hauna nidhamu kwa mkuu wako unaakili kweli?

Na mlinzi kazi yake ni usalama kama kuna mwizi yeye ni kazi kuzuia mwizi asiibe ATM na sio mtu kachukuwa muda mrefu kwenye ATM.

Just imagine ukitoka kwenye ATM uku ukiwa umechukuwa muda mwingi alafu ukakuta foleni kubwa nje how do you feel? Je ni SIFA? NGELEJA hakuafanya hivyo, ni moto wa mlinzi wakuchukulia kila mtu poa ndio umemponza.

Hamjawahi kwenda kwenye ofisi za watu mlinzi anakuuliza: "unataka kumwona boss shida yako nini?" ukimjibu shida binafsi anakwambia mfuate nyumbani!!!:confused:

mambo mengine tuwe tunaacha hao walinzi sometimes wao wanapokuwa walinzi wa benk wanajihisi kuwa na wao wanamamlaka ya Kufanya chochote.
Simlaumu Ngeleja.

Hilo litakuwa ni fundisho kwa walinzi wengine wenye nyodo na waonevu wa rahia wa KAWAIDA

Sasa heshima itakuwepo sababu watakuwa wakiogopa kuwa huyu mtu kwenye ATM anaweza kuwa waziri hivyo nidhamu itakuwepo Kwa watu wa kawaida pia.
.

mkuu, wewe ni msemaji wa Ngeleja?? siamini kama reasoning hii uliyotoa hapa inatoka kwa Mtanzania mwenye uelewa wa mambo......ungekua wewe ndio mlinzi,ungefanyaje kumuona Ngeleja anaongea na simu ndani ya ATM na kuna foleni kubwa??
 
Na hiyo ULTIMATE SECURITY ni kampuni ya RA.... Masikini Bw.Mnaku... Kesi ya Swala na Chui anapelekewa Simba...
 
jamani katika hili ninamtetea Mh. Ngeleja,walinzi wengi approach yao huwa si nzuri wana kauli mbaya sana na hiyo nafikiri ndiyo uliyomfanya mh. Waziri amuulize kama mlinzi alikuwa anajua kauli aliyoitoa aliitoa akijua anaongea na nani.Yeyote aliyewahi kukutana na adha za walinzi hawezi kufanya utetezi wa kishabiki hapa na kutoa kauli za kumdhalilisha mh.waziri ngeleja. Huyo mnaku mwenyewe anaonekana mropokaji sana ndiyo maana anatafuta sympathy kwenye vyombo vya habari.
Tusimshushie makombora mh.bila kuwa na ushahidi wa kutosha uenda mlinzi alitoa kauli isiyo ya kiungwana,tukumbuke kila mtu anapenda kuheshimiwa,kunyenyekewa nk
 
Hii ingetokea kwenye nchi yenye demokrasia ya kweli na uhuru wa kuzungumza na kiwango flani cha "dirty politics" kama Marekani, hiyo footage kwanza ingeuzwa kwa wapinzani halafu ingetumika jimboni kwake kumdiscredit huyu jamaa.

If only....
 
nimesoma hii taarifa na ninadhani naelewa MATATIZO makubwa ni haya:

1. Mlinzi ana makosa makubwa ya kutomfahamu Mheshimiwa waziri, pengine ni kwa sababu huwa hanunui magazeti yenye picha za mawaziri au haangalii TV ambapo hao mawaziri huwa wanaonekana nyakati mbali mbali - Solution mlinzi na wote ambao hawawajui waheshimiwa wa nchi yetu, wanunue TV na wazisome sura za waheshimiwa wote ili ikitokea mahali popote wanapokutana nao wajue jinsi ya kuwaheshimu

2. Benki ina makosa makubwa ya kutotenga ATM maalum kwa ajili ya Waheshimiwa mawaziri maana hawa waheshimiwa huwa inabidi wawasiliane na waheshimiwa wenzao wakati wowote ule hata ikiwa ni kwenye ATM. Solution: Benki zote zilazimishwe kuweka ATM maalum kwa ajili ya waheshimiwa la sivyo zifungiwe leseni ya kuendesha benki

