Kisa cha MwanaHALISI kufungiwa ni Habari ya "Nani anastahili kuombewa kati ya Lissu au Magufuli"

Mkuu kwa hilo mimi huwa napingana hadi na msimamo wa Jeshi,kuniita shujaa wakati sina mguu au mkono kisa nimepigana vita ya Uganda au DRC,mimi siuoni.We uliye mzima nyuma ya keyboard yako baada ya kushiba mchana pengine na moja ya baridi ndo shujaa kuliko hata Lissu.Ukiniambia kwa sasa hivi shujaa ni MBOWE nitakuelewa maana yupo anauguza wakati huo huo anakula bata NAIROBI.
Na maanisha kwenye medani ya propaganda nadhani kaeleweka vizuri kuliko serikali,kwa sasa GOT anapaswa kujinasua kwenye mtego umeenasa pabaya mtu wangu. Heshina imepotea lile jina muuu
 
Mkuu unapotosha halafu unazungumza mafanikio ya kuhadithiwa. Maisha ya wananchi wa kawaida bado ni magumu na biashara zao zinazidi kudoda. Ukweli halisi wa maisha ya wananchi wa kawaida hayajabadilika au yako vilevile. Sanasana kilichobadilika ni kiongozi kutoka JK aliyekuwa na lugha laini lakini aliyeshindwa kwenye rushwa kuelekea huyu wa sasa mwenye lugha za jazba na kejeli jamb anaonyesha kuichukia rushwa. Ukimuangalia na kusikiliza maneno yake ni mtu mwenye nia njema lakini asiyeamini kwenye uwezo au mchango wa mawazo ya wengine. Tabia hii inamjengea chuki ya wazi kwa anaotofautiana au kumkosoa kwani anaamini yuko sahihi. Halafu mnatokea nyie mnaoamini kwamba atalivusha taifa hili kwa yeye kutamka etu kuna vita ya kiuchumi.

Kwa taarifa yako sioni ndoto za jamaa zikifanikiwa sasa au hata mkimuongezea miaka 7 kwani dunia ya sasa ili ufanikiwe sio lazima ukunje ndita na kofokea watu kwa kisingizio cha uzalendo. Halafu ogopa sana mtu anayeanza uzalendo wa chuki baada ya kukwaa madaraka ya juu kabisa. Hayo matatizo ya wanyonge unayosema yanatatuliwa ni yapi mpaka ajenge chuki ya wazi dhidi ya wanaomkosoa? Maendeleo yaliyopatikana chini ya utawala wake ni kama ya watangulizi wake hakuna cha ajabu. Kulinda raslimali zetu ni sawa ila hakuwahi kufanya hivyo huko nyuma hivyo kwake ni hatua iliyochelewa. Je hao walioingiza taifa hili kwenye mikataba ya wizi walipigwa risasi? Kwanini apigwe risasi ambaye hakuwa kuingiza nchi yetu kwenye mikataba na waliongiza nchi kwenye mikataba hiyo wakiwa kimya? Au kwako ww chuki na Unyama ndio sifa ya utendaji wa serekali?
Mkuu naheshimu mawazo yako na nakupa heko kwa kujaribu kuwa neutral.Kwanza JPM asingeweza kupiga kelele zozote kuhusu madini akiwa waziri wa kawaida,matokeo yake CCM wangeogopa hata kumpitisha kugombea kiti cha uraisi.Na huyu Lissu siku zote ambazo anaita media au kwenye tweeter zake hakuna siku hata moja amewahi kukubali au kupongeza jambo lolote alilowahi kufanya JPM,hii inakupa picha gani?,wewe mbona kuna mahali hapa umekubali mazuri au nia nzuri ya JPM?.. hii haikuwahi kuwepo kwa Lissu,,kuhusu kupigania madini huko nyuma,sote tunakubali alikuwa mpiganaji mzuri,sasa tulitegemea kipindi hiki aungane na serikali huku akitoa maoni kistaarabu namna ya kuendeleza mapambano,.,hivi mtu akikutishia TUTANYOLEWA KWA CHUPA,unapata picha gani?,mtu anaposimama mbele ya vyombo vya habari akasema tuna SERIKALI YA OVYO inaleta picha gani? serikali ya ovyo unamaanisha Jeshi la ovyo,polisi ovyo,magereza ovyo,mahakama ovyo,na taasisi zote za serikali ovyo.,hii ni SAWA?,.Katika wanasiasa na wanaharakati wote wa dunia hii ukianzia na akina Nyerere,Sokoine,Mandela,Kwame Nkhuruma,Odinga na wengine wote,nipe mfano wa aliyekuwa na lugha kama za Lissu aliyepata mafanikio na kufika mbali?,tatizo hamtaki kukubali Lissu alizidiwa na jeuri na kitu inaitwa kujifanya ni mjuaji sana pengine kuliko mwanasiasa yeyote TZ na nyie mkawa mnampamba kumtia ujinga.
 
Nibora wangelikuwa wapuuzi hata Mia 7
Walau sasa huyo Lissu awe zaidi ya Rais kweli!

Ulivyo na gundu umetupia coment kwenye uzi wa diamond sio ya kisiasa bado watu wamekufukuza mjipime uwezo wenu wa kufikir na maandiko yenu mnajizalaulisha.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Naona umethibitisha kwa kauli yako kuwa waliompiga Lissu ni serikali iliyopo madarakani au? Kama uliandika bila kufikiria muda unao futa au rekebisha comment yako haraka
 
Get well soon Mr president expected TL
Dr kahitila hongo mwenyekiti wa ACT wazalendo morogoro, amesema angependa mpaka anafariki yeye awe anamuona magufuli akiwa rais wa NCHI hii,

Huo ni mwendelezo wa wale wanaoona Tanzania hakuna mtu mwingine wa kuongoza ispokuwa magufuli,

Ikumbukwe kampeni ya magufuli baki ilianzishwa na mmoja wa ma DAS , Asenga Abubakari, ikafuatiwa na kauli ya Mzee Mwinyi, na watumishi wa serikali RAHCO,

ikaja Juma nkamia akawa na nia ya kuwasilisha mswada wa kumuongezea mda wa kubaki,

Tuwe makini sana ,tusicheze na katiba ,waache wasio jielewa

SI UJINGA KUWA NA MAONI YA MAGUFULI KUONGEZEWA MUDA ILA NI HATARI KWA AFYA YA TAIFA LETU NA DEMOCRACY,

Mawazo ni mazuri ya MAGUFULI atawale zaid ya miaka kumi,

Lakin tujiulize maswali haya,

1. Mungu si athumani rais ni mtu anaweza kutoweka dunian japo tumuombee miaka mingi ya maisha, lakin akitoweka ghafla itakuwaje? Kama watanzania hamna imani Na wengine?

2. Rais MAGUFULI ni mzuri kwa utendaji, namkubali, vipi akiongeza miaka Na kutengua katiba, tunakuwa Na uhakika gani kwamba rais ajaye mbaya naye hatatengua katiba kuongoza miaka 50?

3. Wangekuwa wameshinda urais LOWASA AND COMPANY, ungejisikiaje mwana ccm ukisikia UKAWA wanampigia chapuo kubaki zaid ya muda uliosemwa kwenye katiba?

5. Una uhakika gani kama rais MAGUFULI mwenyewe atakubali kuongoza muda zaid?

Ushauri wangu ni kwamba tunao vijana wengi wenye uwezo wa kuongoza nchi,
Mfano, Mheshimiwa nchemba, Mheshimiwa Gambo, Hussein Mwinyi, Na wengine ambao sijawataja maana ccm ina hazina kubwa mno

Pili mzee MAGUFULI akikubali kupumzika atajenga heshima kubwa mno, maana ukifanya kazi kwa weledi kubaki kuachia haraka kabla hujaaribu ndipo utajenga heshima,

Pili tunaona MAGUFULI anafanya kazi kwa sababu taasisi zetu zimelegea mno, tunaomba mheshimiwa rais atengeneza MAGUFULI wengi wa ku run taasisi hizo,

Mungu ibariki Tanzania,

Mungu mbariki rais MAGUFULI,

Amen,

Video hiyo

Njaa mbaya...hata Mussolini kuna watu walikuwa wanaandamana Italy Ili atawale maisha yake yote...mungu c Abdala wala Zuena WW2 ndo vilivyokuja kumng'oa madarakani kutoka kwa majeshi ya kisovieti....kwetu huku sijui itakuaje mungu mwenyewe ajua
Leo Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa muda wa miaka miwili. HII NDIO MAKALA ILIYOPELEKEA MWANAHALISI KUFUNGIWA!

Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu?

Na Ansbert Ngurumo

TANGU Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.

“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.

“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

"Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!"

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumwombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua nani anastahili kuombea – ni Tundu Lissu.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
mkuu we kweli unajitambua ningekuwa na mamlaka ningekuban maana unatakiwa uwe fb wewe uwezo wako wa kufikir ni mdogo sana
 
Hivi mbona mnateteaga kila upuuzi?,hawa jamaa waliwahi toa FRONT PAGE Ben Saa8 anaonekana vijiwe vya kahawa na rafiki zake,wiki iliyopita walidanganya tena eti Lissu kasema Ninawajua walionipiga risasi tena Front page,kumbe uongo.. Hivi siku hizi mmekuwaje?,mbona hata mnatetea upuuzi?
Tupe kosa au tatizo la post ile ya mwana halisi au ndo ukweli mchungu
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Mmhhh?,wacha nipite nisije nikapigwa ban,
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Huwezi kushindana na serekali???????.........hata kama inakosea!!!, ...ni ubabe huu mloutumia na kuingia mikataba ya hovyo, ambayo sasa hivi mnahangaika na masahihisho.....
 
Nelson Mandela ni vita ya ukombozi wa ubaguzi wa rangi,muache kuwa mnafananisha Mandela na vitu vya kijinga.Mandela hakuwahi kuwa ndumilakuwili kama hawa jamaa zenu wasiojua wanapigania nini?,kama unajua historia ya South Africa utanielewa,ila mtu yeyote anayeielewa South Africa au umewahi kuishi huko huwezi leta mifano ya Mandela hapa.Hawa ni wachumia tumbo tu.Na hili linadhihirishwa na kumkumbatia Lowassa,ni somo tosha tu kuwa sio watu wa kucheka nao hata dakika moja.
Mkuu unachosema kina weza kuwa na chembe ya ukweli, lkn hawa wanasaidia kutufumbua macho au kuamsha hari ya uwajibikaji kwa waliopewa dhamana, ikizingatiwa wengi wao pia ni wachumia tumbo tu km hawa.
 
Polisi na raia wengine waliouawa na majambazi KIBITI hakuna hata aliyethubutu kutangaza kuwaombea ndugu zetu wa KIBITI waliopoteza maisha yao.
Leo anatokea mtu mmoja amejeruhiwa watu wanatangaza maombi. Je, ni Mungu wa wapi huyo tunayemwomba?
 
Huwezi kushindana na serekali???????.........hata kama inakosea!!!, ...ni ubabe huu mloutumia na kuingia mikataba ya hovyo, ambayo sasa hivi mnahangaika na masahihisho.....
Kwahiyo kama walishakosea huko nyuma kwenye serikali zilizopita,na sasa tunahangaika na masahihisho ni sahihi mtu aanze kutukatisha tamaa?,.,katika kipindi ambacho kinahitaji ubabe ni hiki,nyie mnadhani JPM ana deal na upinzani tu Prof Muhongo ni mpinzani?,Simbachawene na wengine waliokumbwa ni wapinzani?,kitu ambacho hammuelewi JPM ni kuwa haangalii sura linapokuja swala la uwajibikaji,hata ukiwa shemeji yake unakwenda na maji.Kuna wakati utafika mtamuelewa tu.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Usisahau udhalimu hulipwa na udhalimu, wote walioongoza kwa mkono wa chuma kufanikiwa ni zero
+++. Bali haki huinua taifa, ukweli una tabia mbaya sana hata uufunike na beseni utachomoza tu ni muda unategemewa.
 
Hapo ndo mnapoanzia kujidanganya,mnadhani wananchi wengi wapo nyuma ya CHADEMA na Kubenea,juzi jumapili kuna watu waliprint t-shirt kibao za PRAY 4LISSU,wakidhani wangeuza hata 100,waliishia kuuza tshirt 3 au 4 tu.Wafuasi na uma mnaousemea umebaki JF tu.Mtaani watu wapo bize na kupambana na hali zao,kujipatia kipato.
kweli mkuu ndiyo maana baada ya kukosa wateja polisi walizifuata dukani na kuzichukua,lkn naona hawakumlipa mchapishaji wa hizo t-shirt una akili sana,tupo tunaendelea kujenga viwanda.
 
Niliwahi kusema, narudia tena "This regime could be the worst regime in the history of this country"
That's according to your point of view but to others it might be the best regime ever,just remember there's nothing best or worse to everyone,that applies to all regimes ever existed in our country.The only thing i see here most of the time,is when some of us conclude that their opinions are the only which appears to be the BEST.That's WRONG totally and completely.
 
Leo Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa muda wa miaka miwili. HII NDIO MAKALA ILIYOPELEKEA MWANAHALISI KUFUNGIWA!

Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu?

Na Ansbert Ngurumo

TANGU Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.

“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.

“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

"Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!"

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumwombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua nani anastahili kuombea – ni Tundu Lissu.
Heri kijana mdogo mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu asiyetaka kusikia maonyo
 
Hivi mbona mnateteaga kila upuuzi?,hawa jamaa waliwahi toa FRONT PAGE Ben Saa8 anaonekana vijiwe vya kahawa na rafiki zake,wiki iliyopita walidanganya tena eti Lissu kasema Ninawajua walionipiga risasi tena Front page,kumbe uongo.. Hivi siku hizi mmekuwaje?,mbona hata mnatetea upuuzi?
Sasa Lissu si ndie aliepigwa risasi na kasema anawafahamu.?
 
Usisahau udhalimu hulipwa na udhalimu, wote walioongoza kwa mkono wa chuma kufanikiwa ni zero
+++. Bali haki huinua taifa, ukweli una tabia mbaya sana hata uufunike na beseni utachomoza tu ni muda unategemewa.
Mkuu hizo ni story tu jamaa yenu wa Kenya tangu aanze kutafuta uraisi miaka ya 2000 na kitu ameshanyonga wakenya kibao,na juzi kanyonga mkuu wa IT tume ya uchaguzi,na nyie ndo mnamuona mwanademokrasia bora East Africa.Hizi akili zenu tunazijua tu.Sijui udhali sijui mkono wa chuma,hakuna kitu.Kama unaweza anzisha movement muingie msituni wawamalize kama wale jamaa wa KIBITI walivyofyekwa.Vinginevyo fanya mambo yako,endelea na juhudi zako za utafutaji.Narudia huwezi shindana na serikali yoyote hata ya Burundi,serikali ina mkono mrefu sanaaa.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Nina hakika kama ulisoma shule ulisoma ile ya kukalia mawe na uliishia darasa la nne.
 
Back
Top Bottom