Kisa cha Profesa na Mvuvi

Kisa cha Profesa na Mvuvi

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,318
Reaction score
12,824
Profesa Sabinus Brarugabwa wakati akifanya utafiti alikuwa akivuka mto Kiwira kwa mtumbwi wa kukodi...wakati akivushwa kwenye mtumbwi huo wakawa wanapiga stori na yule Nahodha wa mtumbwi...Mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
PROFESA: Vipi uliwahi kwenda shule
NAHODHA WA MTUMBWI: Hapana
PROFESA: Oooh! umefeli maisha
NAHODHA WA MTUMBWI: Sio hoja, maisha sijafeli si unaona naishi kama hivi.
PROFESA: Una uelewa wowote kuhusu Baiolojia ya mwili wako?
NAHODHA WA MTUMBWI: Hapana.
PROFESA: Ehee! ushapoteza asilimia 60 ya maisha yako.
NAHODHA WA MTUMBWI: Kufa tutakufa tu.
PROFESA: Unaelewa namna mtumbwi huu unavyofanya kazi, na je unaelewa kanuni zinazowezesha mtumbwi huu kuelea.
NAHODHA WA MTUMBWI: Hapana
PROFESA: Ohoo ushapoteza asilimia 20 ya maisha yako.

Baada ya stori...ghafla dhoruba ikatikisa mtumbwi ukapinduka...

PROFESA: Aisee nibebe mgongoni nazamaa! nakufaa!
NAHODHA WA MTUMBWI: Je unajua sayansi ya kuogelea ili usife.
PROFESA: Hapana.

SOMO: Usiidharau kazi yoyote au ujuzi wowote alionao binaadamu mwenzako kwa sababu kwa wakati husika huo ujuzi wako haumsaidii yeye chochote...muhimu ni kwamba binadamu tunategemeana.

Yule Nahodha wa mtumbwi alimuokoa Profesa akampa vidonge vyake...baada ya kumtapisha vikombe alivyokunywa mle ndani ya mto...
1.jpg
 
View attachment 1023150
Asante kwa funzo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom