Kisa cha kweli: Mama wakwe wengine pasua kichwa

Kisa cha kweli: Mama wakwe wengine pasua kichwa

Ni kisa cha ukweli kabisa na hii ndoa sasa IPO mashakani.Hivi nachokifanya huyu mkwe ni sawa au yupo nje maadili.

Ni hivi huyu mama ana mtoto wa kiume ambae ameoa mwaka 2005 katika miaka ya elfu mbili na kumi mke huyu jamaa alipata mtihani wa maradhi ambayo aliumwa kwa muda wa miaka mwili.KAma unavyojua mwanaume akawa anachepuka pembeni mpaka akamtia mimba mwanamke mwingine na wakazaa mtoto wakiume muda huo alishazaa na mkewe mtoto mmoja na hawakuwa wameachana isipokuwa mke alikuwa anatibiwa maradhi yaliuyokuwa yanamsumbua ya kiswahili.MW mungu akajaalia mke akapona.

Sasa hapa utata uliokuwepo ndugu wa mume wanamsema huyu Dada kwa nini anakataa kulea mtoto wa mumewe na anashutumiwa ana roho mbaya sana.Jamanii hivi kweli ni sawa mwanaume kukuletea mtoto aliyakuwa mpo wote hamjaachana ila yeye kachepuka ni sawa kweli kwa nini huyo mtoto asilelewe na mama yake.yote tisa kumi

Huyu mkwe amejifanya kwenda kumchukua yule mtoto kinguvu ili tu amkomeshe mke wa mwanae amlee yule mtoto.baada ya kuona yule Dada amemkataa mama mkwe kwa vishindo akajifanya kumng'ang'ania yule mtoto amlee yeye eti na unataka yule mke wa mwanae kila wiki akamfulie yule mtoto.

Na anachokifanya anamtumia huyu mwanamke aliyezaa na mwanae kumrusha roho mke wa mtoto wake.basi neno si neno kapigiwa simu huku ukweni kwa sababu kazaa na mwanae.

Wiki kazaa zilizopi eti kapigiwa simu mtoto wake kamaliza chekechea wafanye sherehe alafu mkwe ndio yupo Benet na yule aliyezaa namwanae.DAda wa watu uvumilivu umemshinda ilibidi aulize kwani mama dhamira yako nini kwa hayo unayoyafanya au ndio unaamua kumletea mwanao mke wa pili..mama wacha ajilize katukanwaaa..basi mume wa mtu alivyoambiwa na mama yake mkeo kanitukana karudi kwake kafura na talaka kaandika tayari lakini bado anatembea nayo tu mfukoniii😀😀😀 bado ajamkabidhi anatishia kumuacha.

Hivi wiki sasa inafika nyumba yao aina amani kila MTU anaishi kimpango wake ..kwa sababu ya fitna za huyu mama mkwe..

Sasa najiuliza maswali haya

1 Haoni alipokosea mwanae kwenda kuchepuka mpaka kuleta mtoto akiwa na mke tayari

2 Na kama kosa lishatokea tayari kwa nini amkumbatie hivyo huyo mwamke aliyedhini na mwanae .kama kweli lengo mjukuu wake kwa nini asiendelee kukaa na mjukuu wake bila kuleta mbwembwe zote hizo

Tena huyu mama mkwe wa huyu Dada mume wake miaka ya nyuma alichepuka pia kaja kujua mtoto wa mumewe amekuja akiwa binti wa miaka 25 mkubwa mzima na chozi lilimtoka kwa nini mumewe alichepuka iweje unaona kitu nahisi kwa mwenzie kama yeye MTU mzima nauvumilivu ulimshinda.

OK nisiwachoshe hivi kwa upande wenu mnamchukuliaje mama mkwe wa aina hiii.
Ni jambo la kawaida kwa ndoa za ki Islam &kiswahili.....ndo mfumo wa maisha yao ya siku zote!usipotez3 muda kuomba ushauri
 
Nawachukia sana wanawake wanaozaa halafu anamsusa mtoto akiwa bado mdogo...
Inavyoonekana mama mtu kamtafutia mwanaye kipoozeo...
Kwani uyo binti kaua kwao?

_@Satan_
 
Ni jambo la kawaida kwa ndoa za ki Islam &kiswahili.....ndo mfumo wa maisha yao ya siku zote!usipotez3 muda kuomba ushauri
Tabia haina dini!
Hakuna cha ndoa ya kizungu/ wala kikristo!
Hizi ni tabia tuu!
Ni rafiki hapa mkarismatic lakininalishikuru nkwe alipokufa jinsi alivyokuwa anampelekesha kwa kuwa sio kabila lao ila wote ni waroman!

Wanaume hupenda sana mama zao ,hiyo wakati mwingine huwapumbaza akili au kuwa katka dailema!
Mama au mke? Atakapoegemea hata jali ukweli au uongo!
 
Kwanza pole kwa mhusika wa hiki kisa

Ujue maisha yana mengi na katika mengi lazima uvumilivu uwepo

Swala la kulea mtoto wa mwingne inabidi akubali maana wakati mwingine ili kuweka mazingira ya kipato sehemu moja akikataa inaweza ikawa mwanaume anatoa garama za malezi ambazo zilipaswa ziliwekwe sehemu moja
Ukiletewa mtt wa mkeo utalea?..
 
Mimi mwanaume anifanyie hivi nijue ....sitaondoka bila akae akijua na yeye atalea watoto wa mwanaume mwenzie japo wawili katikaa uzazi wangu kama nimezaa sita akae akijia wanne watakuwa wake wa halali wawili imekula kwake.......mjue wanaume msitufanye kama sisi wanawake tumetolewa nyongooo mnavyoumia nyie na sisi hivyo hivyo
Kwa kweli mtu akizidisha ufirauni hamna namnaa...namtaftia kiben10...stress reliever..isiwe keroo
 
Kuuma inauma ila unapaswa kujua kuwa maisha ya ndoa ni mziki wa mchiriku kuwa ukiuchoka uta sikiliza RNB
Eehh mnakomoleka sanaa tu, mtu akikuamulia huchomoki.. Alikuwepo Samson na bi Delilah ohoo Unadhani wanawake wajinga..hahha
 
Huyo dada nae kakosea.

Si.alishaweka msimamo huyo mtoto asiende kwake???

Angesimamia hapo.

Huyo mama mkwe amchukue (sawa si damu yao) ambebe mgongoni...ampigie simu au au ampe chumba huyo mwanamke wa nje..... mpotezee mazima mazima mazima

Tena akate mawasiliano huko ukweni....atie pamba masikioni wafurukute weee wakimaliza wapambane na hali zao
 
Nina jua ninacho kufanya na nafanya ninacho kielewa
Unamnywesha sumu mtoto au? Ujue mnachokosea ni kutaka kushindana na mwanaume.......we hujiulizi swali dogo tu kuwa kwa nini huyo mwanaume ananitoa kwetu aninipeleka kwao au kwingine kuanza maisha tofauti kabisa
 
Wa mama huwa hawasikilizi kesi za watoto wa wakiume eti wamechepuka au wanatembea na mabinti za watu, kwanza ndio wanafurahia kuwa wanavidume.

Ukijua hilo huwezi mshangaa sana huyo mama mkwe, pia si inasemwa kuwa 'mtoto wa mume ni wa mke na wa mke ni wa mume??'
 
Nimependa hii falsafa "ADUI WA MWANAMKE NI MWANAMKE'' niambie kama niufunuo wako au umeuchepua mahali.
Sio ufunuo wangu bali ni msemo ambao upo siku nyingi, zamani nilikuwa naupinga sana ila sasa naona kabisa. Wanawake tuna matatizo sana.
 
Back
Top Bottom