Kisa cha MwanaHALISI kufungiwa ni Habari ya "Nani anastahili kuombewa kati ya Lissu au Magufuli"

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Leo Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa muda wa miaka miwili. HII NDIO MAKALA ILIYOPELEKEA MWANAHALISI KUFUNGIWA!

Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu?

Na Ansbert Ngurumo

TANGU Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.

“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.

“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

"Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!"

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumwombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua nani anastahili kuombea – ni Tundu Lissu.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
 
Akili ya kulewa madaraka na kujiona nyinyi ni miungu watu!!
 
Kikalyamanzira zaidi mkuu
 
Unaweza kushindana na serikali lakini sio nchi, nchi ikisimama pamoja hakuna wakuishinda.
 
Unapomwambia baba yako hapa tusifanye hivi,tufanye vile ni kushindana naye? Kuna serikali yoyote ile duniani isiyoambiwa/isiyokosolewa inapokosea? Hii nchi ni yetu,Watanzania. Serikali ni yetu na ni sisi.
 
Akili ya kulewa madaraka na kujiona nyinyi ni miungu watu!!
Hivi mbona mnateteaga kila upuuzi?,hawa jamaa waliwahi toa FRONT PAGE Ben Saa8 anaonekana vijiwe vya kahawa na rafiki zake,wiki iliyopita walidanganya tena eti Lissu kasema Ninawajua walionipiga risasi tena Front page,kumbe uongo.. Hivi siku hizi mmekuwaje?,mbona hata mnatetea upuuzi?
 
Unaweza kushindana na serikali lakini sio nchi, nchi ikisimama pamoja hakuna wakuishinda.
Hapo ndo mnapoanzia kujidanganya,mnadhani wananchi wengi wapo nyuma ya CHADEMA na Kubenea,juzi jumapili kuna watu waliprint t-shirt kibao za PRAY 4LISSU,wakidhani wangeuza hata 100,waliishia kuuza tshirt 3 au 4 tu.Wafuasi na uma mnaousemea umebaki JF tu.Mtaani watu wapo bize na kupambana na hali zao,kujipatia kipato.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Hivi Nelson Mandela alikua anapambana na yanga fc?
 
Similar Discussions

56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom