Kisa cha kweli: Mama wakwe wengine pasua kichwa

Kisa cha kweli: Mama wakwe wengine pasua kichwa

Kuna kitu kinaitwa Karma... Huyo mwanaume na mama yake siku moja karma itawatafuna...

Huyu mdada anaefanyiwa haya kwanini asiondoke kwao?
Aondoke? Nyie wanawake mbona huwa mna roho mbaya hivyo mnashindwa kulea watoto wa wanawake wenzenu? Ndio maana huwa mnasemwa hampendani.........wanaume sisi tunalea watoto wa wanaume wenzetu hata kama ulichepuka ntasema tu kitanda hakizai haramu!!
 
Ni kisa cha ukweli kabisa na hii ndoa sasa IPO mashakani.Hivi nachokifanya huyu mkwe ni sawa au yupo nje maadili.

Ni hivi huyu mama ana mtoto wa kiume ambae ameoa mwaka 2005 katika miaka ya elfu mbili na kumi mke huyu jamaa alipata mtihani wa maradhi ambayo aliumwa kwa muda wa miaka mwili.KAma unavyojua mwanaume akawa anachepuka pembeni mpaka akamtia mimba mwanamke mwingine na wakazaa mtoto wakiume muda huo alishazaa na mkewe mtoto mmoja na hawakuwa wameachana isipokuwa mke alikuwa anatibiwa maradhi yaliuyokuwa yanamsumbua ya kiswahili.MW mungu akajaalia mke akapona.

Sasa hapa utata uliokuwepo ndugu wa mume wanamsema huyu Dada kwa nini anakataa kulea mtoto wa mumewe na anashutumiwa ana roho mbaya sana.Jamanii hivi kweli ni sawa mwanaume kukuletea mtoto aliyakuwa mpo wote hamjaachana ila yeye kachepuka ni sawa kweli kwa nini huyo mtoto asilelewe na mama yake.yote tisa kumi

Huyu mkwe amejifanya kwenda kumchukua yule mtoto kinguvu ili tu amkomeshe mke wa mwanae amlee yule mtoto.baada ya kuona yule Dada amemkataa mama mkwe kwa vishindo akajifanya kumng'ang'ania yule mtoto amlee yeye eti na unataka yule mke wa mwanae kila wiki akamfulie yule mtoto.

Na anachokifanya anamtumia huyu mwanamke aliyezaa na mwanae kumrusha roho mke wa mtoto wake.basi neno si neno kapigiwa simu huku ukweni kwa sababu kazaa na mwanae.

Wiki kazaa zilizopi eti kapigiwa simu mtoto wake kamaliza chekechea wafanye sherehe alafu mkwe ndio yupo Benet na yule aliyezaa namwanae.DAda wa watu uvumilivu umemshinda ilibidi aulize kwani mama dhamira yako nini kwa hayo unayoyafanya au ndio unaamua kumletea mwanao mke wa pili..mama wacha ajilize katukanwaaa..basi mume wa mtu alivyoambiwa na mama yake mkeo kanitukana karudi kwake kafura na talaka kaandika tayari lakini bado anatembea nayo tu mfukoniii😀😀😀 bado ajamkabidhi anatishia kumuacha.

Hivi wiki sasa inafika nyumba yao aina amani kila MTU anaishi kimpango wake ..kwa sababu ya fitna za huyu mama mkwe..

Sasa najiuliza maswali haya

1 Haoni alipokosea mwanae kwenda kuchepuka mpaka kuleta mtoto akiwa na mke tayari

2 Na kama kosa lishatokea tayari kwa nini amkumbatie hivyo huyo mwamke aliyedhini na mwanae .kama kweli lengo mjukuu wake kwa nini asiendelee kukaa na mjukuu wake bila kuleta mbwembwe zote hizo

Tena huyu mama mkwe wa huyu Dada mume wake miaka ya nyuma alichepuka pia kaja kujua mtoto wa mumewe amekuja akiwa binti wa miaka 25 mkubwa mzima na chozi lilimtoka kwa nini mumewe alichepuka iweje unaona kitu nahisi kwa mwenzie kama yeye MTU mzima nauvumilivu ulimshinda.

OK nisiwachoshe hivi kwa upande wenu mnamchukuliaje mama mkwe wa aina hiii.
Hukusikiliza Zari alichokisema?
 
bdba0ca0a34c98c60d9d4f4f7472682e.jpg
 
Roho mbaya tu ndio maana walikupachika magonjwa ya kiswahili...ushindwe kulea mtoto kisa ujazaa wewe si ushetwani huoo??
 
Aondoke? Nyie wanawake mbona huwa mna roho mbaya hivyo mnashindwa kulea watoto wa wanawake wenzenu? Ndio maana huwa mnasemwa hampendani.........wanaume sisi tunalea watoto wa wanaume wenzetu hata kama ulichepuka ntasema tu kitanda hakizai haramu!!
Waite wanaume wenzakoo hapa waje wathibitishe kama wana uwezo wa kukubali mkewe achepuke amletee mtoto sio wake akubali alafu anajua si wake labda uniambie amemkuta nae hapo sawa
 
weeee usifanye utani na kuletewa mtoto ukiwa upo kwenye ndoa bola Mara mia umkute nae...Mimi siwezi binafsi na sina moyo huo nikimkuta sawa ....yahni Mimi Nike kuhudumia mtoto kumfulia kumfanyia kila kitu alafu wamenifanyia usaliti.....Tena Mara mia aje akiwa na akili zake timamu anaweza kufanya kila kitu
Huyo jamaa kaandika talaka kimzaha hiyo tayari imethibiti talaka kwa mafundisho ya kiislaam haina mzaha
 
Demi uko sahihi kwani waangalie tu wamama walivyo wa ajabu kwamba; WANAPENDA KUWACHOKOZA WAKE WA WANAO LAKINI HATAKI KUSIKIA BINTIYE ALIYEOLEWA KAKEMEWA. Ni watata sana hawa.
Wa baba waaala
 
Shetani bado anamtumia Mwanamke kuvuruga Amani Duniani....
Huyo mama kuna evil spirit ndani yake pasipo yeye kujijua na ameruhusu kutumika ili kuvuruga Amani kwenye Ndoa ya Mwanae...
 
[QUOT
Huyo jamaa kaandika talaka kimzaha hiyo tayari imethibiti talaka kwa mafundisho ya kiislaam haina mzaha
alafu kumpa ampi anajizungusha nayo....lakini kisheria mpaka amlabidhi kwa sababu hajamtakia kwa mdomo bado si talaka haijakamilika
 
Back
Top Bottom