Uchambuzi na Majibu: Kitabu cha Mkapa my life my Purpose by Padre Privatus Karugendo

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,456
KITABU CHA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN WILLIAM MKAPA.

Nimefurahi sana kumaliza kukisoma kitabu cha Mheshimiwa Rais wa awamu ya tatu ya uongozi wa Taifa letu la Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa: My Life, My Purpose; A Tanzanian President Remembers.

Nilitamani sana kukisoma kitabu hiki kilipotoka, lakini bei yake kubwa sikuweza kukinunua, na sifikiri kama kweli hiki ni kitabu cha watu maskini watu pembezoni, kama anavyowataja yeye mwenyewe kwenye kitabu chake. Binti yangu mwenye kazi yake nzuri, aliponitembela kwangu, alikuja na kitabu hiki, hivyo nikapata nafasi ya kukisoma. Nilipokishika sikukiweka chini hadi nikakimaliza.

Ni kitabu kizuri sana, lugha yake ni nyepesi na kinasomeka kwa urahisi kabisa. Mheshimiwa Mzee Mkapa, ameadika kwa uwazi kabisa juu ya maisha yake.Hata mambo ambayo tulifikiri ni stori tu za kutungwa, yeye ameyaongelea na kuyaelezea kwa undani kabisa, sakata la EPA, uhusiano wake na profesa Mahalu, Kiwira, Kombe, Mikopo ya Benki, Ubinafsishaji, Kiburi chake, uhusinao wa kimapenzi yaliyofanikiwa kama ya Mama Anna, na mengine ambayo hayak ufanikiwa, na mengine mengi ambayo wengine wangeficha kuyasema.

Nilitamani nimpongeze na kujadiliana naye mambo machache. Lakini kwa mfumo wetu wa sisi wananchi na viongozi wetu, si rahisi kupata nafasi hiyo. Wao wako juu kule na sisi tuko chini kule. Ingawa ni viongozi wetu lakini mfumo wa kukutana nao na kujadiliana nao ni wakikoloni kidogo.

Sina uhakika kama hiki ninachokifanya hapa kuwasiliana na Mheshimiwa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, kwa njia hii ya mitandao ya kisasa ni sahihi au hapana. Lakini kwa heshima na unyenyekevu mkubwa ni lazima niandike kitu, ni wazi ukishaandika kama alivyofanya yeye huwezi kukwepa maoni: Kilichoandikwa kimeandikwa ni lazima kitajibiwa tu! Kisipojibiwa leo, ni kesho au keshokutwa; Mungu akikupenda sana, basi kinajibiwa wakati wa uhai wako! Nina uhakika ujumbe huu utamfikia Mheshimiwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa.

Mbali na pongezi nyingi za uandishi mzuri uliotukuka, nina machache kwa Mzee wetu Mkapa;

1. Hiki kitabu umewaandikia watanzania wa Lupaso, Ibwera, Magu, Mto wa Mbu na kwingineko Tanzania? Au unawaandikia watu wa nje wa Ulaya, Amerika na kwingineko Afrika? Baada ya kuiongoza Tanzania kwa miaka kumi, na kufanya kazi za Utumishi wa Umma kwa miaka mingi, ndani ya nchi; unaandika kitabu kwa lugha ya Kigeni? Ni watanzania wangapi watakisoma na kukielewa? Uliyekuwa kiongozi wa nchi, wananchi waswahili, unawaandikia kwa lugha ya kigeni? Hili sikulielewa! Si vibaya kuandika kwa lugha ya kiingereza amacho unaweza kujielezea vizuri, lakini nafikiri ungeaandika kwanza kwa Kiswahili, na baadaye wakatafsiri au wewe ukatafsiri kwa kiingereza.

2. Umekuwa ni mtu unayewalaumu sana waandishi wa habari wa Tanzania. Unataja kwenye kitabu chako kwamba wewe ulipoteuliwa kuongoza Magazeti ya Chama, Mwalimu Nyerere, alikutuma Uingereza, kusoma na kujiandaa vizuri ili uje kongoza magazeti ya chama. Bahati mbaya katika kitabu chako sikuona unataja popote kwamba uliwaandaa waandishi wa habari wa Tanzania kama wewe ulivyoandaliwa na Mwalimu. Au kuonyesha kwamba tasinia hii ya Uandishi wa habari ulifanya jitihada ipi ya kuiboresha kama ulivyofanya kwenye senkta nyingine nyingi.

3. Kati ya sababu ulizozitaja kutaka kugombea Urais, ni kuvifufua vyama vya ushirika na vyama vya wafanyakazi. Bahati mbaya hukutaja kwamba Mwalimu, alikosea kuviingilia vyama hivi vya ushirika. Unakumbuka kwamba Chama cha Ushirika cha Nyanza, wakati ule kilikuwa ni chama cha ushirika duniani chenye fedha nyingi. Wasomi unaowasikia Bukoba, Mwanza na Moshi, walisomeshwa na vyama hivi vya ushirika.

Vyama hivi vilikuwa na uwezo wa kuwasomesha wanafunzi ndani na nje ya nchi, vyama hivi vilikuwa na miradi mikubwa ya kuzalisha fedha. Vyama hivi vilikuwa na mfumo mzuri saaana wa kujiendesha na vilikuwa na nguvu kubwa. Ni wazi, Mwalimu, alikuwa na lengo zuri, maana bila kuvidhibiti vyama hivi vingeleta shida labda umoja wa kitaifa ungekuwa mgumu. Kosa kubwa lililofanyika ni KUINGIZA SIASA kwenye vyama hivi. Ikafikia hatua kwamba huwezi kuwa mwenyekiti wa chama cha Ushirika bila kuwa Mwanachama wa CCM.

Fedha za vyama hivi zikatumika kwenye siasa, viongozi wa vyama hivi wakateuliwa kufuata uanachama wa CCM, zaidi ya kuwa ni wakulima. Walichaguliwa watu ambao kwa mfano hawakuwa wakulima wa kahawa, korosho au chai. Kwa njia hii vyama hivi vimekufa kabisa na kuvifufua ni tatizo kubwa, hadi pale ikiondolewa siasa, vikajiendesha, kazi ya serikali ikawa ni kuviwezesha kwa kuvipatia wataalamu mbali mbali.

Vyama hivi ni msingi mkubwa wa maendeleo ya taifa letu. Jambo hili umeliacha hewani kwenye kitabu chako na hukupenda kuonyesha wazi kwamba chama chako cha CCM ndicho kimevivuruga vyama hivi vya ushirika. Mtu kama wewe ukilisema hili litasisikika.

4. Katika kitabu chako unasema huwezi kukumbuka yote, hii ni kweli. Ingawa umejitahidi saana, kukumbuka mengi. Ni wazi ulianzisha mambo mengi sana PCB, TASAF, MKUKUTA, MKURABITA na mengine mengi. Ila kuna mambo ambayo hukutaja kabisa, sina uhakika ni kuyasahau:

5. Mfano Msamiati wa kibaguzi wa Uhamiaji haramu, na kunyosheana kidole cha uraia, uliuanzisha wewe. Kwa mara ya kwanza katika taifa letu, kusikia mtu si raia, mtu ambaye ameshika nafasi za uongozi na kufanya mengi kwa taifa hili, kusikia kwamba si Mtanzania, ulianzisha wewe.

Nilitegemea uandike mistari miwili mitatu juu ya utamaduni huu Mbaya kabisa. Na sasa umekuwa ni utamaduni wa kudumu na silaha ya kuwanyamazisha watu.Mtu anayekosoa, au kuwa na mawazo tofauti, utasikia wanaema huyu si raia. Tulishuhudia Bwana Jenelali Ulimwengu, Amani na Bandola, labda huyu wa tatu nimekosea jina, alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria? Kitu kama hicho.

Tukasikia si raia! Mwalimu Nyerere, alikaribisha watu wengi hapa Tanzania, na wengine tunaambiwa waliendelea kutumia Hati zetu za kusafiria hadi wamekuwa Marais wa nchi zao. Lakini mipaka yetu pia ilivyo, mfano kule kwetu Kagera, kama mtu hana chimbuko la Burundi, Rwanda na Uganda, huyo si mwenyeji wa Kagera. Pia na wewe unataja kwenye kitabu chako kwamba mlivuka mto kutokea Msumbiji.

Hivyo nilitegema, uonyeshe kuguswa au kukubali kwamba uliteleza kwa hilo la kuanzisha utamaduni hu mbaya kabisa katika Taifa letu na katika jitihada za kujenga Shirikisho la Afrika mashariki na Umoja wa Afrika. Sipendi kuamini kwamba hili umelisahau? Inawezekana mlitofautina na rafiki yako Bwana Ulimwengu, na wala hili sitaki kuliingilia, wewe ni binadamu, unaweza kukosea au kukosana na mtu; ila hili la kuwabagua watu ambao tumeishi nao kwa muda mrefu ambao ndugu zao wote ni Watanzania, lakini wao tu kwa sababu fulani za kisiasa si watanzania si la kufumbiwa macho au kusema umelisahau, si mtu kama wewe!

6. Jingine ni lile la wakimbizi wa kutoka Rwanda, waliokuwa kwenye Kambi za Karagwe, walivyofurushwa na kuswagwa na Jeshi letu hadi kurudi kwao, nafikiri ni mwaka 1997? Nilishuhudia mimi mwenye tukio hilo, watu walitembea kwa miguu zaidi kilomita 200 kwa miguu, wanawake walijifungua barabarani na wengine walikufa njiani. Ninajua lengo lako lilikuwa zuri kwa pande zote mbili, kwa Rwanda na kwa Tanzania, lakini jinsi tukio hilo lilivyotekelezwa halikuwa zuri. Nilifikiri ungeliligusia hili na kuonyesha kuumia au kwamba uliteleza pia! Siwezi kuamini kwamba hili umelisahau, au si la maana! si mtu kama wewe!

7. CCM na “Utanzania”. Wewe ulikuwa mwenyekiti wa CCM, unajua kwamba kuna kuchanganya vitu hivi viwili. Kuna wanaofikiri kwamba kuwa Mtanzania ni kuwa CCM, hivyo mtu kama si mwanachama wa CCM, ni sawa na msaliti. Ushabiki wa chama, majigambo ya chama, vimekuwa juu ya utaifa. Hii ni hatari na si nzuri kwa taifa letu. Huonyeshi kwenye kitabu chako, jitihada zako za miaka kumi kama kiongozi wa chama na Kiongozi wa taifa, za kuuondoa jambo hili na kuusimika “Utanzania”.

8. Unataja katika kitabu chako jinsi ndugu zetu Wahindi, wanavyofanikiwa katika biashara zao. Ukweli ni kwamba wao, maisha yote yameungana: Dini, siasa, uchumi, familia. Haya yote ni maisha yaliyoungana. Ni sawa na ile historria ya wana wa Israeil: Historia ya Mungu na watu wake.

Mipango ya Biashara ya wahindi inajadiliwa kwenye ibada zao; wanasaidiana, wanashauriana huko huko kwenye ibada zao. Sisi tulifundishwa na wamisionari kwamba ya Kazari mpe kaizari na ya Mungu, mpe Mungu. Hivyo tunatenganisha maisha ya dini na maisha ya kawaida. Tunakutana kanisani na miskitini, lakini kwenye maisha ya kawaida ya kila siku kila mtu yuko kivyake; hatuna mfumo wa kusahihishana, kuwajibishana, kuelekezana, kuinuana na kusaidiana kwenye ibada zetu. Ndiyo maana mafanikio yanakuwa ni mtu mmoja mmoja!

Na hili halina afya kwa biashara zetu, kwa miradi yetu ya kitaifa, kwa viwanda vyetu na kwa maendeleo ya taifa zima. Ni lazima tuwe na mfumo wa kuyaunganisha maisha yetu yote: Imani za dini, siasa, uchumi, familia… Historia ya Mungu na taifa lake la Tanzania. Nchi zote zilizoendelea duniani zina mshikamano huo, si lazima iwe ni imani ya dini ,lakini ni lazima kiwepo kitu cha kuwaunganisha watu kama taifa na kuwaingiza kwenye historia moja yao na Muumba wao na taifa lao.

9. Wewe pia hukuliona hili, nina mashaka kama unaliona hata sasa. Mwalimu Nyerere, naye hakuliona.Kushindwa kwake katika mipango yake ya kujenga Ujamaa na kujitegemea na kulisimika azimio la Arusha, hakuweza kuyaunganisha haya, au ilibidi ashike moja na kuacha jingine au ayashike yote mawili, lakini kwa mfumo wa dini nyingi tulizoletewa,hasingeweza kuyashika yote. Kama angetaka kufanikiwa, angefanya kama Cuba!

10. Wewe mwenyewe unashangaa saana, kuona kwa miaka 50 ya uhuru bado tunahitaji msaada wa kuchimbiwa vyoo kwenye mashule. Ulianzisha mambo mengi sana ya kuleta maendeleo lakini yalikwama. Ni kwamba tunahitaji Mfumo wa kuwaandaa watu. Uzalendo, uaminifu na kujituma, si vitu vinavyonyesha kama mvua.

Ni lazima Mfumo. Kama vile Mwalimu, alivyokuwa ameanzisha Cho cha Kivukoni, tatizo kikawa mshika mbili! Tunahitaji mfumo wa Kujenga Uzalendo, uwajibikaji na uaminifu. Tunahitaji mfumo wa kuunganisha maisha yote: Dini, siasa na Uchumi. Katika mfumo wa sasa wa dini nyingi tulizonazo, na zote dini za kigeni, mfumo wa ushabiki wa vyama vya siasa, ni shida sana kujenga mfumo huu ninaouongelea. Bila mfumo, bila kuwaandaa watu, bila kubadilisha fikra za watu, bila kujenga falsafa ya maisha yetu kama taifa, hatuwezi kuendelea kamwe!

11. Tunahitaji viongozi, ninafikiri kwa sasa vijana, ambao wamejikomboa kifkra, wanaitambua falsafa sahihi ya kutuongoza; falsafa ya kutembea na dunia ya leo ya Uchumi wa upole wa njiwa na ujanja wa nyoka, dunia ya kuishi na wanadamu wengine kama washirika na wala si wa kututupia mkate na kutujengea vyoo; dunia ambayo jiwe haliwezi kubadilika likawa nyoka, dunia inayoamini chanya na hasi, dunia ya sayansi na teknolojia, watuongoze na kutupeleka mbele.

12. Wewe ni shupavu, wewe unajiamini na wewe una msimamo, lakini kitabu chako umekiandika kwa unyonge! Nimeshangaa sana unakubali kuwa mnyonge! Unatupilia mbali ushawishi wako mkubwa kwenye taifa letu la Tanzania, unatupilia mbali uzoefu wako wa miaka mingi wa kulitumikia taifa letu, uzoefu wa kufanya kazi na baba wa Taifa. Unyonge wako unauficha kwenye maandishi haya ambayo umeyaandika kwenye lugha ya kigeni. Andika Kiswahili: Chimurenga..Ukombozi wa fikra..Mapambano yanaendelea.

Wasalaam,

Padre Privatus Karugendo.

+255 754633122

pkarugendo@yahoo.com
 
Asante mkuu kwa kutonesha kutokufaulu kwa mwandishi, tena aliyejiita mzalendo lakini akashindwa kuonesha uzalwendo kwenye lugha badala yake akaenda kutukuza lugha ya kigen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I

Ingelikuwa ni Ndugu Privatus Karugendo kapost mwenyewe, nami ningelikuwa na ya kumuuliza.
 
Uchambuzi mzuri kabisa wa kitabu cha Mzee Mkapa. Hivi kitabu cha Mzee wa Msoga kiko wapi? Kuna kipindi nilisikia anaandika kitabu kinaitwa From Barefoot Student to The President.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
matumizi ya kingereza kwenye vitabu vya Mkapa,Mengi na Nyerere ni kwamba Kiswahili hakina maneno ya kugusa? Hivi kweli wangeshirikiana na TUKI wangeshindwa kufikisha ujumbe
 
Mwanafunzi wake karithi upumbavu wa mwalimu wake. Kila anayemkosoa anachunguzwa uraia wake. Hovyo kabisa.
 
Kutonesha hujaliona? Kwa wengi ninao wafahamu wanapenda sana Kiswahili lakini hushindwa kujieleza vizuri bila kuweka na kimombo. Sizungumzii wale wa mbwembwe. Hapana. Wapo ambao hawapendi kabisa kiswangilish lakini hawawezi. Kwa dhati kabisa na bila ya mbwembwe.
Mkapa hata Kiingereza chenyewe kilimjua. Aliandika na kuongea kwa ufasaha. Alijua sana Kiingereza na alijisikia vizuri zaidi katika hiyo lugha. Sijashangaa kuandika kumbukizi yake kwa Kiingereza. Sioni kosa lolote. Uzalendo si lugha. Kuna nchi nyingi hazina lugha yao ya taifa lao lakini wazalendo wa kutupwa. Hilo la kukosa hiyo lugha kama huchochea uzalendo wao! Waswahili wanafiki na wasaliti wa nchi yao tunao si haba.
Nawashangaa ninyi mnaotaka hicho kitabu kisomwe na Watanzania wengi zaidi hamchukui hiyo fursa ya kutafsiri. Wasomaji wengi Tanzania wa kusoma kitabu kama hiki wanajua Kiingereza. Wasomaji wengine si aina ya vitabu vyao. Gazeti tu lenyewe angalia wanasoma riwaya za udaku na michezo na burudani. Waandishi wao sio akina Mkapa bali akina Shigongo! Tusidanganyane.
 
Back
Top Bottom