Kisa cha mtu aliyebeba punda na Watanzania

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,384
17,953
Mwanadamu mmoja alikua akisafiri na mkewe wakitumia usafiri wa punda yaani wakiwa wamempanda punda yule lakini wakiwa njiani katikat ya safari yao wakakutana ma wanadamu wakawapazia sauti wakisema; ''ninyi watu hamuoni ya kuwa mnamuumiza punda huyo iweje ninyi wote wawili mumpande punda mmoja?

Jamaa kuskia hivyo akaona isiwe shida akaona amwambie mkewe ashuke apande yeye peke yake na mkewe akakubali safari ikaendelea lakini walipofika mbele wakakutana na wanadamu wengine wakamdhihaki tena bwana yule wakisema; ''Wewe mbona ni mwanaume usiye na huruma yaani wewe umepanda punda huyo na kumwacha mwanamke wako atembee em kuwa na huruma hata''

Jamaa akaona isiwe shida acha nishuke apande mke wangu na safari ikaendelea. Wakiwa njiani tena wakakutana na wanadamu wengine tena na walipomtazama tu bwana yule na mkewe wakaangua vicheko vya dharau wakisema; ''Tazama mwanaume yule asivyokua na akili yaani yeye anatembea kwa miguu na kumuacha mkewe apande punda?''

Jamaa kusikia vile akaona mke wangu isiwe shida acha tushuke sie na kumuacha punda atembee mwenyewe sie tutembee kwa miguu basi wakafanya hivyo na safari ikaendelea lkini walipofika mbele wakakutana na wanadamu wengine nao walipowaona tu wakawadhihaki wakisema; ''Tazama wajinga wale watembea kwa miguu ilihali wana punda na wanaweza kumpanda''

Basi baada ya mambo yale jamaa akawaza akaamua kumbeba punda. Nimekumbuka kisa hiki nikawatazama watanzania wanavyokosoa namna Rais SSH anavyoendesha nchi.

Chonde chonde Rais Samia usibebe punda, unafanya vizuri sana, endelea hivyo hivyo. Kimsingi wewe umewapa uhuru wa kusema, waache waseme lakini fanya yale uliyopanga kuwafanyia watanzania. Huwezi kuwaridhisha wote kwa namna wanavyotaka.
 
Ukisimama-simama njia kusikiliza makelele ya wapinzani maadui na watetezi wa mabepari, kamwe hutafika kule uendako --- Watanzania, mimi kamwe sikubali kugeuka nyuma! ~ Nyerere. JPM was right!!! Bi Mkubwa kachemsha ^key-know-mar^
 
Daah!!!! Kisa Kizuri Sana, lakini kumbuka Rais ni Kama tembo ambaye sikuzote Hashidwi kubaba Mkonga wake. Madam President Tunaamini Utaweza Kutubaba Watanzania wote regardless of our political affiliation, religious and gender. Mama Tunakuamini Unaweza.. shikilia Hapo Hapo ni sehemu Sahihi.
 
Kikubwa sisi tuna amani maendeleo kila mtu atafuta kwa muda wake na familia yake, maza apige 15 amani iendele kuliko maendeleo ya masimango hata choo cha shule kikiwa kinazinduliwa mtasimangwa kama vile ametoa pesa yake mfukoni, maza kiuongozi ni dhaifu lakini hana shida na mtu tupo naye pamoja.
 
Mbowe yuko bize anakula vya haramu
20210527_213348.jpg
 
^Ukisimama-simama njia kusikiliza makelele ya wapinzani maadui na watetezi wa mabepari, kamwe hutafika kule uendako --- Watanzania, mimi kamwe sikubali kugeuka nyuma!^ ~ Nyerere. JPM was right!!! Bi Mkubwa kachemsha ^key-know-mar^
Kachemsha kwa sababu hajaua mtu hata mmoja mpaka sasa wala hamiliki kikundi cha watu WASIOJULIKANA.

Kachemsha kwa sababu ameruhusu Uhuru wa maoni kama unavyoutumia sasa.

Mungu anatupenda Watanzania, Kama Mwendazake angekuwapo tulikuwa tunaelekea kuwa Zimbabwe nyingine.

Kazi iendelee, waache Sukuma Gang waendelee kusema kwa vile umewapa uhuru
 
Mwanadamu mmoja alikua akisafiri na mkewe wakitumia usafiri wa punda yaani wakiwa wamempanda punda yule lakini wakiwa njiani katikat ya safari yao wakakutana ma wanadamu wakawapazia sauti wakisema; ''ninyi watu hamuoni ya kuwa mnamuumiza punda huyo iweje ninyi wote wawili mumpande punda mmoja?

Jamaa kuskia hivyo akaona isiwe shida akaona amwambie mkewe ashuke apande yeye peke yake na mkewe akakubali safari ikaendelea lakini walipofika mbele wakakutana na wanadamu wengine wakamdhihaki tena bwana yule wakisema; ''Wewe mbona ni mwanaume usiye na huruma yaani wewe umepanda punda huyo na kumwacha mwanamke wako atembee em kuwa na huruma hata''

Jamaa akaona isiwe shida acha nishuke apande mke wangu na safari ikaendelea. Wakiwa njiani tena wakakutana na wanadamu wengine tena na walipomtazama tu bwana yule na mkewe wakaangua vicheko vya dharau wakisema; ''Tazama mwanaume yule asivyokua na akili yaani yeye anatembea kwa miguu na kumuacha mkewe apande punda?''

Jamaa kusikia vile akaona mke wangu isiwe shida acha tushuke sie na kumuacha punda atembee mwenyewe sie tutembee kwa miguu basi wakafanya hivyo na safari ikaendelea lkini walipofika mbele wakakutana na wanadamu wengine nao walipowaona tu wakawadhihaki wakisema; ''Tazama wajinga wale watembea kwa miguu ilihali wana punda na wanaweza kumpanda''

Basi baada ya mambo yale jamaa akawaza akaamua kumbeba punda. Nimekumbuka kisa hiki nikawatazama watanzania wanavyokosoa namna Rais SSH anavyoendesha nchi.

Chonde chonde Rais Samia usibebe punda, unafanya vizuri sana, endelea hivyo hivyo. Kimsingi wewe umewapa uhuru wa kusema, waache waseme lakini fanya yale uliyopanga kuwafanyia watanzania. Huwezi kuwaridhisha wote kwa namna wanavyotaka
You are right
 
Back
Top Bottom