Kisa cha MwanaHALISI kufungiwa ni Habari ya "Nani anastahili kuombewa kati ya Lissu au Magufuli"

Leo Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa muda wa miaka miwili. HII NDIO MAKALA ILIYOPELEKEA MWANAHALISI KUFUNGIWA!

Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu?

Na Ansbert Ngurumo

TANGU Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.

“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.

“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

"Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!"

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumwombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua nani anastahili kuombea – ni Tundu Lissu.

Mungu si mwanadamu na atatenda atakalo muda si mrefu.
 
Polisi na raia wengine waliouawa na majambazi KIBITI hakuna hata aliyethubutu kutangaza kuwaombea ndugu zetu wa KIBITI waliopoteza maisha yao.
Leo anatokea mtu mmoja amejeruhiwa watu wanatangaza maombi. Je, ni Mungu wa wapi huyo tunayemwomba?

Mkuu kila mtu ana vionjo vyake, huwezi kulazimisha kila mtu awaombee watu wa kibiti. Sio lazima wanaotaka kumuombea Lissu watake pia kuwaombea watu wa Kibiti. Kosa lingekuwa hao wanaotaka kumuombea Lissu kama walikataa watu wa kibiti kuombewa. Acha kubeba maneno ya propaganda za kizee hapa jukwaani na wewe kujifanya unajengea hoja zako toka hapo. Msilazimishe watu kuonyesha mapenzi yao kwa watu wasiofungamana nao. Hata wewe ukitaka kuwajibu vizuri hao wafuasi wa cdm wanaotaka kumuobea Lissu, kusanya wenzako kawaombee watu wa kibiti hakuna atakaye kukataza.
 
Ili gazeti kwa matusi haya lingefutwa kabisa..yani unamtukana Rais hivi uachwe? Shenzi.kabisa
 
Watanzania wanajuta sasa. Badala ya kuendeleza amani yetu ametuletea machafuko. 2020 ni bora tumrejeshe kwao akalime viazi vitamu. Hatufai kabisa.
 
Nakubaliana kabisa na wewe, je kumpiga risasi ndio ilikuwa adhabu stahiki? Lissu ni jeuri na hilo halina ubishi, ila kumbuka kila mtu ana madhaifu yake. Mimi sio mara moja au mbili nimesema Lissu anaongea lugha za kejeli lakini hana tofauti na Magufuli tofauti yao mmoja ni rais na mwingine ni mbunge. Hizo lugha alizoongea Lissu ni lugha za kawaida kabisa za wanasiasa, ni nani hakusikia na kuona kesi alizofunguliwa Lissu kuhusu utetezi wake kwenye madini? Kama Lissu aliumizwa na kudhalilishwa kwenye utetezi wake wa madini na Magufuli akiwa ndani ya watesi hao, utamkatazaje Lissu kupiga madongo apendavyo watu waliokuwa wanafanya siasa ya dhahiri na kumtesa yeye alipokuwa kwenye mapambano? Je Watanzania wamewahi kuwapiga risasi hao waliongia hiyo mikataba ya wizi? Kuna yoyote aliyefungwa kwa kuingia mikataba hiyo?

Tukubali tukatae kwa hili la kupigwa Lissu risasi ni kuvuka mipaka, na ni moja ya siasa za hovyo hata mtu ukijivika uzalendo wa aina gani. Kwani kulikuwa na ulazima gani wa kumpiga risasi wakati watu wangeweza kutenda kazi zao na kumpuuza tu? Kuna tabia huwezi kuzibadili hata ufanyeje bali kuzipuuza tu. Mfano mrahisi JK alikuwa anasafari sana mbali ya kelele za hali ya juu, je aliacha kusafiri? Kuna mtu alimpiga risasi wakati alikuwa analitia taifa hasara kwa safari zake? Mfano mwingine leo hii Magufuli anaongea lugha za kejeli na jazba za wazi, unadhani haoni kwamba watu wanakerwa na tabia hiyo? Je umeona mtu wakimpiga risasi zaidi ya watu kumpuuza? Haya tuseme Lissu sio mzalendo kwa kukashifu hiyo approach ya Magufuli kwenye madini, je tuna uhakika gani approach yake ya sasa ndio itatufaidisha kwenye sekta ya madini? Kumbuka tunachimba tukawauzie wazungu, je wakiamua kutokuyanunua tutakuwa tumefaidika na nini? Au unadhani Tanzania tu ndio yenye madini na hakuna nchi nyingine zenye madini dunia hii? Haingii akilini ukae serekalini zaidi ya miaka 20 useme eti ungepiga kelele ungekosa madaraka kisha ukae kimya wakati tunaingia hasara mpaka uwe rais. Je watanzania wote sasa hivi tukisubiri tuwe marais ndio tuonyeshe uzalendo tutatoboa?
Mkuu una maswali mazuri na fikirishi.. Sipendi nionekane najitetea au natetea serikali kuhusu hili.Nakupa mfano mmoja.,ukiwa unagombana na mkeo kila mara kwa sauti,huku ukiwa unampiga mikwara kibao.Huku majirani wakitega sikio na kusikiliza ugomvi wenu,siku ikitokea akapatwa na madhara moja kwa moja,majirani watajua kuna namna unahusika kutokana na ugomvi wenu wa mara kwa mara,wakati huo huo kutokana na ugomvi wenu kama kuna jirani yako yeyote alikuwa na visa binafsi na mkeo anaweza kumdhuru mkeo akijua wote watakuhisi wewe.Tukirudi kwenye ishu ya Lissu,kwa mtiririko wake wa kisiasa alikuwa anajenga hali tofauti,kumbuka tupo kwenye vita kali sana.Huwezi kunishawishi kwamba adui wa Lissu ni serikali ya TZ,hakuna mtu mwingine anaweza kuwa adui yake.So,yawezekana serikali ikahusika au akawa mtu mwingine,ila mimi hapa JF naongelea kwa ujumla Lissu angekosoa bila kejeli,na madharau na kuwa mwiba kwa serikali,asingetoa mwanya kwa serikali au mtu yeyote kumshoot kwa kisingizio chochote,inaweza isiwe serikali na bado aliyempiga risasi asipatine wala kujulikana milele,hata ungewaita CIA au scotland yard,aliyemuua JF Kennedy aliwahi patikana?,aliyemuua 2Pac aliwahi kujulilkana?,tukubali ukweli kuwa Lissu alisahau yeye sio Raisi wa Jamhuri,ingawa upo sahihi kauli nyingine za Raisi sio nzuri.
 
Na unapoanza kumwambia huyo huyo baba yako,ukiwatangazia ndugu zako kuwa Tuna baba wa Hovyo hovyo,na uongozi wa hovyo wa familia.Unategemea nini?,ndo nidhamu.Na unapoomba mbele za media familia yenu itengwe na marafiki zenu,msipewe msaada wowote ndo kumkosoa baba yako?,, mtakataa siku zote,ila yule chizi wenu alizidiwa na kitu kinaitwa MUCH KNOW,ndo maana pamoja na kufatiliwa na gari muda mrefu,akijifanya MUCH KNOW hakuona umuhimu wa kwenda polisi kuripoti kwa dharau,matokeo yake anapumulia mipira.Na anaweza kuwa kitandani hata mwaka mzima.
You are really, giant fool.
 
Kwahiyo kama walishakosea huko nyuma kwenye serikali zilizopita,na sasa tunahangaika na masahihisho ni sahihi mtu aanze kutukatisha tamaa?,.,katika kipindi ambacho kinahitaji ubabe ni hiki,nyie mnadhani JPM ana deal na upinzani tu Prof Muhongo ni mpinzani?,Simbachawene na wengine waliokumbwa ni wapinzani?,kitu ambacho hammuelewi JPM ni kuwa haangalii sura linapokuja swala la uwajibikaji,hata ukiwa shemeji yake unakwenda na maji.Kuna wakati utafika mtamuelewa tu.
Bora yawe masahihisho sahihi sasa. Hao wakosoaji wenu wewe umeamua kuwaita"wakatisha tamaa" wakati wenzako wakiwaita wasaliti. Nikiwarejea hao wanao wakatisha tamaa kwa kukosoa approach inayo tumika sasa hivi huko nyuma waliwahi pia kukosoa mkawapa majina mabaya kama mnavo fanya sasa hivi!!!.....laiti wangesikilizwa hakika muda huu tungekuwa tunafanya mambo mengine. Ni takriban miaka 20 imepita ndo mmegutuka na kubaini makosa!!!!....wenye utambuzi wanapo waonya mkubali maonyo yao na si kuwapa majina mabaya! zingatieni mnacho ambiwa kwani uwezo wa ku load tunazidiana, wengine hutumia sekunde, dakika, siku,.........wengine miaka 20 kama nyinyi. Ndugu swala si kufanya masahihisho bali ni kuweka majawabu sahihi, ili baadaye usirudie kufanya masahihisho ya masahihisho!
 
That's according to your point of view but to others it might be the best regime ever,just remember there's nothing best or worse to everyone,that applies to all regimes ever existed in our country.The only thing i see here most of the time,is when some of us conclude that their opinions are the only which appears to be the BEST.That's WRONG totally and completely.
You haven't said anything new!!! So obvious that even an imbecile knows that!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Mbona unashindwa kuzipangua hizo hoja???
Msaliti ni mikataba mibovu, na walioiingiza nchi kwa maslahi yao AU ni Lisu anaeikosoa, na kuwaelimisha wananchi.???? HUONI KWAMBA HAPO KUNA FILAMU YA KICHINA???
 
You are very right. Ile makala nimeisoma jana imenitoa machozi nilipomkumbuka mzalendo wa kweli na mtz muhimu zaidi nchini anayepaswa kuombewa.......hawa walaaniwa ccm na baradhuri wao mkuu wanaharibu nchi wkt hawana faida yoyote..
 
Hapo ndo mnapoanzia kujidanganya,mnadhani wananchi wengi wapo nyuma ya CHADEMA na Kubenea,juzi jumapili kuna watu waliprint t-shirt kibao za PRAY 4LISSU,wakidhani wangeuza hata 100,waliishia kuuza tshirt 3 au 4 tu.Wafuasi na uma mnaousemea umebaki JF tu.Mtaani watu wapo bize na kupambana na hali zao,kujipatia kipato.
we mbwa acha uongo....watz wanatafuta hizo t-shirt bila mafaniko
 
Mkuu una maswali mazuri na fikirishi.. Sipendi nionekane najitetea au natetea serikali kuhusu hili.Nakupa mfano mmoja.,ukiwa unagombana na mkeo kila mara kwa sauti,huku ukiwa unampiga mikwara kibao.Huku majirani wakitega sikio na kusikiliza ugomvi wenu,siku ikitokea akapatwa na madhara moja kwa moja,majirani watajua kuna namna unahusika kutokana na ugomvi wenu wa mara kwa mara,wakati huo huo kutokana na ugomvi wenu kama mke wako alikuwa na visa binafsi na mkeo anaweza kumdhuru mkeo akijua wote watakuhisi wewe.Tukirudi kwenye ishu ya Lissu,kwa mtiririko wake wa kisiasa alikuwa anajenga hali tofauti,kumbuka tupo kwenye vita kali sana.Huwezi kunishawishi kwamba adui wa Lissu ni serikali ya TZ,hakuna mtu mwingine anaweza kuwa adui yake.So,yawezekana serikali ikahusika au akawa mtu mwingine,ila mimi hapa JF naongelea kwa ujumla Lissu angekosoa bila kejeli,na madharau na kuwa mwiba kwa serikali,asingetoa mwanya kwa serikali au mtu yeyote kumshoot kwa kisingizio chochote,inaweza isiwe serikali na bado aliyempiga risasi asipatine wala kujulikana milele,hata ungewaita CIA au scotland yard,aliyemuua JF Kennedy aliwahi patikana?,aliyemuua 2Pac aliwahi kujulilkana?,tukubali ukweli kuwa Lissu alisahau yeye sio Raisi wa Jamhuri,ingawa upo sahihi kauli nyingine za Raisi sio nzuri.

Sasa naona umejadili kwa hoja, huo udhaifu wa Lissu kila mtu anaujua hilo halina ubishi, lakini nimekuambia kila mtu ana madhaifu yake. Kuna watu wana viherere, waongo, wanafiki, washirikina nk. Lakini tunaishi nao hivyo hivyo na kero hizo na sio sahihi kuondoa uhai wao kisa wana tabia zinazokera. Sisemi serekali inahusika lakini kwa mazingira ndio kinara namba moja hata ukiangilia mfano wa mtu mwenye ugomvi na mkewe. Nikupe mfano mmoja unaaocha shaka, kwenye eneo aliloshambuliwa Lissu kulikuwa na askari polisi wa kulinda eneo lile. Kwa askari wenye weledi halafu usikie mlio wa smg tena risasi zaidi ya 30, halafu litoke gari eneo hilo hilo bila kulizuia, inahitaji uwezo wa kufikiri uwe umefika mwisho ndio usione huo utata. Hata mimi sina utaalamu wa silaha, lakini mlio wa bunduki ukilia tena risasi zisizopungua 30 nitajua hilo eneo sio salama, sembuse askari anayejua silaha?

Mkuu hebu tujadili mengine sio hili, ndo maana nakuambia hata uwe mzalendo vipi, kipimo chake hakiwezi kuwa kilichomkuta Lissu. Kumbuka Lissu ana rekodi nzuri ya kutetea raslimali zetu kuliko mzalendo academia. Kama wengine ndio wanahisi vita ya raslimali zetu zimeanza leo, tunabaki tunawashangaa kumbe wenzetu ndio wanaamka sasa wakati vita vilianza muda mrefu tu. Kwa hiyo kwetu sisi tunaona ni kick za kisiasa tu, tulitarajia tuombwe msamha wa wizi uliotokea na kukubali hadharani jitihada za wale waliopigania raslimali hizo toka zamani. Kisha kama taifa tusonge pamoja. Lakini kiongozi wetu leo kujiona ndio mzalendo sana, kwa sisi wakristo tuna mfananisha na mtu aliyealikwa harusini kisha akalazimisha kukaa katika kiti cha mbele.
 
Sawa uwezo wangu mdogo ila usini ban,ila pingana na mimi kwa kushindana na serikali,anza na kuandamana tu,anzisha movement yoyote ya kelele zozote mtaani kwenu,waje FFU wakutengue kiuno ukaugulie halafu urudi hapa uelezee u GENIOUS wako hapa.Shwein.
Nampigia mbuzi gitaa
 
Ila miaka hii kazi ipo kweli kweli,ngoja tuone,yangu macho bora tufike salama
 
haka kakipande ka hii habari ngoja ni kakariri katanifaa sana 2020...katanisaidia kuombea kura zote, lakini pia nikiwa kwenye foleni ya kura kataniliwaza...
 
Kwani Rais wako watatu?
Ni kweli ni watatu"
Rais wa kwanza ni mikataba ya wizi, iliosainiwa na serikali zilizopita,, akiwepo huyu rais wasasa. Itawakandamiza hadi muda waliokubaliana kuiba uishe.

Rais wa pili ni Magu, anatuchezea filamu yakutokuitambua, mikataba ambayo mwanzo aliijua na kuikubali.

Rais wa tatu, ni rais Tundu Lisu. Huyu ni wa kujitolea, na wa Muda wote.
Alianza kuikosoa na kuipinga hio mikataba tangu miaka 16 iliopita, kwa marais wengine.
Huyu ndie anaewapigania wa nyonge, kwa kuisema kweli yoote...
Mfno:: Swala la kukamatwa ndege,serikali iliwadanganya wananchi. Lisu akasema ukweli. ..baadae serikali ikakiri na kuongea ukweli.

KINACHOMUUA LISU NI UKWELI.
 
Mkuu sipingi utetezi wako kwa serekali kwa hiki kilichomkuta Lissu na umedhibitisha Lissu alitarajia kuishinda serekali sasa kwa kupigwa risasi serekali ndio imeshinda. Umeeleweka kwa ufafanuzi wako. Sishangai kwani ww unalipwa na serekali, una maisha mazuri, watoto wako hawasomi shule za kata kama wetu, unapata huduma zote kwa gharama ya serekali kama umeme, maji nk hata kama mshahara na marupurupu unayolipwa hayalingani na tija yako kwa taifa hili ila unaringia kulipwa kisheria. Sasa ukishindwa hata kutetea unyama dhidi ya raia utakuwa na faida gani?

Kwako ww serekali ni malaika hairuhusiwi kuikosoa kwani tafsiri ya kukosoa kwako ni kushindana nayo. Na unapata kiburi cha kuandika uliyoandika kwani unajua serekali inayopeleka watoto wako chooni ikiondoka hadhi yako itashuka.

Mungu akubariki sana Mkuu.Ni Watu wachache wenye Ubinadamu ktk Dunia hii ,inasikitisha sana kuona Raia asie na silaha/mtetezi wa Raia anashambuliwa kwa Silaha za moto (kali) kama Mnyama mkali alieingilia makazi ya Watu ..Inahuzunisha zaidi kuona na kusikia baadhi ya Watu wasio na Ubinadamu wakilifurahia hili na kushangilia.

Umasikini na Ujinga umetufanya kiasi tumepoteza ule uwezo wa kufikiri mpaka tunawaaabudu na kuwatukuza Binadamu wengine na kuwageuza Miungu (Watu) wasiokosea....
 

Similar Discussions

56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom