William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Wanazuoni:

Kichwa cha habari hapo juu sio kwamba ni cha uchochezi au kwamba kimelenga kupasukia watu kwa kashifa au kwamba ni kufuru kwa Mungu.La hasha, bali ni tafsiri ya kile alichomaanisha Mwanajeshi mmoja huko Marekani pale alipoibuka na Formula ya kukokotoa tarehe ya kurudi kwake Yesu duniani. Jamaa huyo anaitwa WILLIAM MILLER.

William Miller
alizaliwa tarehe 15 Februari1782, huko Jimboni Massachusetts, Marekani na kisha kulelewa katika familia ya Kikristu iliyokuwa na makazi yake Jimbo la New York ya Kaskazini.Familia ya William Miller ilikuwa ya Kibaptisti. Babu yake na wajomba zake wawili walikuwa ni wachungaji katika kanisa la Wabaptisti. Kanisa la Kibaptisti, ni mumeguko karne ya 17 BK kutoka Kanisa la England,yaani Kanisa la Serikali ya Uingereza (Anglikani) ambalo leo linaitwa Kanisa la Kianglikana.

Miller, katika ujana wake alipata kujiunga na jeshi laMarekani na kufikiaCheo cha Kapteini, wakati wa vita kati ya Marekani na Uingereza (Great Britain) mnamo mwaka 1812.Na inasemekana alikuwa na akili sana na kwamba alikuwa na kipaji cha kufafanua mambo.Bwana Miller baada ya kumaliza utumishi wake Jeshini na kurudi toka vitani (kati ya Marekani na Uingereza mwaka 1812), alianzisha makazi katika Shamba lake huko Low Hampton, New York, ambamo alikuwa amejenga nyumba na akawa akiishi hapo na wakati fulani akawa akienda kusali kwenye kanisa la Baptist la karibu yake.

Bwana Miller kwa kujishughulisha na mambo ya kiimani alipata kuwa mwana-DEIST,yaani alipata kuamini katika Falsafa ya Deism.

Deism ni Falsafa inayokazia kwamba Mungu hajihusishi moja kwa moja na mambo ya ulimwengu huu; kwamba yeye ndiye muumba wa vyote na kwamba ni mkamilifu lakini mungu huyo, hajiingizi katika mambo ya ulimwengu unaonekana kwa njia ya miujiza na kuwa ufunuo sio chimbuko pekee la maarifa juu ya imani na kwamba kufikiri tu kwa mwanadamu na kufanya utafiti juu ya maumbile kunatosha kufahamu na kubainisha kwamba kuna Mungu mmoja.

Kwa hiyo, tafsiri ya imani hii ya Deism ni kwamba Mungu baada ya kuumba ulimwengu alijiondokea zake na kuacha vitu vyote tuvirithi na tokea wakati huo hana mpango navyo tena na wala hajali yanayoendelea huku duniani.

SASA katika mkururu huo wa kutaka kuchimbua mambo magumu ndio William Miller alijikuta akivamia suala ambalo ndio kiini cha mjadala huu wa leo.Ni suala la tarehe ya kurudi kwa YESU KRISTU.

Ni hivi, kwa muda miaka miwili William Miller alipata kujichimbia ndani kwake “akibundi” au akibukua Biblia na ndipo katika kukisoma Kitabu cha Nabii Daniel, sura 8:13-19 ambacho kiliandikwa kabla hata Yesu hajazaliwa akagundua fomula ya kukotoa tarehe ya kurudi kwa Yesu duniani ambako inasomeka hivi:

“13.Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa. 15 Ikawa mimi, naam, mimi Danieli, nilipoyaona maono hayo, nalitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu.16 Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya.17 Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.18 Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.19 Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa.”

Kanuni ya Miller inadai kwamba kinabii siku moja kwa Mungu ni sawa na mwaka mmoja wa Kalenda ya wakati huo na hata sasa. Kwa msingi hiyo, siku alizoziongelea Daniel kwa jicho la Miller ni sawa na miaka 2,300 kwa kutumia Kalenda ya wakati huo ambayo ilikuwa ni ya Gregori na ambayo inatumika hadi sasa. Kalenda ya Gregori ilianza kutumika nchini Marekani mwaka 1752. (Kalenda ya Gregori ilizinduliwa rasmimwaka 1582 na kuanza kutumiwa na nchi kama Ufaransa, Italia, Polandi, Ureno na Uhispania).

Katika Sadikifu(thesis) hiyo ya Miller, alikaza kudai kwamba wapo wasomi wengine kama yeye ambao tafiti zao zimeonyesha kuwa tarehe ya kurudi kwa Yesu INAKOKOTOLEKA KIRAHISI SANA. Miongoni mwa wanazuoni waliotajwa alikuwa ni Mwanasayansi Sir Issac Newton.Huyu kwa mjibu wa Miller anadai naye alipata kufanya hesabu kama zake (alipokuwa akitafiti juu ya Kanuni za asili zinazotawala mvutano kati ya Dunia na Jua, Laws of Gravity) na kupata majibu sawa na ya Miller juu ya unabii huo wa Biblia wa kurudi kwa Yesu, na kwamba Newton aliacha maandishi mengi sana juu ya jambo hilo!

Kwa maelezo ya Miller na kwa kadri ya “ufunuo wake” na kwa kanuni yake (ya Kitabu cha Daniel) na kwa kusoma historia, aliweza kwa hakika kwa madai yake kuona kuwa mwaka wa kuanza kuhesabika hizo siku 2,300 ambazo ni sawa na miaka 2,300 ilikuwa mwaka 457K.K. Kwa hiyo, kwa kutumia alichofanya ni kuchukua huo mwaka 457BK ns kutoa miaka 2,300 na hivi kupata jibu la 1843 kwamba ndiyo ingalikuwa ni muda wa kutakaswa “patakatifu pa patakatifu.” Hata hivyo baadaye tarehe ilisogezwa mbele hadi tarehe 22 Oktoba 1844.

Mathematically,Kanuni ya Miller ilikuwa ni hii:

2,300-457=1843 (siku ya kuingia Yesu duniani).

Vigezo alivyotumia Miller katika kuthibitisha Sadikifu yake

Kuna mambo mawili Miller aliyatumia katika kuthibitisha kwamba fomula yake ilikuwa sawa:

  • Miller alidai kuwa uelewa wa watu wa wakati wake ilikuwa kwamba patakatifu pa patakatifu kulimaanisha ulimwengu wetu tunamokaa..
  • Kutakaswaa kwa Ulimwengu tena kwa moto kulikuwa na maana ya kufikia mwisho na kufikia mwisho kwa dunia maana yake ni Yesu Kurudi?
Nini kilitokea baada ya Fomula ya kurudi Yesu kugunduliwa?

Baada ya Miller kuwa amechoropoka na fomula yake alianza kupita huko na huko akiwahubiria watu ili wachukue tahadhari kwa kujiandaa kumpokea Yesu.Miongoni mwao alikuwa mwanamama anayedaiwa kuwa “Nabii mahiri” sana kuwahi kutokea hapa duniani(kwa sababu aliwahi kupewa maono zaidi ya 2000) kusimika usabato duniani na ambaye anatajwa kuwa ndiye amepewa “maono” juu ya jinsi ambavyo Papa atawafumusha wasabato waanze kusali Jumamosi siku zijazo.

Msimamo wa yesu juu ya mwisho wa dunia

Utakumbuka kuwa Kitabu cha Daniel kiliandikwa miaka mingi sana kabla Yesu hajazaliwa.Na utaona kwamba hata Kanuni ya Miller juu ya kurudi kwake ilianza kuhesabiwa mwaka 457BK. Kwa hiyo, wakati Yesu anazaliwa kitabu cha Daniel kilikuwepo tayari na hizo habari za kutakaswa Patakatifu pa Patakatifu Yesu alikuwa amezisoma.

Pamoja na ukweli huo wote kwamba Yesu alikuwa amekisoma kitabu hicho bado alipoulizwa juu ya mwisho wa dunia alisema hivi kwa kadri ya Injili ya Matayo 24:35-38:

“35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina.”

Analysis ya Sadikifu ya “Mwanahisabati” Miller

Kwa kuisoma Sadikifu (thesis) ya Miller na msimamo wa Yesu juu ya mwisho wa dunia,yafuatayo yanajitokeza:

1. Miller na wenzie walikosea wapi katika fomula yao kiasi kwamba Yesu hajawahi kuonekana toka mwaka 1843?

2. Je, wanahisabati wanaweza kuendeleza pale Miller na wenzie walipoishia katika kukokotoa mwisho wa dunia kwa kuihakiki hiyo fomula ya Kisabato juu ya kurudi kwa Yesu?

3. Je, Miller na wenzie hawakuwa wamefanikiwa kulisoma Agano Jipya ambamo msimamo wa Yesu juu ya tarehe ya mwisho wa dunia unawekwa wazi wazi kuwa tarehe husika haijulikani?

4. Je, ikiwa Miller na wafuasi wake akiwemo Mama wa “maono”,Ellen White, walikuwa wamelisoma Agano Jipya ni kwa nini wao waliamua kuasisi Fomula ya jambo ambalo Yesu alikwisha kusema hana uwezo nalo?

5. Je, kwa Yesu kusema haijui tarehe halafu Miller na Ellen White wakaja wakasema wanaifahamu tarehe ina maana Wasabato hao na wa leo mbingu ni yao kiasi kwamba wanaingia na kutoka hata wameweza kushirikishwa yanayoendelea huko Mbinguni?

6. Je, kwa Miller na Ellen kukubaliana kwamba wao walikuwa wameipata fomula ya kurudi kwa Yesu walimaanisha kwamba wao walikuwa ni wasomi sana na kwamba Yesu kusema haijui tarehe kulimaanisha Yesu alikisoma Kitabu cha Daniel na kutokikielewa au kwamba Yesu alikuwa anasoma mambo kwa kurukaruka?

7. Je, hadi sasa tumsikilize nani kati ya Yesu na wasabato juu ya mwisho wa dunia kwa sababu Ellen White ameshapewa maono yanayoonyesha kwamba Yesu ameshaanza kushuka na kwamba kwa sasa yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu sana ambako anapitia majina ya wasabato na akitoka hapo moja kwa moja anatia timu hapa duniani?

Kwa yote hayo,sasa KARIBUNI kwa mjadala.
 
Ilishaandikwa "Hakuna ajuaye siku wala saa ya kurudi kwa mwana wa Adam" ikimaanisha kurudi kwa Yesu Kristo ni siri ya Mungu mwenyewe, kwahiyo huyo Miller na wapuuzi wenzie waondolee huko upuuzi wao
Wapo wanaojua bwana. Kuna watu wanatumia brains zao vizuri. We endelea kulala tu ukiwela mikono chini ya kitovu na kuamka asubuhi mbele pamevimba
 
Wanazuoni:

Kichwa cha habari hapo juu sio kwamba ni cha uchochezi au kwamba kimelenga kupasukia watu kwa kashifa au kwamba ni kufuru kwa Mungu.La hasha, bali ni tafsiri ya kile alichomaanisha Mwanajeshi mmoja huko Marekani pale alipoibuka na Formula ya kukokotoa tarehe ya kurudi kwake Yesu duniani. Jamaa huyo anaitwa WILLIAM MILLER.

William Miller
alizaliwa tarehe 15 Februari1782, huko Jimboni Massachusetts, Marekani na kisha kulelewa katika familia ya Kikristu iliyokuwa na makazi yake Jimbo la New York ya Kaskazini.Familia ya William Miller ilikuwa ya Kibaptisti. Babu yake na wajomba zake wawili walikuwa ni wachungaji katika kanisa la Wabaptisti. Kanisa la Kibaptisti, ni mumeguko karne ya 17 BK kutoka Kanisa la England,yaani Kanisa la Serikali ya Uingereza (Anglikani) ambalo leo linaitwa Lutheran Church.

Miller, katika ujana wake alipata kujiunga na jeshi laMarekani na kufikiaCheo cha Kapteini, wakati wa vita kati ya Marekani na Uingereza (Great Britain) mnamo mwaka 1812.Na inasemekana alikuwa na akili sana na kwamba alikuwa na kipaji cha kufafanua mambo.Bwana Miller baada ya kumaliza utumishi wake Jeshini na kurudi toka vitani (kati ya Marekani na Uingereza mwaka 1812), alianzisha makazi katika Shamba lake huko Low Hampton, New York, ambamo alikuwa amejenga nyumba na akawa akiishi hapo na wakati fulani akawa akienda kusali kwenye kanisa la Baptist la karibu yake.

Bwana Miller kwa kujishughulisha na mambo ya kiimani alipata kuwa mwana-DEIST,yaani alipata kuamini katika Falsafa ya Deism.

Deism ni Falsafa inayokazia kwamba Mungu hajihusishi moja kwa moja na mambo ya ulimwengu huu; kwamba yeye ndiye muumba wa vyote na kwamba ni mkamilifu lakini mungu huyo, hajiingizi katika mambo ya ulimwengu unaonekana kwa njia ya miujiza na kuwa ufunuo sio chimbuko pekee la maarifa juu ya imani na kwamba kufikiri tu kwa mwanadamu na kufanya utafiti juu ya maumbile kunatosha kufahamu na kubainisha kwamba kuna Mungu mmoja.

Kwa hiyo, tafsiri ya imani hii ya Deism ni kwamba Mungu baada ya kuumba ulimwengu alijiondokea zake na kuacha vitu vyote tuvirithi na tokea wakati huo hana mpango navyo tena na wala hajali yanayoendelea huku duniani.

SASA katika mkururu huo wa kutaka kuchimbua mambo magumu ndio William Miller alijikuta akivamia suala ambalo ndio kiini cha mjadala huu wa leo.Ni suala la tarehe ya kurudi kwa YESU KRISTU.

Ni hivi, kwa muda miaka miwili William Miller alipata kujichimbia ndani kwake “akibundi” au akibukua Biblia na ndipo katika kukisoma Kitabu cha Nabii Daniel, sura 8:13-19 ambacho kiliandikwa kabla hata Yesu hajazaliwa akagundua fomula ya kukotoa tarehe ya kurudi kwa Yesu duniani ambako inasomeka hivi:

“13Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa. 15 Ikawa mimi, naam, mimi Danieli, nilipoyaona maono hayo, nalitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu.16 Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya.17 Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.18 Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.19 Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa.”

Kanuni ya Miller inadai kwamba kinabii siku moja kwa Mungu ni sawa na mwaka mmoja wa Kalenda ya wakati huo na hata sasa. Kwa msingi hiyo, siku alizoziongelea Daniel kwa jicho la Miller ni sawa na miaka 2,300 kwa kutumia Kalenda ya wakati huo ambayo ilikuwa ni ya Gregori na ambayo inatumika hadi sasa. Kalenda ya Gregori ilianza kutumika nchini Marekani mwaka 1752. (Kalenda ya Gregori ilizinduliwa rasmimwaka 1582 na kuanza kutumiwa na nchi kama Ufaransa, Italia, Polandi, Ureno na Uhispania).

Katika Sadikifu(thesis) hiyo ya Miller, alikaza kudai kwamba wapo wasomi wengine kama yeye ambao tafiti zao zimeonyesha kuwa tarehe ya kurudi kwa Yesu INAKOKOTOLEKA KIRAHISI SANA. Miongoni mwa wanazuoni waliotajwa alikuwa ni Mwanasayansi Sir Issac Newton.Huyu kwa mjibu wa Miller anadai naye alipata kufanya hesabu kama zake (alipokuwa akitafiti juu ya Kanuni za asili zinazotawala mvutano kati ya Dunia na Jua, Laws of Gravity) na kupata majibu sawa na ya Miller juu ya unabii huo wa Biblia wa kurudi kwa Yesu, na kwamba Newton aliacha maandishi mengi sana juu ya jambo hilo!

Kwa maelezo ya Miller na kwa kadri ya “ufunuo wake” na kwa kanuni yake (ya Kitabu cha Daniel) na kwa kusoma historia, aliweza kwa hakika kwa madai yake kuona kuwa mwaka wa kuanza kuhesabika hizo siku 2,300 ambazo ni sawa na miaka 2,300 ilikuwa mwaka 457K.K. Kwa hiyo, kwa kutumia alichofanya ni kuchukua huo mwaka 457BK ns kutoa miaka 2,300 na hivi kupata jibu la 1843 kwamba ndiyo ingalikuwa ni muda wa kutakaswa “patakatifu pa patakatifu.” Hata hivyo baadaye tarehe ilisogezwa mbele hadi tarehe 22 Oktoba 1844.

Mathematically,Kanuni ya Miller ilikuwa ni hii:

2,300-457=1843 (siku ya kuingia Yesu duniani).

Vigezo alivyotumia Miller katika kuthibitisha Sadikifu yake

Kuna mambo mawili Miller aliyatumia katika kuthibitisha kwamba fomula yake ilikuwa sawa:

  • Miller alidai kuwa uelewa wa watu wa wakati wake ilikuwa kwamba patakatifu pa patakatifu kulimaanisha ulimwengu wetu tunamokaa.
  • Kutakaswaa kwa Ulimwengu tena kwa moto kulikuwa na maana ya kufikia mwisho na kufikia mwisho kwa dunia maana yake ni Yesu Kurudi?
Nini kilitokea baada ya Fomula ya kurudi Yesu kugunduliwa?

Baada ya Miller kuwa amechoropoka na fomula yake alianza kupita huko na huko akiwahubiria watu ili wachukue tahadhari kwa kujiandaa kumpokea Yesu.Miongoni mwao alikuwa mwanamama anayedaiwa kuwa “Nabii mahiri” sana kuwahi kutokea hapa duniani(kwa sababu aliwahi kupewa maono zaidi ya 2000) kusimika usabato duniani na ambaye anatajwa kuwa ndiye amepewa “maono” juu ya jinsi ambavyo Papa atawafumusha wasabato waanze kusali Jumamosi siku zijazo.

Msimamo wa yesu juu ya mwisho wa dunia

Utakumbuka kuwa Kitabu cha Daniel kiliandikwa miaka mingi sana kabla Yesu hajazaliwa.Na utaona kwamba hata Kanuni ya Miller juu ya kurudi kwake ilianza kuhesabiwa mwaka 457BK. Kwa hiyo, wakati Yesu anazaliwa kitabu cha Daniel kilikuwepo tayari na hizo habari za kutakaswa Patakatifu pa Patakatifu Yesu alikuwa amezisoma.

Pamoja na ukweli huo wote kwamba Yesu alikuwa amekisoma kitabu hicho bado alipoulizwa juu ya mwisho wa dunia alisema hivi kwa kadri ya Injili ya Matayo 24:35-38:

“35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina.”

Analysis ya Sadikifu ya “Mwanahisabati” Miller

Kwa kuisoma Sadikifu (thesis) ya Miller na msimamo wa Yesu juu ya mwisho wa dunia,yafuatayo yanajitokeza:

1. Miller na wenzie walikosea wapi katika fomula yao kiasi kwamba Yesu hajawahi kuonekana toka mwaka 1843?

2. Je, wanahisabati wanaweza kuendeleza pale Miller na wenzie walipoishia katika kukokotoa mwisho wa dunia kwa kuihakiki hiyo fomula ya Kisabato juu ya kurudi kwa Yesu?

3. Je, Miller na wenzie hawakuwa wamefanikiwa kulisoma Agano Jipya ambamo msimamo wa Yesu juu ya tarehe ya mwisho wa dunia unawekwa wazi wazi kuwa tarehe husika haijulikani?

4. Je,ikiwa Miller na wafuasi wake akiwemo Mama wa “maono”,Ellen White, walikuwa wamelisoma Agano Jipya ni kwa nini wao waliamua kuasisi Fomula ya jambo ambalo Yesu alikwisha kusema hana uwezo nalo?

5. Je,kwa Yesu kusema haijui tarehe halafu Miller na Ellen White wakaja wakasema wanaifahamu tarehe ina maana Wasabato hao na wa leo mbingu ni yao kiasi kwamba wanaingia na kutoka hata wameweza kushirikishwa yanayoendelea huko Mbinguni?

6. Je,kwa Miller na Ellen kukubaliana kwamba wao walikuwa wameipata fomula ya kurudi kwa Yesu walimaanisha kwamba wao walikuwa ni wasomi sana na kwamba Yesu kusema haijui tarehe kulimaanisha Yesu alikisoma Kitabu cha Daniel na kutokikielewa au kwamba Yesu alikuwa anasoma mambo kwa kurukaruka?

7. Je, hadi sasa tumsikilize nani kati ya Yesu na wasabato juu ya mwisho wa dunia kwa sababu Ellen White ameshapewa maono yanayoonyesha kwamba Yesu ameshaanza kushuka na kwamba kwa sasa yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu sana ambako anapitia majina ya wasabato na akitoka hapo moja kwa moja anatia timu hapa duniani?

Kwa yote hayo,sasa KARIBUNI kwa mjadala.
Umeandika kiushabiki sana. Lengo lako ni kuwaattack wasabato na wala si vinginevyo.

Mambo mengi uliyoeleza hapa si ya kweli, kama ifuatavyo.

1. Miller haukuwa msabato na hata kipindi akiwa anahubiri kurudi kwa Yesu, hapakuwa na dhehebu la kisabato.

2. Mama White pia hakuwa msabato kipindi hicho maana hapakuwa na hilo dhehebu, na wala hakuwa mwanzilishi wa hiyo kanuni ya kurudi Yesu unayoisema, isipokuwa alikuwa mfuasi wa Miller.

3. Papa hatawafumusha wasabato kusali jumamosi kama ulivyodai, badala yake atawalazimisha watu wote kusali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili) badala ya siku ya saba ya juma (yaani Jumamosi).

4. Yesu yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu mbinguni akifanya huduma ya uombezi, na si kwamba ameshaanza kushuka kuja duniani kama unavyodai. Maana patakatifu pa patakatifu ni mbinguni.

5. Wasabato hawaja set siku yoyote ya kuja kwa Yesu kama unavyotaka kuwaaminisha watu, badala yake wamaamini kwamba Yesu amekaribia sana maana dalili karibia zote zimeshatimia.

6. Pamoja na kukosoa mahesabu ya Miller kuhusiana na unabii wa Daniel wa siku 2,300, hujatoa tafsiri mbadala wa unabii huo kana k
kwamba unabii huo hauna maana yoyote kwa wanadamu wa leo.

7. Ukweli ni kwamba, mahesabu ya Miller yalikuwa sahihi, kwamba mwaka 1844 kulikuwa na tukio kubwa lilikuwa linaenda kutokea. Kosa la Miller ni kwamba, alitafasri vibaya kuwa hekalu ni dunia na kutakaswa kwa Hekalu ni dunia kusafishwa kwa moto (kama ulivyoelezea vizuri kabisa).

Ukitaka kujua tafasri ya huo unabii wa siku 2,300 unakaribishwa kuuliza.
 
Hiyo namba NNE umeitoa kwenye andiko gani?
 
. Miller haukuwa msabato na hata kipindi akiwa anahubiri kurudi kwa Yesu, hapakuwa na dhehebu la kisabato.
Hakuna mahali mtoa mada kasema William Miller alikuwa Msabato.....Toka nimesoma bandiko lake nimeona kuwa William Miller alikuwa M-baptist ...

Ila kuna uhusiano Mkubwa kati ya Miller na Seventh Day Adventist

Ngoja wajuvi waje tuendelee kuwasikiliza
 
Mama White pia hakuwa msabato kipindi hicho maana hapakuwa na hilo dhehebu, na wala hakuwa mwanzilishi wa hiyo kanuni ya kurudi Yesu unayoisema, isipokuwa alikuwa mfuasi wa Miller.
Ume-panic sana mpaka inafikia hatua umeamua kujitungia mambo....Hebu kaa chini usome mada ueleww.....mbona mada ina mlenga nwana hisabati nguli wa kukokotoa tarehe Bw William Miller....

Mada haimuongelei Ellen G White.....Kwanini unalazimisha kumuweka Ellen G White....?
 
Papa hatawafumusha wasabato kusali jumamosi kama ulivyodai, badala yake atawalazimisha watu wote kusali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili) badala ya siku ya saba ya juma (yaani Jumamosi).
Mkuu tulia...usome mada uelewe.....

Hebu tuanbie labda itawezekanaje huyo Papa kuwalazimisha watu kusali Jumapili angali dunia hii kuna uhuru wa kuabudu....mbona ni kichekesho cha karne hiki...

Haya labda utuambie haya umeyapatia wapi....?
 
. Yesu yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu mbinguni akifanya huduma ya uombezi, na si kwamba ameshaanza kushuka kuja duniani kama unavyodai. Maana patakatifu pa patakatifu ni mbinguni.
Hapa ndio patamu sana.....Hiki nacho ni kituko kingine cha karne..

Sasa kwa hiki ulichokiandika ndio kitatuonesha muunganiko wa William Miller na genge lake la Ellen G White..

Na pia tutaona kwanini hata leo Wasabato bado wanaendeleza ile roho ya William Miller ya Kutabiri mambo....Wenyewe Wasabato wanaita "Roho ya kinabii'

Mkuu umerukia mambo makubwa sana angali sisi bado tupo na Bw. Miller...huko kumsingizia Yesu amejibanza kwenye kauchochoro mbinguni ni baadae sanaa...
 
Ukweli ni kwamba, mahesabu ya Miller yalikuwa sahihi
Mwanzoni ulimkana Miller na sasa kwa ujanja unakubali.... Hiki ni kituko kingine...ehhhh
,
kwamba mwaka 1844 kulikuwa na tukio kubwa lilikuwa linaenda kutokea
Hapa ndio pa tamu sasa.....Kama ulikuea hunui Bwana Joseph Bates ndiye aliyanza kumsafisha William Miller baada ya Great Disappointment....kisha baadae ndio akaja Bi Ellen G White.....

. Kosa la Miller ni kwamba, alitafasri vibaya kuwa hekalu ni dunia na kutakaswa kwa Hekalu ni dunia kusafishwa kwa moto (kama ulivyoelezea vizuri kabisa).

Sasa mkuu wewe unsonekana una uelewa kidogo wa mambo ya Kisabato...utatusaidia kujibu maswali yetu ...

japo umeanza kwa kukanusha kuwa humjui miller na wala hakuna msabato na hana mahusiano na usabato, hali kijanja ukaja kumkubali.....
 
2 Petro 8 inasema siku moja ni sawa na miaka elfu. Pengine hapo ndio hesabu zilipopishana. Ila swali utaanza kuihesabu tangu lini mpaka lini?
Kwa Kalenda ipi...

Utatumia hii hii ya Wakatoliki ya Gregorian...?
 
Back
Top Bottom