Kisa cha ''magaidi'' wawili: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
KISA CHA ''MAGAIDI'' WAWILI: SHEIKH RAMADHANI RAJAB CHAMBUSO NA SHEIKH AHMADA KIDEGE

''Akauliza muulizaji katika kuwahoji kwa shutuma za ugaidi ni nani anawalipa kwa kazi hiyo ya kusomesha Qur'an.

Jibu likatoka kuwa hakuna anaewalipa ila wanaifanya kazi hiyo ili Allah awaridhie na kesho kiama awatie peponi.''

Charles Dickens ameandika kitabu maarufu, ''A Tale of Two Cities.''

Nimechukua jina la kitabu hiki kufanya ndiyo anuani ya hii makala ambayo kwa kweli nimeaindika mwaka wa 2016 lakini nimeona niiweke tena upya watu waisome kwa kuwa muda uliopita unaweza kutufunza mengi ya manufaa katika hili tatizo la Waislam wanaosomesha Qur'an kukamatwa na kufunguliwa kesi za ugaidi.

Kama ilivyokuwa kwa Masheikh wa Uamsho ushahidi haupatikani na baada ya watuhumiwa kuteseka gerezani huachiwa.

Vijana hawa wawili wote ni waalim wa Qur'an na vijana wazuri na wema wao unafahamika na kila mtu mjini Tanga wanapoishi na kufundisha Uislam.

Kwa sifa hizi zao walipokamatwa kwa vipindi tofauti kwa tuhuma za ugaidi watu walisema, ''Si bure kuna jambo Chambuso na Ahmada walezi na walimu wa wanetu hawawezi kuwa magaidi.''

Hili jambo ni lipi?

Mpenzi msomaji wangu makala hii inaweza kukutegulia kitendawili hiki.

Soma na tafakari na ukimaliza kutafakari waombee dua vijana wetu wanaoshughulika na kukisomesha kitabu cha Allah:

"Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso ni katika vijana wadogo wa Tanga niliopata kusubiana naye kwa kipindi cha miaka 15 niliyoishi Tanga.

Nilifahamiana pia na mwenzake Ahmada Kidege ambao wote wakishughulika na kusomesha Uislam.

Sheikh Chambuso yeye ndiye alikuwa karibu na mimi zaidi.

Nilimjua kama mwalimu wa Islamic Knowledge akipita shule za sekondari akisomesha wanafunzi wa Kiislam elimu ya dini yao.

Kabla hatujafahamiana vizuri tulikuwa tukipishana alfajr tukifanya mazoezi ya kukimbia Barabara ya Bombo.

Nakumbuka kumuona akitembea kwa miguu shule moja baada ya nyingine jasho likimtoka kwenda kuwahi kipindi mimi nikiwa katika gari yangu na kiyoyozi kinaunguruma.

Wakati ule sikuwa sana karibu na yeye lakini nilipokuja kumzoea nikajafahamu kuwa anasomesha kote mjini na nje ya mji kwa kujitolea.

Haukupita muda alinunuliwa baiskeli na muhisani aliyeguswa na juhudi ile ya kijana mdogo kujitolea kuwasomesha watoto dini ya Allah bila ya malipo yoyote yeye akitegemea radhi za Allah.

Huu ukawa pia ni mwanzo wa uhusiano wangu na Sheikh Chambuso ikawa na mimi kwa namna yangu nasoma kwake kila tunapokuwa pamoja katika mazungumzo ya kawaida tu.

Ukiwa karibu ya waridi hukosi kunukia.

Sheikh Chambuso akanisoemsha historia ya Tanga na taasisi zake kubwa za Uislam kama Shamsiyya, Zahrau na Maawal Islam na baadae Shamsi Maarif ilipokuja kuanzishwa wakati mimi bado nipo Tanga.

Sheikh Chambuso ni kijana maarufu mjini kwa ile heshima yake ya kumtumika Allah na waja wake.

Waarabu wana msemo kuwa, "Anaewatumikia watu ndiye bwana wao."

Wanafunzi waliopita mikononi mwake kuwasomeshsa hawana idadi.

Kupitia Sheikh Chambuso na mimi rafiki na nduguye nikawa nasafiria nyota yake nikifahamika kama ‘’rafiki yake Chambuso.’’

Sheikh Chambuso hakutosheka na kuwa anapita kwenye shule kusomesha akawa sasa anaingia hadi kufanya ushauri kwa wanafunzi wa Kiislam katika wale aliokuwa akiwasomesha dini masomo gani wachukue kwa ajili ya mstakbali wao wa baadae.

Hapa ikawa sasa Sheikh Chambuso anaingia katika anga ambayo kwa hakika ilikuja kuwanufaisha vijana wengi na wengi wao wakafanikiwa.

Lakini kubwa lililokuja kunifurahisha ni pale alipoamua yeye na wenzake kuanzisha shule ya chekechea ya Kiislam na kuanza shule ya msingi.

Sasa tena Sheikh Chambuso akawa anaongeza ulezi juu ya kusomesha.

Madrasa yake na shule ya chekechea ikawa imejaa pomoni.

Mimi binafsi furaha yangu ilikuwa haina kifani.

Sheikh Chambuso akaongeza na ‘’idara,’’ nyingine siyo rasmi akawa anapita kwa Waislam kuwaomba kuwasomesha katika shule yake watoto mayatima na wale ambao wazazi wao Allah amewapa mtihani wa kipato.

Haikuwa ajabu kumuona Sheikh Chambuso amafatana na daktari kumpeleka katika nyumba ili amtie suna mwanafunzi wake ambae kwa shida za umasikini kapita umri wa kutiwa suna.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso.

Siku moja baada ya kutoka Tanga kwa kustaafu kazi nilirudi Tanga na nikenda kumtembelea Sheikh Chambuso shuleni kwake.

Ile kuniona tu na baada ya kusalimiana ghafla akasimamisha masomo katika madarasa yote akawatoa wanafunzi wote nje ya wakapanga mstari ili wanisalimie.

Sheikh Chambuso alikuwa anazugumza na ule mkusanyiko kwa Kiarabu.

Niliyoshuhudia pale niliinamisha kichwa changu chini sikuweza kujizuia.

Machozi yalinilengalenga.

Kumbe mambo haya yanawezekana…

Lakini kuutumikia Uislam kuna changamoto zake hasa nyakati hizi za ''siasa za ugaidi.''

Haukupita muda Sheikh Chambuso akakamatwa na kuwekwa rumande kwa kesi ya ‘’kushawishi mauaji,’’ akawekwa ndani rumande Handeni majuma mawili.

Kasafirishwa kafungwa kitambaa cheusi machoni chini ya ulinzi mkali.

Sheikh Chambuso hana sifa ya uovu mimi binafsi na kila aliyesikia habari hizi alisikitika na kushangaa.

Hii ilikuwa kesi ya kubambikizwa kama ilivyokuja kudhihirika hapo baadae.

Siku ya pili yake zilipopatikana taarifa kuwa Sheikh Chambuso kakamatwa mji mzima wa Tanga ulizizima kwani ni nani asiyemjua Sheikh Chambuso mwalimu na mlezi wa watoto wao?

Ule msururu wa ingia toka nyumbani kwake kuanzia alfajir kuna baadhi ya watu walidhani nyumbani kwake kuna msiba kafa mtu.

Sheikh Chambuso alihangaishwa sana na kesi hii ambayo alinifahamisha kuwa polisi wanaiita, ''kumfunga mtu paka mweusi shingoni.''

Sheikh Chambuso mwenyewe alikuja kunambia kuwa ile kesi imemfunza mengi na imemuongezea elimu ambayo asingeweza kuipata popote.

Kwangu mimi ikawa sasa Sheikh Chambuso kawa shule na mwalimu pia na mimi nasoma kwake na kujifunza.

Hii ilipelekea mimi kuandika mengi kuhusu madhila mengi yanayowakabili Waislam kiasi nilimkaribisha msikiti kwetu aje kuzungumza na Waislam na nilimwekea ukurasa makhsusi kwa ajili yake katika kipindi chote alichokuwa mahakamani kujibu tuhuma za ''kushawishi mauaji:''

Ukurasa huu wa Sheikh Chambuso ulisomwa na watu wengi sana na ulikuwa na taarifa nyingi za uchunguzi kwa kuhusu ukweli wa tuhuma za ugaidi dhidi ya Waislam.

Huwa kila akija Dar es Salaam basi Sheikh Chambuso atanipitia kwangu kunijulia hali na kunieleza shule inavyokwenda na taarifa nyingine za vijana wa Kiislam Mkoani Tanga.

Mara ya mwisho nilipokutananae nilimuuliza kuhusu mwanafunzi wake mmoja bint nillitaka kujua maendeleo yake.

Sheikh Chambuso akaniambia, ‘’Yule bint anamaliza shahada yake ya Udaktari.’’

Kama nilivyotahadharisha hapo awali.

Kabla hatujaagana Sheikh Chambuso akanifahamisha kuwa wamefungua shule ya ushoni kwa wasichana inayoongozwa na Sheikh Khamisi Shemtoi ambae yeye mwenyewe licha ya kuwa sheikh ni fundi cherahani bingwa.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso na wenzake kila unapokutananao basi watakuwa na jema la kukueleza kukufurahisha.
Kubwa ninalofaidi kwa Shekh Chambuso ni kule kunifunza misemo ya Kiarabu ambayo imekuwa silaha yangu kubwa katika mijadala.
Mathalan siku moja tunazungumza jambo akanipa jibu kwanza kwa Kiarabu kisha akanifanyia tafasiri akasema, ''Ukiijua sababu inaondoa ajabu.''

Kuna mfano mmoja alinipa kueleza jambo lililovurugika na watu kujaribu kulirejesha kama lilivyokuwa hapa mwanzo.

Akanambia, ''Sheikh Mohamed chukua mfano wa kioo kishavunjika na wewe ukajaribu kukiunga, hakiwezi kuwa kama kilivyokuwa hapo mwanzoni.

Ukijitazama na kioo hicho utaiona tofauti.''

Sheikh Chambuso anasema yeye misemo hii kafundishwa na Sheikh wake Marehemu Sheikh Mohamed Ayub.

Siku moja tulikuwa katika gari yangu nikaweka CD ya Sheikh Mohamed Ayub anadarsisha tafsir ya Qur'an darsa za L'Asr Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Msomaji kasoma aya mbili tatu kamaliza Sheikh Mohamed Ayub anaanza kusomesha.
Nikamuona Sheikh Chambuso ghafla uso umembadilika kajiinamia akanambia, ''Sheikh Mohamed mimi hapo nipo sisi wanafunzi wadogo tuko safa ya nyuma mbele pale namuona sheikh mwenyewe kazungukwa na wanafunzi wake wakubwa ambao ndiyo walikuwa walimu wetu sisi, Sheikh Mohamed Bakari, Sharif Sayydid Hussein, Sheikh Zuher bin Ali bin Hemed bin Al Buhry...''

Sheikh Chambuso hakika ni kijana hazina kwa watu wa Tanga na umma wa Waislam wa Tanzania kwa usomi wake makini na jinsi amavyojibiidisha kuitumikia jamii.

Sheikh Ahmada Kidege hivi sasa yuko Gerezani kwa tuhuma za ugaidi na wakati anakamatwa alikuwa anasimamia ujenzi wa hospitali kwa ajili ya wanawake.

Picha: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso akigawa mashafu tafasiri ya Sheikh Ali Muhsin Barwani kwa wanafunzi wake St. Christina Secondary School Tanga
Picha ilipigwa 2006 wakati akiwa Sheikh na Mwalimu ''mtoto.''

Picha ya pili kulia ni Sheikh Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege.

Screenshot_20210618-073942_Gallery.jpg
 
Mwambieni Samia atawatoa.
Kipaji,
Mimi huwa siandiki kwa nia ya kutoleana jeuri na wasomaji.

Hupenda kalamu yangu ielimishe jamii.

Hapa nimeeleza vipi ninavyowajua hawa vijana kama walimu na watu wema.

Naeleza kuwa labda kama ni kosa ni kuwa kuna nguvu nchini ina uoga na chuki na Uislam.

Hofu na chuki kama zipo vyote havina sababu.

Jamii inahitaji kujulishwa haya na ndiyo maana nikaweka picha ya Sheikh Chambuso yuko ndani ya darasa la shule ya wasichana anawafunza Uislam.

Siku hii alinialika kwa sababu tulikuwa tumewapelekea wanafunzi zawadi ya Qur'an.

Nini Sheikh Chambuso anawafunza mabinti zetu?

Anawafunza maneno ya Allah waje kuwa mama wema wajenge familia bora.
 
Interesting...imekuwaje wamefungwa sababu ya ugaidi kama hawana shida na mtu yoyote? Kumuonea mtu sio sawa. Ila mtu anayejihusisha na mabo yasiyotakiwa akiwajibishwa pia tusiseme anaonewa
Rogo...
Sheikh Chambuso aliachiwa na mahkama kwa kuwa hakuwa na kosa.

Hakuwaficha waliokuwa wakimhoji huku wakimkejeli na kumtisha kuwa yeye ni mwalimu wa Qur'an.

Alipokuwa Handeni rumande wafungwa walikuwa wanamuheshimu na askari jela Waislam walikuwa wakipita mbele yake wakiinamisha shingo kwa heshima.

Na siku alipoachiwa jela nzima wafungwa waliingia simanzi.

Sheikh alikuwa akisimama kusalisha alikuwa akiwastarehesha kwa kiraa cha Qur'an akiwasomea zile aya Allah anazowatia matumaini watu wema wanaomuamini Mungu mmoja kuwa ushindi siku zote utakuwa wao.

Hawa nduguze walikuwa wanasikitika kuwa hawataisikia tena Qur'an ikisomwa kama alivyokuwa akiisoma Sheikh Chambuso.
 
Tanga hasa maeneo ya Handeni na kule Amboni kwenye mapango mmnh!

Serikali izidi kuimarisha udhibiti (Controls) ambazo zitawawezesha ku detect uharifu wa kigaidi kabla ya kutokea na kuleta madhara makubwa.

Nazani wawe makini hata kwa maeneo mengine Pia yasiyo na viashiria kwa tahadhari zaidi.

Wazidi kuwa proactively.

Nani angejua mwanafunzi wa Kule Dodoma Bihawana angefundishwa Ugaidi?

Wakasema alikuwa haingii darasani muda mwingi alikuwa msikitini.

Mama yake mzazi akiongea kwa masikitiko makubwa na majonzi mazito.

Mzazi anajua mtoto kaenda Shule kusoma kumbe?!

Yule Mtanzania alokamatwa chuo kikuu Garisa nchini Kenya?!

Na haijulikani kama akifundishwa peke yake au kuna wenzie wengine of which is most likely!
 
Tupendane!

Hakuna mwanadamu alojiumba mwenyewe.

Hakuna mwanadamu alofanya bidii ya kujiumba na kuzaliwa.

Sote tumejikuta tushaumbwa na kuzaliwa.

Ukimchukia binadamu mwenzio kiasi cha kutaka kumuua maana yake unamfanya Mungu alomuumba kuwa mkosa.

Tudumishe amani yetu na kuienzi kwa manufaa yetu na vizazi vyetu.
 
Tanga hasa maeneo ya Handeni na kule Amboni kwenye mapango mmnh!

Serikali izidi kuimarisha udhibiti (Controls) ambazo zitawawezesha ku detect uharifu wa kigaidi kabla ya kutokea na kuleta madhara makubwa.

Nazani wawe makini hata kwa maeneo mengine Pia yasiyo na viashiria kwa tahadhari zaidi.

Wazidi kuwa proactively.

Nani angejua mwanafunzi wa Kule Dodoma Bihawana angefundishwa Ugaidi?

Wakasema alikuwa haingii darasani muda mwingi alikuwa msikitini.

Mama yake mzazi akiongea kwa masikitiko makubwa na majonzi mazito.

Mzazi anajua mtoto kaenda Shule kusoma kumbe?!

Yule Mtanzania alokamatwa chuo kikuu Garisa nchini Kenya?!

Na haijulikani kama akifundishwa peke yake au kuna wenzie wengine of which is most likely!
Vipi kesi ya yule padri aliyekamatwa Na bunduki Na bastola Na makasha ya risasi, iliishia wapi?
 
Padri kama raia anaruhusiwa kumiliki silaha kwa mujibu wa sheria za nchi.

Walikamatwa watu 50 ,

Katika silaha 48 yake ni moja ambayo imethibitika anaimiki kihalali.

Tatizo liko wapi hapo?

Soma ile taarifa kwa utulivu between lines.

Halafu mimi nimejifunza kuwa fair na honest ,

Haijalishi ni mtu ni ndugu yangu , au mtu wa imani yangu siwezi mtetea kwa vyovyote vile hata pale ambapo amefanya makosa itakuwa dhambi kubwa sana machoni pa mwenyezi Mungu na Wanadamu.

Awe padre awe askofu akifanya makosa na ikathibitika kuwa mkosa Basi sheria ichukue mkondo wake.

Lakini tabia ya kutetea mtu au watu sababu ni dini yangu mimi siwezi sababu kwa imani yangu ni sawa na udhalimu mkubwa Yani kama vile nafurahishwa na ule uovu waletendea wengine kitu ambacho ni machukizo machoni pa Mungu.
 
Sasa kile kitu najiuliza kwanini makundi karibia yote ya ugaidi ni ya kiislam? kwanzia al qaida, alshabab, isis na hata boko haram? bona hatujawai kusikia kundi lolote la kigaidi la kaa wakiristo, budhaa na wengine,Najua hii itawauma sana waislamu lakini ukweli ni kuwa hii kitabu cha dini ya kiislam, mambo mengi mabya, kaa kulipua mabomu ya kujitoa muhanga, kuua makafili(wale wasioamini dini ya kiislamu na mengine mengi) jiulize kwanini mataifa kaa ya huko warabuni kaa saudi arabia ukiwa wa dini kaa mkiristo adhambu ni kifo? jiulize kwanini huwezi kuta kitu kaa kanisa mahali kaa kuwait na saudi? jiulize bona huko pakistani na mataifa mengine kubadilise dini toka uislamu na kujiunga na dini ingine adhabu ni kifo, au hata kusema vibaya kuhusu mohhamed adhabu ni kifo, kule pakistani **** mama moja mkristo alisingiziwa ati amemutukana mtume mohhamed kahukumiwa kifo, kakaa jela miaka 9 kisa mahaka ya juu ikamuachilia lakini waislamu wakaleta hujo kutaka kumuua mpaka yeyena jamii yake wakatorokea kaifa moja sitalitaja sababu ya usalama wa huyu mama mkristo.bona mataifa kaa pakistan wanateka mabinti wadogo wa kikiristo wana walazimisa kuwaoa na kuwangeuza kuwa waisilamu, ??????? angalia hata jirani yetu musubiji zile kundi la kigaidi la kiisilamu linaua watu bila huruma huko cabo delgado, angalia nigeria, mali, burkina faso, niger vile makundi ya kigaidi ya kiisilamu yanaua wakiristo na hatujawai sikia kundi la kigaidi la kikiristo au dini ingine, kwa maoni yangu iko shida na mafudisho ya kiisilamu
 
Makanisani na misikitini na masinagogi watu wafundishwe kuwapenda binadamu wenzao bila kujali tofauti zao.

Ni kujidanganya kwamba Eti itatokea watu imani fulani wataangamizwa kisha wabaki wa imani nyingine pekeyao.
Mkuu tatizo hizi dini mafundisho yake ndio tatizo, sasa kila mmoja anamuona mwenzake alietofautiana Imani kuwa ni kafiri au mpagani, hii changamoto ni kubwa na inahitajika nguvu kubwa na maarifa mengi kumaliza tatizo hili
 
Wengi katika Watu wapo kishabiki sana katika Dini Elimu kwao ni ziro.Mtu anakuja kuwasifu watu pasi na elimu....eti walikuwa hivi na vile...!!!!

Uislam una misingi yake, na msingi mkuu ni elimu sahihi

Chambuso na kundi lake, kwa Masheikh wa Tanga wanawajua sana, kwanza hawakuwa na elimu sahihi, kisha walikuwa hawana tofauti na Muslim BrotherHood ya Misri kwa upande wa Utikadi.

Kiujumla, hawa wanaoitwa Wanaharakati mfano kwa leo Shee Ponda na genge lake, mrengo wao ni wa uvuragaji katika Dini
Najua siku.... Utakuja hapa Jf(Mohammad Said)na kuja kumsifu iwapo atakutangulia

Mzee wangu(Mohamd Said) naomba ubadili upepo wako wa kuelimisha Jamii... bado pumzi unayo.. kaa chini tena na usome Dini yako kwa lengo la kukuongoza wewe na familia yako kisha umma kwa ujumla

Hii ni nasaha ya bure kwako
Shukran sana
 
Sasa kile kitu najiuliza kwanini makundi karibia yote ya ugaidi ni ya kiislam? kwanzia al qaida, alshabab, isis na hata boko haram? bona hatujawai kusikia kundi lolote la kigaidi la kaa wakiristo, budhaa na wengine,Najua hii itawauma sana waislamu lakini ukweli ni kuwa hii kitabu cha dini ya kiislam, mambo mengi mabya, kaa kulipua mabomu ya kujitoa muhanga, kuua makafili(wale wasioamini dini ya kiislamu na mengine mengi) jiulize kwanini mataifa kaa ya huko warabuni kaa saudi arabia ukiwa wa dini kaa mkiristo adhambu ni kifo? jiulize kwanini huwezi kuta kitu kaa kanisa mahali kaa kuwait na saudi? jiulize bona huko pakistani na mataifa mengine kubadilise dini toka uislamu na kujiunga na dini ingine adhabu ni kifo, au hata kusema vibaya kuhusu mohhamed adhabu ni kifo, kule pakistani **** mama moja mkristo alisingiziwa ati amemutukana mtume mohhamed kahukumiwa kifo, kakaa jela miaka 9 kisa mahaka ya juu ikamuachilia lakini waislamu wakaleta hujo kutaka kumuua mpaka yeyena jamii yake wakatorokea kaifa moja sitalitaja sababu ya usalama wa huyu mama mkristo.bona mataifa kaa pakistan wanateka mabinti wadogo wa kikiristo wana walazimisa kuwaoa na kuwangeuza kuwa waisilamu, ??????? angalia hata jirani yetu musubiji zile kundi la kigaidi la kiisilamu linaua watu bila huruma huko cabo delgado, angalia nigeria, mali, burkina faso, niger vile makundi ya kigaidi ya kiisilamu yanaua wakiristo na hatujawai sikia kundi la kigaidi la kikiristo au dini ingine, kwa maoni yangu iko shida na mafudisho ya kiisilamu
Tajiri...
Ikiwa mtu atajadili tatizo la ugaidi kwa mtazamo wa Marekani na kudhani kuwa Tanzania kuna ugaidi atapata shida kubwa sana.

Matokeo yake ndiyo haya ya juhudi ya kutaka kuaminisha kuwa Tanzania kuna magaidi na magaidi wenyewe ni Waislam.

Waislam wanakamatwa kwa vishindo vikubwa wanatupwa magerezani na kesi zinashindikana kwa kukosa ushahidi.

Hadi hivi sasa tunapojadili kuwekwa kwa mashekh gerezani kwa miaka tisa na ushahidi kukosekana kuwa masheikh walikuwa magaidi, hakuna mahakama yeyote Tanzania iliyoweza kumuhukumu mtuhumiwa yeyote awaye yule kwa kosa la ugaidi.

Anakamatwa Sheikh Chambuso Mwalimu wa kusomesha Qur'an na Islamic Knowledge anapewa tuhuma za ugaidi, mtu ambae hana mafunzo yoyote ya matumizi ya silaha ila kushika chaki mbele ya ubao kufundisha.

Anafungwa kitambaa cheusi usoni akihamishwa Tanga kwenda kuwekwa gerezani Handeni akiwa chini ya ulinzi mkali.

Njia nzima kutoka Tanga hadi Handeni Sheikh Chambuso akiwa katikati ya askari waliosheheni silaha anasoma Surat Yasin na kumsalia Mtume SAW akiomba nusra yake na ya Waislam.

Ndani ya jela Sheikh Chambuso anakuwa Imam wa kusalisha sala zote tano na kusomesha Uislam kiasi wafungwa wenzake wanaambizana kuwa inaelekea kuna nguvu inapiga vita Uislam kwa mgongo wa ugaidi.

Nina ''paper,'' niliwasilisha katika mkutano Chuo Kikuu Cha Ibadan kuhusu ugaidi.
Haya hapo chini ni baadhi ya maneno yaliyomo katika ''paper,'' hii:

''In order to understand the Tanzanian political environment and to appreciate and comprehend the impact of ‘terrorism’ as defined by the United States, first we need to point out that this phenomenon was and still is a problem which involves the government of the United States and to a limited extent its allies.

The shock of 9/11 forced the United States to not only to include its allies in its war against terrorism but also other governments not forming part of the United States geo-political sphere like Tanzania.

It is in this way that Tanzania and other African countries were included in the war against terrorism.

Secondly, we have to look into the perception of associating Islam as an ideology which nourishes terrorism, the notion which seems to be gaining ground.

Thirdly, we have to qualify the notion of ‘terror.’

What kind of violence qualifies to be considered as an act of ‘terrorism’ and therefore deserving condemnation?

At the moment it seems it is only when civilians are targeted for attack that the act assumes the connotations of ‘terror.’

This is in contrast where modern weaponry is used by nation states in annihilation of a people.

Examples of the latter are abound.

The sight of a suicide bomber in television screens is just as familiar as the sight of the Apache helicopters supported by heavy fortified tanks bombing, killing and maiming innocent civilians, be it in Afghanistan, Gaza or Iraq.

Now where do we draw the line between these two scenarios?''

Kwa mukhtasari nilikuwa nasema kuwa Tanzania kwa shinikizo la Marekani imetiwa katika vita ambavo haviwahusu.

Ugaidi umesababishwa na Wamarekani wenyewe kwa ubaya wao dhidi ya mataifa mengine.

Maneno haya yalinisababishia matatizo makubwa sana kwani Wamerekani walikuwapo katika mkutano ule kama wafadhili na waliyachukua maneno yangu katika picha na sauti na walifikisha yote hapa nyumbani ili nishughulikiwe kama inavyostahili.

Haukupita muda mrefu nikirejea Dar es Salaam nilikamatwa Uwanja wa Ndege Dar es Salaam na kuhojiwa na maofisa wa usalama.

Marekani wakaniorodhesha katika orodha yao ya ''Sympathisers,'' yaani wanaohurumia magaidi na pasi yangu ya kusafiria ikawekewa alama maalum ambayo kwa jicho huioni ila ''Passport Control,'' uwanja wa ndege kokote duniani inaonekana.

Matokeo yake watu wa usalama kote unakosafiri wanakufatilia ingawa unaruhusiwa kusafiri na kuingia nchi yeyote.

Inakera kidogo kwani unashughulishwa viwanja vya ndege kwa upekuzi zaidi ya kawaida, unapata shida kutumia ATM nje ya nchi na kwa ufupi unaishi ukihisi kuwa kuna watu wanakutazama muda wote.

Yamenitokea Namanga, Schipol Amsterdam Netherlands, Detroit Marekani na Berlin Ujerumani.

Kisa kwa kusema kweli.
Uonevu bila sababu.

Unaweza kuisoma ''paper'' yote hapo chini:
 
KISA CHA ''MAGAIDI'' WAWILI: SHEIKH RAMADHANI RAJAB CHAMBUSO NA SHEIKH AHMADA KIDEGE

''Akauliza muulizaji katika kuwahoji kwa shutuma za ugaidi ni nani anawalipa kwa kazi hiyo ya kusomesha Qur'an.

Jibu likatoka kuwa hakuna anaewalipa ila wanaifanya kazi hiyo ili Allah awaridhie na kesho kiama awatie peponi.''

Charles Dickens ameandika kitabu maarufu, ''A Tale of Two Cities.''

Nimechukua jina la kitabu hiki kufanya ndiyo anuani ya hii makala ambayo kwa kweli nimeaindika mwaka wa 2016 lakini nimeona niiweke tena upya watu waisome kwa kuwa muda uliopita unaweza kutufunza mengi ya manufaa katika hili tatizo la Waislam wanaosomesha Qur'an kukamatwa na kufunguliwa kesi za ugaidi.

Kama ilivyokuwa kwa Masheikh wa Uamsho ushahidi haupatikani na baada ya watuhumiwa kuteseka gerezani huachiwa.

Vijana hawa wawili wote ni waalim wa Qur'an na vijana wazuri na wema wao unafahamika na kila mtu mjini Tanga wanapoishi na kufundisha Uislam.

Kwa sifa hizi zao walipokamatwa kwa vipindi tofauti kwa tuhuma za ugaidi watu walisema, ''Si bure kuna jambo Chambuso na Ahmada walezi na walimu wa wanetu hawawezi kuwa magaidi.''

Hili jambo ni lipi?

Mpenzi msomaji wangu makala hii inaweza kukutegulia kitendawili hiki.

Soma na tafakari na ukimaliza kutafakari waombee dua vijana wetu wanaoshughulika na kukisomesha kitabu cha Allah:

"Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso ni katika vijana wadogo wa Tanga niliopata kusubiana naye kwa kipindi cha miaka 15 niliyoishi Tanga.

Nilifahamiana pia na mwenzake Ahmada Kidege ambao wote wakishughulika na kusomesha Uislam.

Sheikh Chambuso yeye ndiye alikuwa karibu na mimi zaidi.

Nilimjua kama mwalimu wa Islamic Knowledge akipita shule za sekondari akisomesha wanafunzi wa Kiislam elimu ya dini yao.

Kabla hatujafahamiana vizuri tulikuwa tukipishana alfajr tukifanya mazoezi ya kukimbia Barabara ya Bombo.

Nakumbuka kumuona akitembea kwa miguu shule moja baada ya nyingine jasho likimtoka kwenda kuwahi kipindi mimi nikiwa katika gari yangu na kiyoyozi kinaunguruma.

Wakati ule sikuwa sana karibu na yeye lakini nilipokuja kumzoea nikajafahamu kuwa anasomesha kote mjini na nje ya mji kwa kujitolea.

Haukupita muda alinunuliwa baiskeli na muhisani aliyeguswa na juhudi ile ya kijana mdogo kujitolea kuwasomesha watoto dini ya Allah bila ya malipo yoyote yeye akitegemea radhi za Allah.

Huu ukawa pia ni mwanzo wa uhusiano wangu na Sheikh Chambuso ikawa na mimi kwa namna yangu nasoma kwake kila tunapokuwa pamoja katika mazungumzo ya kawaida tu.

Ukiwa karibu ya waridi hukosi kunukia.

Sheikh Chambuso akanisoemsha historia ya Tanga na taasisi zake kubwa za Uislam kama Shamsiyya, Zahrau na Maawal Islam na baadae Shamsi Maarif ilipokuja kuanzishwa wakati mimi bado nipo Tanga.

Sheikh Chambuso ni kijana maarufu mjini kwa ile heshima yake ya kumtumika Allah na waja wake.

Waarabu wana msemo kuwa, "Anaewatumikia watu ndiye bwana wao."

Wanafunzi waliopita mikononi mwake kuwasomeshsa hawana idadi.

Kupitia Sheikh Chambuso na mimi rafiki na nduguye nikawa nasafiria nyota yake nikifahamika kama ‘’rafiki yake Chambuso.’’

Sheikh Chambuso hakutosheka na kuwa anapita kwenye shule kusomesha akawa sasa anaingia hadi kufanya ushauri kwa wanafunzi wa Kiislam katika wale aliokuwa akiwasomesha dini masomo gani wachukue kwa ajili ya mstakbali wao wa baadae.

Hapa ikawa sasa Sheikh Chambuso anaingia katika anga ambayo kwa hakika ilikuja kuwanufaisha vijana wengi na wengi wao wakafanikiwa.

Lakini kubwa lililokuja kunifurahisha ni pale alipoamua yeye na wenzake kuanzisha shule ya chekechea ya Kiislam na kuanza shule ya msingi.

Sasa tena Sheikh Chambuso akawa anaongeza ulezi juu ya kusomesha.

Madrasa yake na shule ya chekechea ikawa imejaa pomoni.

Mimi binafsi furaha yangu ilikuwa haina kifani.

Sheikh Chambuso akaongeza na ‘’idara,’’ nyingine siyo rasmi akawa anapita kwa Waislam kuwaomba kuwasomesha katika shule yake watoto mayatima na wale ambao wazazi wao Allah amewapa mtihani wa kipato.

Haikuwa ajabu kumuona Sheikh Chambuso amafatana na daktari kumpeleka katika nyumba ili amtie suna mwanafunzi wake ambae kwa shida za umasikini kapita umri wa kutiwa suna.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso.

Siku moja baada ya kutoka Tanga kwa kustaafu kazi nilirudi Tanga na nikenda kumtembelea Sheikh Chambuso shuleni kwake.

Ile kuniona tu na baada ya kusalimiana ghafla akasimamisha masomo katika madarasa yote akawatoa wanafunzi wote nje ya wakapanga mstari ili wanisalimie.

Sheikh Chambuso alikuwa anazugumza na ule mkusanyiko kwa Kiarabu.

Niliyoshuhudia pale niliinamisha kichwa changu chini sikuweza kujizuia.

Machozi yalinilengalenga.

Kumbe mambo haya yanawezekana…

Lakini kuutumikia Uislam kuna changamoto zake hasa nyakati hizi za ''siasa za ugaidi.''

Haukupita muda Sheikh Chambuso akakamatwa na kuwekwa rumande kwa kesi ya ‘’kushawishi mauaji,’’ akawekwa ndani rumande Handeni majuma mawili.

Kasafirishwa kafungwa kitambaa cheusi machoni chini ya ulinzi mkali.

Sheikh Chambuso hana sifa ya uovu mimi binafsi na kila aliyesikia habari hizi alisikitika na kushangaa.

Hii ilikuwa kesi ya kubambikizwa kama ilivyokuja kudhihirika hapo baadae.

Siku ya pili yake zilipopatikana taarifa kuwa Sheikh Chambuso kakamatwa mji mzima wa Tanga ulizizima kwani ni nani asiyemjua Sheikh Chambuso mwalimu na mlezi wa watoto wao?

Ule msururu wa ingia toka nyumbani kwake kuanzia alfajir kuna baadhi ya watu walidhani nyumbani kwake kuna msiba kafa mtu.

Sheikh Chambuso alihangaishwa sana na kesi hii ambayo alinifahamisha kuwa polisi wanaiita, ''kumfunga mtu paka mweusi shingoni.''

Sheikh Chambuso mwenyewe alikuja kunambia kuwa ile kesi imemfunza mengi na imemuongezea elimu ambayo asingeweza kuipata popote.

Kwangu mimi ikawa sasa Sheikh Chambuso kawa shule na mwalimu pia na mimi nasoma kwake na kujifunza.

Hii ilipelekea mimi kuandika mengi kuhusu madhila mengi yanayowakabili Waislam kiasi nilimkaribisha msikiti kwetu aje kuzungumza na Waislam na nilimwekea ukurasa makhsusi kwa ajili yake katika kipindi chote alichokuwa mahakamani kujibu tuhuma za ''kushawishi mauaji:''

Ukurasa huu wa Sheikh Chambuso ulisomwa na watu wengi sana na ulikuwa na taarifa nyingi za uchunguzi kwa kuhusu ukweli wa tuhuma za ugaidi dhidi ya Waislam.

Huwa kila akija Dar es Salaam basi Sheikh Chambuso atanipitia kwangu kunijulia hali na kunieleza shule inavyokwenda na taarifa nyingine za vijana wa Kiislam Mkoani Tanga.

Mara ya mwisho nilipokutananae nilimuuliza kuhusu mwanafunzi wake mmoja bint nillitaka kujua maendeleo yake.

Sheikh Chambuso akaniambia, ‘’Yule bint anamaliza shahada yake ya Udaktari.’’

Kama nilivyotahadharisha hapo awali.

Kabla hatujaagana Sheikh Chambuso akanifahamisha kuwa wamefungua shule ya ushoni kwa wasichana inayoongozwa na Sheikh Khamisi Shemtoi ambae yeye mwenyewe licha ya kuwa sheikh ni fundi cherahani bingwa.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso na wenzake kila unapokutananao basi watakuwa na jema la kukueleza kukufurahisha.
Kubwa ninalofaidi kwa Shekh Chambuso ni kule kunifunza misemo ya Kiarabu ambayo imekuwa silaha yangu kubwa katika mijadala.
Mathalan siku moja tunazungumza jambo akanipa jibu kwanza kwa Kiarabu kisha akanifanyia tafasiri akasema, ''Ukiijua sababu inaondoa ajabu.''

Kuna mfano mmoja alinipa kueleza jambo lililovurugika na watu kujaribu kulirejesha kama lilivyokuwa hapa mwanzo.

Akanambia, ''Sheikh Mohamed chukua mfano wa kioo kishavunjika na wewe ukajaribu kukiunga, hakiwezi kuwa kama kilivyokuwa hapo mwanzoni.

Ukijitazama na kioo hicho utaiona tofauti.''

Sheikh Chambuso anasema yeye misemo hii kafundishwa na Sheikh wake Marehemu Sheikh Mohamed Ayub.

Siku moja tulikuwa katika gari yangu nikaweka CD ya Sheikh Mohamed Ayub anadarsisha tafsir ya Qur'an darsa za L'Asr Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Msomaji kasoma aya mbili tatu kamaliza Sheikh Mohamed Ayub anaanza kusomesha.
Nikamuona Sheikh Chambuso ghafla uso umembadilika kajiinamia akanambia, ''Sheikh Mohamed mimi hapo nipo sisi wanafunzi wadogo tuko safa ya nyuma mbele pale namuona sheikh mwenyewe kazungukwa na wanafunzi wake wakubwa ambao ndiyo walikuwa walimu wetu sisi, Sheikh Mohamed Bakari, Sharif Sayydid Hussein, Sheikh Zuher bin Ali bin Hemed bin Al Buhry...''

Sheikh Chambuso hakika ni kijana hazina kwa watu wa Tanga na umma wa Waislam wa Tanzania kwa usomi wake makini na jinsi amavyojibiidisha kuitumikia jamii.

Sheikh Ahmada Kidege hivi sasa yuko Gerezani kwa tuhuma za ugaidi na wakati anakamatwa alikuwa anasimamia ujenzi wa hospitali kwa ajili ya wanawake.

Picha: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso akigawa mashafu tafasiri ya Sheikh Ali Muhsin Barwani kwa wanafunzi wake St. Christina Secondary School Tanga
Picha ilipigwa 2006 wakati akiwa Sheikh na Mwalimu ''mtoto.''

Picha ya pili kulia ni Sheikh Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege.

View attachment 1822295
hivi mzee said mfano una binti yako kampenda mkristo utamkubalia aolewe kweli
 
Back
Top Bottom