3. Mwajiri ana makosa ya kutowafundisha watumishi wake ( walinzi) namna ya kuheshimu WAHESHIMIWA wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Solution: kila mwajiriwa wa sehemu yoyote inayotoa huduma kwa wananchi, apewe mafunzo au semina ya jinsi ya kuwafahamu waheshimiwa na namna ya kuwatetemekea

Kwa kuwa sote tunajua kuwa Waheshimiwa wamepewa heshima na ruhusa ya kufanya chochote wakati wowote na wananchi (walala hoi) wote wanapaswa kuwatetemekea tu.
***********************************************
Na hiyo ndiyo Tanzania niijuayo.
Ndio maana mafisadi wameweza kushamiri kwa sababu ya Uheshimiwa huu.
Pengine hili tukio ni la kweli, pengine ni uzushi, lakini ni tukio ambalo si ajabu kutokea Bongo land, mifano iko mingi tu.
 
Hii ingetokea kwenye nchi yenye demokrasia ya kweli na uhuru wa kuzungumza na kiwango flani cha "dirty politics" kama Marekani, hiyo footage kwanza ingeuzwa kwa wapinzani halafu ingetumika jimboni kwake kumdiscredit huyu jamaa.

If only....

Rais Kabila wa DRC amemfuta kazi waziri wake kwa kuwa amegombana kwenye public. Tanzania inawapongeza viongozi wanaokiuka maadili.
 
Hii mbona haijakaa vizuri? Alishindwa nini kumueleza huyo mlinzi kuwa anatoa pesa kwa awamu? Na ninadhani kuna kiwango cha kutolea kwenye hizo ATM kabla haijawa kero kwa watumiaji wengine. Mathlani kwenda kutoa milionio kumi kwwenye ATM ni kuwasumbua wateja wengine. Huyu waziri alitakiwa aonyeshe kukomaa kwa kuliachia hili suala liishie pale pale kwenye tukio. Kwa kuliendeleza na kuhatarisha kibarua cha huyu mtanzania ndiko kunakoonyesha kiburi chake.

Badala ya kumuuliza huyu Bw. Mnaku kama anamjua yeye ni nani ni bora kwanza ajiulize mwenyewe kama anajua huyo Mnaku ni nani? Huyu ndiye ambaye waziri aliapa kumtumikia. Ni kwa niaba ya huyu Huyo Mnaku ndipo Rais alipomteua yeye kuwa waziri ili amtumikie vyema zaidi. Ni huyu Mnaku ambaye anaweza kuathirika na maamuzi yote yote potovu ambayo yeye na waheshimiwa wenzake wanayoweza kufanya kwa niaba yake. Huyu Mnaku ndiye bosi wake, zaidi ya huyo aliyemteua. Wengi wanalisahau hili.

Amandla....
na tena angejiuiza huyu mlinzi si ananilinda mimi na hizi milioni nianazozichukuwa. Hivi angechukua hizo milioni halafu akapigwa bao nje ya hiyo ATM si angesema Mlinzi alikuwa hafanyi kazi yake na menginene mengi. tehe tehe...
 
waziri ana mambo mengi jamani. ukichukulia pia wizara anayoiongoza ni mzozo mtupu. wakati mwingine dogo (ngeleja) hana makosa. kuna maamuzi anashindwa kuyafanya kutokana na kupewa shinikizo na wakubwa wake wa kazi hivyo kuhamishia hasira kwa wengine. hiyo inaitwa internecine violence. huwezi kujua pale ndani ya ATM alikuwa anazungumza nini na nani. labda pale palikuwa ni sehemu ya usalama zaidi kuzungumzia hiyo ishu, na ndio maana akawaka sana. hivyo kabla ya kulaumu sana tujaribu na kujenga picha akilini kujua ni nini huyu bwana alikuwa anawaza na aina ya kazi yake pia. ni hayo kwa sasa
 
Alikuta MGAO haujaingizwa kwenye account yake, akaanza kuulizia kwa simu, mwisho hasira zikaishia kwa mlinzi
 
Back
Top Bottom