Profesa Kabudi, Tundu Lissu na Kisa cha “Msomi Mshamba

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
_Na Masondore Masondore, Canada_

Katika gazeti la Tanzania Daima toleo la Jumatano Machi 6, 2019, ambalo sasa naliona limeamua kugeuka kuwa kikaragosi cha Tundu Lissu kuandika kila aina ya utumbo dhidi ya nchi yake, nimeshangaa sana kusoma habari isemayo *“Lissu Amgonga ‘Nyundo’ 13 Waziri Kabudi.”*

Toleo hili na andiko hilo ni kitu kingine cha kuisikitikia taaluma ya uandishi wa habari hapo nyumbani; imeshuka, imeporomoka kwa kiwango cha wanahabari hawaulizi maswali, hawana habari sasa ni mwendo wa kupokea tu kila kinachosemwa na Wanasiasa.

Nimejitahi sana kuzitafuta “nyundo” katika habari hiyo na kubahatika tu kukutana na udhaifu wa kiwango cha kihistoria katika ujenzi wa hoja na usanifu wa hoja zenyewe. Nazidi kupata wasiwasi, kama “nyundo” hizo ni kweli ameandika Tundu Lissu, basi tuendelee kumwombea sana ndugu yetu huyu azidi kupona, arejee katika hali ya kawaida tena.

Maana kwanza, pamoja na kujinasibu kuwa na “nyundo” 13, unaposoma makala hiyo hakuna hizo hoja 13 zaidi mhariri na Lissu wake kuhangaika kutajataja tu jina la Prof. Paramagamba Kabudi. Kimsingi andiko hilo lina masuala (na hoja) matatu pekee. Nimeona nishiriki katika mjadala huu.

*Kwamba Prof. Kabudi Hajui Sheria!*

Hii ni hoja ya kwanza na inayoonesha udhaifu wa pande zote; aliyeitamka na aliyeichapisha bila kuihariri.

Na hapa nitangulize mapema kuomba tuwasamehe wote hawa wawili maana kuna maradhi yamewashika.

Sisi tunaomjua Profesa Kabudi, tunafahamu kwamba usomi, uwezo na ujuzi wake katika sheria hauna shaka na hahitaji utambulisho katika taaluma ya sheria; he is just one of our own finest Professors of Law.

Lakini Prof. Kabudi ni zaidi ya Profesa wa sheria. Hata kama ingetokea akawa si Profesa, usomi, weledi na umanju wake katika sheria si tuu unashadidishwa na GPA ya daraja la kwanza aliyoipata lakini tazama:

Mosi, Lissu anamzungumzia Kabudi mwanafunzi bora wa mwaka wa kwanza katika kitivo cha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1980/81);

Pili, Lissu anamzungumzia Kabudi mwanafunzi bora zaidi wa mwaka wa pili UDSM aliyekuwa na alama nyingi kuliko wote katika somo la taaluma za maendeleo (DS) mwaka 1982;

Tatu, Lissu anataka kubishana na uwezo wa Kabudi mwanafunzi bora akiwa na alama za juu kuliko wote katika somo la sheria za kimataifa (international law) UDSM mwaka 1983?;

Nne, Lissu anamdharau Kabudi mwanafunzi bora wa mwaka 1983 kwa kuwa na alama za juu katika wanafunzi wa mwaka wa tatu mwaka 1983?;

Tano, Lissu anajua anajidharaulisha kumbeza Kabudi mwanafunzi bora wa mwaka wa mwisho katika kitivo cha sheria UDSM mwaka 1983?;

Sita, Lissu anafahamu kwamba anataka kujiweka mstari mmoja na mwanafunzi wa PhD ambaye akiwa masomoni nchini Ujerumani aliweka rekodi ya kuwa mmoja wa wanafunzi wachache wa kimataifa waliomudu kutetea tasnifu yao kwa kutumia lugha ya Kijerumani?

Nadhani katika udhaifu wa maneno ya Lissu katika hili, niseme tu inatosha kuhitimisha kuwa Lissu anaposema Profesa wa sheria tena wa aina ya Kabudi hajui sheria si kumshusha Profesa ni kujishusha yeye na kuzidi kujimaliza kisiasa kwa sababu Kabudi ni manju asiyepingika katika sheria na pia sheria za kimataifa.
*Kwamba Kuna Tofauti Kati ya Nchi na Serikali!*

Hapa ndio utacheka mpaka basi. Lissu kachomoka na vifungu kadhaa vya Katiba ikiwemo ile ibara 1(2) inayoeleza eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mipaka yake akionesha Prof.

Kabudi eti hajui tofauti ya nchi na Serikali. Hapa kaonesha udhaifu mwingine mkubwa; kukosa umakini wa kusikiliza na kuelewa.

Prof. Kabudi hakuna mahali popote katika hotuba yake alijadili dhana ya nchi na Serikali. Namfahamu Prof.

Kabudi kwa sababu hata tasnifu yake ya shahada ya umahiri (masters) aliyoifanya katika eneo la sheria za kimataifa amechambua sana masuala ya muundo na juriprudensia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Prof. Kabudi amekuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za Kimataifa UDSM kwa miaka mingi, ameandika sana, kufanya utafiti sana na hata kushiriki sana katika maendeleo ya eneo hili la sheria hivyo anaufahamu vyema mjadala wa hadhi na nafasi za nchi na serikali katika sheria za kimataifa.

Hoja ya msingi ya Profesa Kabudi akiwa Ikulu ilikuwa wazi, ni kwamba iwe unatukana nchi au Serikali yako ukiwa nje ya nchi yako, unalipaswa kujua (hakumtaja Lissu lakini kashajihisi) ni kwamba unaowachafua ni viongozi wa nchi yako na unayoichafua ni taswira ya nchi yako.

Sasa cha ajabu Lissu anayejifanya kujua kila kitu kavamia mjadala usio wake na sasa anazidi kutia aibu.

Maana hata dhana aliyokuja nayo ili tu kumkosoa Prof. akijitahidi kutofautisha nchi na Serikali nayo imesheheni upotofu.

Lissu anataka tuamini kuwa neno nchi (state) na serikali (government) kuwa ni vitu viwili tofauti katika taswira ya kimataifa.

Kwa kweli hapa katia aibu wasomi wa sheria. Katika mawanda na muktadha wa Prof. Kabudi aliyekuwa akijadili umuhimu wa kulinda taswira ya nchi yetu kimataifa, Lissu, kwa mara nyingine tena si tu katia aibu bali kaudanganya umma!

Kwa mujibu wa tafsiri ya Mkataba wa Montevideo wa mwaka 1933 na ambayo imekubalika kimataifa, neno nchi (state) moja ya moyo/sifa/vigezo vyake ili ikamilike ni uwepo wa Serikali.

Hivyo nchi katika sheria za kimataifa huwezi kamwe kuitenganisha na Serikali na hapa hoja nyingine ya Lissu inaanguka kwa aibu. Ibara ya 1 ya Mkataba wa Montevideo inasema:

“The state as a person of international law should possess the following qualifications: a. permanent population b. a defined territory c. government and d. capacity to enter into relations with other states.”

Hivyo Prof. Kabudi yuko sahihi, huwezi kuchafua nchi, ukasema haujachafua serikali husika katika nchi husika kwa wakati huo. Vile vile, huwezi kuitukana na kuichafua Serikali ukasema haujaichafua nchi.

*Kuropoka, Kukashifu VS Uhuru wa Mawazo*

Ukisoma makala hiyo ya Tanzania Daima utashangazwa na kushuka kwa kiwango kikubwa kwa uwezo wa Lissu katika ujenzi wa hoja. Bado natafakari kama makala hizi anaandika au kwa sababu ya hali yake iliyomsibu anaandikiwa.

Nimemuona Lissu akijenga hoja kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania kuwa ana haki ya uhuru wa mawazo akionesha kuwa onyo la Profesa Kabudi halimhusu yeye kwa sababu ana kinga hiyo ya kikatiba.
Ni aibu lakini twende naye hivyo hivyo, hatuwezi kumkana mwenzetu.

Kwanza niseme Katiba ya nchi yoyote haifasiriwi kama anavyotaka kutuaminisha leo Lissu. Kwamba kwa sababu Ibara ya 18 imesema ana uhuru wa mawazo basi tuishie hapo. Hapana. Katiba inajitafsiri. Iko wazi.

Ukiisoma ibara ya 18 aliyoitumia Lissu inakupasa pia uende katika Ibara ya 30 inayoainisha ukomo wa haki mbalimbali zilizoainishwa.

Haki za kikatiba zina ukomo kwa lengo la kulinda haki za wengine na zaidi usalama na ustawi wa Taifa. Ndio maana ibara ya 30(1) inasema:

*“30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.”*

Lakini kama nilivyosema awali, Prof. Kabudi, alikuwa anazungumza katika muktadha wa kimataifa.

Lissu kama alitaka kusanifu hoja yake vyema alipaswa, kabla ya kupingana na Prof. Kabudi, ajiulize huko nje anakoropoka, kutukana na kukashifu viongozi, taasisi na nchi yetu, Je, sheria za kimataifa zinamkinga?

Jibu ni hapana. Katika sheria za kimataifa za haki za binadamu uhuru wa mawazo umesisitizwa sana (nenda ibara ya 18 ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na Ibara ya 19[1] ya Mkataba wa Kimataifa Kuhusu Haki za Kisiasa na Kiraia, 1966).

Lakini si Prof. Kabudi, bali mikataba hiyo hiyo ya kimataifa, imeweka ukomo katika mtu kufaidika na haki zake ikiwemo ukomo katika mtu kusema chochote. Ibara ya 19(3) ya Mkataba wa mwaka 1966 nilioutaja hapo juu inakataza, huwezi kuropoka chochote tu popote na kukashifu watu/taasisi, ukaingilia faragha, ukaharibu usalama wa nchi na ustawi wa jamii.

Hapa Canada miaka kadhaa iliyopita Mahakama zimepata kuamua kuwa kutusi au kudhalilisha wartu wengine ukiwa nje ya mipaka ya nchi hakuondolei kuwajibika kisa anatekeleza haki yako ya uhuru wa mawazo/kujieleza.

Uamuzi huu unaogusa pia namna nchi zinavyopaswa kuratibu makosa mitandaoni umo katika kesi mashuhuri hapa Canada ya kwenye Mahakama ya Rufaa ya Ontario katika Breeden Versus Black ([2012] 1 S.C.R. 666).

Na hili Lissu alielewe vyema, sio Prof. Kabudi anayemnyamazisha bali sheria za kimataifa na pia ajue Mahakama katika nchi nyingi duniani zimechukua hatua kwa waropokaji kama yeye kwa sababu ya kanuni hii hii kwamba uhuru wa habari haumaanishi haki ya kutukana, kudanganya, kudhalilisha au kukashifu.

Mwaka 2000 hapa Canada tena aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Serikali za Mitaa katika Jimbo la Ontario, Tony Clement, alimfungulia mashtaka ya kashfa aliyekuwa kiongozi wa Chama Upinzani cha Liberal, Dalton McGuinty, na kumdai Dola za Kimarekani milioni 1.7.

Msingi wa kesi hii (_Clement v McGuinty_) ni kitendo cha Bw. McGuinty, kama anavyofanya Lissu sasa, kuropoka katika mahojiano mbalimbali ya redio, akimtuhuma Bw. Clement kwa rushwa.

Alipoona kesi imemkalia vibaya na kwamba aliripoka tu hakuwa na ushahidi hatimaye mwaka 2001 McGuinty aliomba radhi na kulipa gharama za kesi Dola 75,000.

Kwa muktadha huo, Prof. Kabudi yuko sasa kuwaonya aliowaonya kuwa wakae kimya (hakumtaja Lissu).

Wenye busara watakaa kimya. Wehu wataongeza kelele lakini siku yakiwafika wasilalamikie sheria. Sheria ni msumeno.

Nimemsikiliza sana Lissu katika hotuba zake akiwa nje ya nchi, nimefuatilia sana anachokisema. Naungana naye kuwa akiwa raia anazo haki kusema masuala kadhaa ya nchi au serikali yake kwa nia ya pale anapoamini kuna changamoto zifanyiwe kazi. Naungana naye katika hili.

Hata hivyo, labda kwa tatizo lile lile, Lissu hatoi maoni ya kuijenga nchi yake wala hata hiyo Serikali yake, anatoa maoni yaliyosheheni kashfa, upotoshaji, dhihaka, uongo na kuwadhalilisha viongozi wa kitaifa na jina la nchi ya Tanzania.

Nitakupa mfano: Akiwa kwenye kipindi cha Hard Talk Uingereza ametuhumu viongozi wanaohama kutoka Chadema kwenda CCM kuwa wanahongwa hela. Alipotakiwa kuthibitisha hakuwa na ushahidi.

Akaulizwa kuhusu mageuzi yanayoendelea katika sekta ya madini na makubaliano ya awali kati ya Serikali na Barrick, akaropoka na kusema uongo kuwa hakuna makubaliano yoyote.

Ushahidi ukatolewa kuhusu makubaliano ya Oktoba, 2017 hadi leo hajarudia tena neno lake la kipumbavu eti “there is no any deal!”

Akiwa Marekani akamtuhumu wazi wazi Rais Magufuli anawaweka ndani wapinzani na akataja mfano wa Kiongozi Mkuu wa Upinzani, Freeman Mbowe kuwa eti kafungwa jela.

Balozi Masilingi aliyekuwepo akafafanua kwa kumpa Lissu darasa la tofauti ya Mbowe ambaye yuko mahabusu tena kwa yeye mwenyewe kuvunja masharti ya dhamana na mtu aliyefungwa jela, akafaidhaika sana.

Mahojiano aliyoyafanya sasa yamebainisha ni mtu mwongo mkubwa, mzandiki mkubwa ambaye bahati nzuri sasa wazungu aliodhani atakuwa akiwadanganya, chini kwa chini wanafuatilia mambo, na kubaini ukweli. Mzungu mmoja nikiwa Quebec wiki iliyopita aliniuliza huyu mtu ni mzima? Natafuta jibu bado la kumtetea mtu wa aina ya Lissu.

Niseme tu Lissu, akiwa Mtanzania kama wengine, anaweza kuwa na hoja zake kuhusu Serikali au nchi yake, sisi sote tulioko nje tunao ndugu huko Tanzania na zipo sehemu kuna changamoto, nyingine zimetatuliwa nyingine bado lakini hatuwezi kuwa huku tukawa mawakala wa kuitukana na kuidhalilisha nchi yetu. Hakuna sababu. Ukionewa fuata sheria.

Tanzania ina sheria nzuri tu za mtu anayeamini kakosewa haki zake na Serikali kufungua shauri kudai fidia. Kwa nini Lissu hafungui kesi hiyo badala yake azunguke duniani kuzurura tu na kutukana nchi?

Aidha, mpaka Novemba, 2018 Tanzania pia ilikuwa ni miongoni mwa nchi tisa (9) tu za Afrika zilizokubali kwa hiari yake kuruhusu raia wake waishtaki Serikali kwenye Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika na tayari zipo kesi Serikali ya Tanzania imeshindwa katika Mahakama hiyo.

Kitendo cha Lissu na mwingine yeyote, kuacha utaratibu wa kisheria na kwenda nje ya nchi si kutoa maoni ya haki bali kumkashifu Rais wetu, taasisi zetu, wataalamu wetu na kila kinachomjia mbele yake kuhusu Tanzania nakubaliana na wengi kuwa ni uzandiki na usaliti.

Unapokwenda kulalamika katika nchi kama Marekani kuwa umepigwa risasi kwa hiyo Tanzania nzima haina demokrasia ni ya kidikteta, au haifai kushirikishwa katika maendeleo ya uchumi watu wanashindwa kukushangaa kwa sababu hata katika Marekani yenyewe wengi tu si kupigwa, wameshauawa kwa risasi lakini ndugu hawatoki nje ya nchi kuitukana nchi yao.

Nilipoisoma makala moja kuhusu idadi ya watu waliouawa kwa risasi nchini Marekani alikokwenda Lissu kulialia na kuwa nako vimeongezeka hadi kufikia watu 40,000 mwaka 2018, nilijikuta namsaidia Lissu kuona aibu. Soma hii: Gun deaths in US rise to highest level in 20 years, data shows

Hali ni kama hiyo pia ipo hapa Canada ambapo mwaka 2017 vifo vya watu kuuana kwa risasi vilifikia kiwango chake cha juu kuliko wakati wowote katika kipindi cha miaka 25 ambapo watu zaidi ya 200 waliuawa kwa risasi. http://time.com

Ndio maana ninapoyatafakari ya umanju wa Kabudi na udhaifu wa Lissu inanijia kumbukizi ya kisa cha zamani enzi za wanafalsafa wa Kigiriki na ambacho kilirudiwa kama mjadala katika makala moja ya kisomi ya Prof. Issa Shivji kuwa kuna Msomi Makini (Intellectual) na Msomi Mshamba (Barbarian Intellectual). Namuona Lissu akihamia kundi la pili.

Alamsiki.

_*Mwandishi wa makala haya ni Mtanzania aishie nchini Canada ambaye pamoja na maeneo mengine ya kisera na utawala bora, pia ni mtaalamu katika sheria za kimataifa.*_

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hongera kwa kuandika! Umemsifia sana Prof.Kabudi au ni wewe Kabudi maani hujawa verified? weka namba ya simu Kabudi atakukumbuka akiwa kimataifa zaidi hongera sana
 
Nilidhani anajibu yeye kumbe mawaidha ya mtu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lissu vs the whole world. yet, he conquers all before him.

kubalini tu kuwa hii vita yenu dhidi ya Lissu mmeshindwa kabla hata hamjaianza!
 
Sijataka hata kuumaliza kusoma nilipoona mautumboutumbo.Wewe sijajua unamuongelea Prof.Kabudi yupi?Mana huyo uliyeanza kwakumsifia alikuwa ni Kabudi yule wa Tume ya Warioba.Huyu wasasa nikibaraka tu wa Aliyemchagua.Chukua muda umchunguze utajua huyu siye Kabudi unayemuongelea Wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
:D:D Tungekuwa tulimjengea Sanamu, basi leo hii tungeenda kubomoa.
Sasa nimegundua kwanini Kanisa Katoliki humtangaza mtu mtakatifu baada ya kufariki na sio akiwa hai.
 
Ni Kabudi mwenyewe. Mbona unajitahidi sana kutuaminisha kuwa imeandikwa nchini Canada? Binafsi maisha Tanzania na Canada na yeyote aishie Canada angeandika jimbo na si "Canada" tu. Hujawahi kuishi Canada, unaisikia tu.
 
Kwa ufupi kwa mnaoona ndefu.

Jamaa anashangaa Tanzania Daima kusema Lisu katoa Nyundo 13 wakati yeye kaziona tatu.

Amesema Lisu kusema Kabudi hajui sheria ni kujidhalilisha.

Amesema kupigwa risasi na kwenda kusema sema hovyo nje wakati Marekani na Canada mauaji kwa risasi yapo juu ni kua kituko.

Hapo akamkumbuka Shivji aliyesema kuna msomi makini na mshamba, na Lisu ni msomi mshamba.
 
Inaonekana umeandika kiushabiki, kushabikia serikali bila kujua kinachoendelea nchini. Nadhani uko nje ya inchi kwa muda mrefu. Kwanza ungejibu hoja zake za kutaka kuuawa na kunyimwa matibabu na kesi ya kutaka kuuawa kutotolewa majibu. Juzi tu rais alishangaa kesi yakutekwa MO, ya Lisu kimywa????
 
Back
Top Bottom