JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,106
- 3,523
Salamu wanajamvi!
Mwaka 2008, Mwezi Julai, Tanzania ilishuhudia tukio la aina yake la kiimani. Wahubiri wa Injili 17 wa madhehebu ya waadventist Wasabato masalia walipiga kambi uwanja wa ndege wa Dar es salaam wakisema wanataka kwenda kuhubiri Injili Ulaya na Marekani huku wakiwa hawana visa wala ticketi za kwenda huko.
WAO WALIDAI TIKETI ZAO NI BIBLIA NA KWAMBA MUNGU ATATENDA MIUJIZA. Askari wakawatimua. Siku tatu baadae wakarudi tena! Safari hii wakiwa 51! Kwa madai yaleyale.Serikali ikawatimua tena bila huruma. Imani pasipo maarifa.
Kisa hiki kinatufundisha nini? Tuweni na Imani lakini tusiache maarifa kando.Tutaangamia na Mungu hawezi kutusaidia.
Katika hali kama hii ya Covid-19 yatupasa tuwe timamu kimwili kiakili na kiroho. Kamwe tusiache maarifa kando. Maarifa yanatoka kwa Mungu. Mungu ndiye aliyetuhimiza kuyatafuta ili yatusaidie sisi binadamu kuishi kwa amani.
Covid-19 ni hatari. Kuamini kuwa ugonjwa huu utatokomea kwa kunawa maji tiririka na kuvaa barakoa ni Imani iliyopitiliza kama ya Wasabato masalia wa 2008.
Njia ya uhakika kuliko zote ingawa inadhoofisha uchumi ni lockdown walau kwa siku 30. Tena kama ikichukuliwa wakati sahihi. Tukichelewa kama ilivyo kuwa Italy na Spain au hata Marekani tutajuta. Hatuja chelewa bado.
Hakuna kibaya kama ubinafsi. Na ndio unao tugawanya. Kuna watu wanawaza sadaka hawataki kusikia habari ya lockdown. Kuna watu wanawaza biashara zao wanasahau ubinadamu! Ubinafsi.