Kisa cha kibibi kilichopinda mdomo

Status
Not open for further replies.

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
21,799
39,610
Naam katika siku nyingine tena, naitafakari siasa katika sura yake halisi hasa siasa za chama tawala kwa yale ambayo yanaendelea huko na tafakuri yangu hiyo imenifanya nikumbuke kisa cha zamani ambacho niliwahi kukisoma katika moja ya vitabu mashuhuri vya hadithi pindi nikiwa shule ya msingi. Kisa cha Kibibi kilichopinda mdomo; kisa chenyewe ni hiki kifuatacho.

Na mimi, ewe Seyyid yangu, kilianza kile kibibi cha pili, nilikuwa mpinzani pia. Na, kwa wafuasi wangu, nilikuwa mkali kupita kiasi. Sikuwaruhusu hata kidogo kucheza bali nilisisitiza wakati wote wajishughulishe na siasa zetu tu hata kama wakati umekwisha.
Siku moja, kiongozi mpinzani mmoja mwerevu kuliko wenzake, kwa tamaa zake, alikata shauri kunitumia. Aliwashauri wenzake kuwa, kila wakija ofisini, waniulize, “Katibu, mbona unaonekana umepauka hivyo, unaumwa?” Kwa kuwa mimi mwenyewe sikuhisi maumivu yoyote, nilistaajabu kusikia yale waliyoniambia wafuasi wake, lakini sikuyafatiliza.


Siku ya pili, na siku zilizofuata mpaka siku ya tano, kila walipoingia ofisini mamluki wale waliendelea kuniuliza swali hilo hilo; ndipo nilipoanza kufikiria labda kweli nimepatikana na jambo fulani lililonipausha, nikakaa shauri kuliepuka kwa kulichukulia hatua. Siku ya sita nilibaki nyumbani. Mamluki wale walipoarifiwa, walikusanya sarafu mia moja, wakaja, wakaniomba nizipokee kama dalili yao ya kunitakia afya njema. Nilifurahishwa sana na kile kitendo chao, nami nikawakubalia malengo yao
Upokeaji wangu wa zile fedha ulinisababisha niendelee kujifanya mgonjwa kwa muda wa siku kadhaa, na mamluki wale nao waliendelea kila siku kuliletea fedha, nami nikiwaahidi nitawaunga mkono. Siku ya kumi, yule kiongozi mwasi aliyefanya mpango ule, alikuja chumbani nilimojilaza huku amechukua zile fedha.


Wakati huo, mbele yangu palikuwa na yai moto lililochemshwa ambalo, wakati nilipomwona yule kiongozi mamluki akiingia,. Nililibugia mdomoni, nikifikiri, akijua ninaweza kula, bila shaka atatambua kuwa sina ugonjwa wowote na hawataniletea tena fedha! Yule mamluki, walakini, alitambua ujanja wangu, akanijia huku akijifanya anasikitikia, akasema kwa mshangao, “Lo, kibibi katibu mbona mashavu yamekuvimba hivyo!”. Wakati akisema hivyo aliyabana kwa nguvu mashavu yangu kwa mikono yake miwili, wakati lile yai moto likiwa mdomoni mwangu! Akijifanya ananipangusa jasho, Yule mamluki aliyabana tena kwa nguvu mashavu yangu mpaka lile yai moto lililokuwa mdonomi mwangu lilipasukia kinywaji mwangu, na ile njano yake moto ikanitiririkia koono mwangu, ikatoka mdomoni mpaka kidevuni ikaniunguza vibaya! Yule mamluki alipoona vile alipiga kelele ya furaha akisema “Mwenyezi Mungu Asifiwe, ewe kibibi katibu! Ule ugonjwa umepondeka na sasa utapata nafuu! Sisi mamluki tunamshukuru Mola kwa kupona kwako!”


Wakati huo mdomo wangu ulikwisha pinda kwa kuungua, ukawa kama hivi unavyoniona, nikawa kichekesho kwa adui zangu mpaka ikanibidi NIFUKUZWE ofisini kwaku. Na hicho, Seyyid yangu, ndicho kisa changu, kilichonifanya nipinde mdomo!”
Kwa kila ambaye ni mmoja wa great thinker atakuwa amepata picha ni kitu gani nakifananisha na kisa hiki kitamu, ambacho mwisho wake ni kwamba KIBIBI kimepata msongo wa mawazo wa kudumu kwa fikra zake fupi za kudhani kuwa wapinzania wote ni majuha na hakuna mwerevu mpaka pale walipomtimuwa.
 
Kibibi kinatumika tu sasa huko magambani sijui nacho kimeshaluwa mzigo...watakireject sasa hv
 
Watu hajaelewa hiki kisa coz vijana wengi hawana akili pana ya kujaji mambo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom