Kisa cha Generali Yoabu kumuua Generali Abneri bila ruhusa ya Mfalme Daudi ni kielelezo kuwa kuna Matukio hutokea Rais hahusishwi au hajulishwi

Kisa cha Generali Yoabu kumuua Generali Abneri bila ruhusa ya Mfalme Daudi ni kielelezo kuwa kuna Matukio hutokea Rais hahusishwi au hajulishwi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,047
Reaction score
79,390
Kwema Wakuu!

Tulikuwa na Magufuli, akafanya aliyoyafanya. Yapo mazuri akapongezwa kwa mazuri. Na yapo mabaya akalaumiwa na kukemewa, kuliliwa na kutukanwa kwa Mabaya.

Moja ya Mabaya yaliyotokea kipindi cha Magufuli ni pamoja na utekaji, kujeruhiwa na mauaji. Huku matukio hayo mengi yakiwa hayapatiwa haki. Kitendo cha serikali kutokufanya wajibu wake ikiwemo Kulinda raia, na kama raia amedhuriwa basi serikali inaowajibu wa kufanya uchunguzi na haki ipatikane lakini haikufanya hivyo ndio maana inahusishwa Moja kwa moja na matukio hayo.

Swali linakuja, je ni kweli magufuli alikuwa mtekaji au Muuaji?
Swali hili itategemea unalijibu katika msingi UPI.
Je unajibu kifalsafa, au kisheria, au kisiasa au unajibu kwa namna ipi.

Kama Magufuli alikuwa Muuaji na mtekaji, je mara baada ya kufariki je matukio hayo yalikoma na kuisha kabisa au bado yanaendelea?

Kama yanaendelea hiyo itamuondoa Magufuli kwenye shutuma za utekaji na uuaji?
Swali hili linamajibu mawili. Hivyo jibu lake linakuwa inategemea.

Sasa Kaingia Rais Samia akirithi kiti cha Mtangulizi wake.
Lakini matukio ya utekaji na mauaji hayakukoma, yanaendelea.
Wengine husema Kama walivyosema kwa Magufuli yakuwa Mama ni mtekaji na muuaji kwa sababu zilezile walizotumia kwa mtangulizi wake.

Swali linakuja, Je ni kweli Rais Samia ni mtekaji au muuaji?
Kama sio, Nani anayeteka na kuua watu?

Kwa nini Rais Samia ahusishwe katika matukio hayo yenye sifa Mbaya.
Jibu lipo wazi, ni kwa sababu yeye ndiye amiri jeshi Mkuu, ambaye anaweza kutoa tamko Moja na vyombo vote vya Dola vikatii. Katiba ya nchi imempa mamlaka hayo MTU mwenye cheo cha Urais katika nchi yetu

Swali linakuja, je Katiba inamaana gani kwa Watawala na vyombo vya Dola?
Je wanaiheshimu na kuifuata.
Kikawaida heshima haipimwi kwenda juu yaani Mdogo Kumheshimu Mkubwa bali heshima inapimwa na kupewa thamani pale Mkubwa anapoheshimu wadogo zake.

Je kwa mazingira ya nchi yetu viongozi wanaifuata katiba kuheshimu waliowadogo?
Kama wadogo hawapewi heshima hii itamaanisha hata wakubwa hawaheshimiwi. Kwa sababu heshima huanzia kwa wakubwa kwenda kwa wadogo.

Hii inamaanisha nini?
Kwenye Dola Sheria zipo za aina mbili. Sheria za Heshima ambazo ndizo huongoza nchi na watu na kufanya utawala uwe stable.
Na zipo Sheria za Kishenzi, hizi hutumika zaidi kwa washenzi na watu wenye makosa Makubwa hasa ya uasi, uhaini na ugaidi.
Sheria zote zinatumika kwenye kuendesha taifa.

Lakini inatokea mkanganyiko na mchanganyo ambapo serikali huchanganya iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Sehemu ya kutumia sheria za heshima hutumika Sheria za kishenzi. Na sehemu ya kutumia sheria za kishenzi hutumika Sheria za heshima Jambo ambalo huzua mtafaruku sio tuu kwa watu wa kawaida bali hata vyombo vya Dola.

Kuua MTU au kuteka MTU zipo kwenye sheria za kishenzi ambapo mtu mpaka ahukumiwe kwa Sheria za kishenzi lazima afanye moja ya makosa yafuatayo;
1. Uhaini.
2. Kuiba siri nyeti za serikali na kuuza kwa maadui.
3. Ugaidi
4. Kufanya na kuchochea uasi jeshini zingatia sio uraiani.
5. Kuhatarisha usalama kwa kiwango cha taifa. Na hii isitumike kisiasa.
6. Kukatisha uchunguzi wenye tija kwa taifa kimakusudi kwa MTU kumuua shahidi ili ku-cover siri isifichuke ambayo uchunguzi unafanyika kuipata siri hiyo.

Tukiachana na huko, tukirudi kwenye mada.
Tunajua kuwa Rais au Mfalme hawezi kuongoza na kutawala bila Vyombo vya Dola.

Swali linakuja, je kuna wakati vyombo vya Dola huweza kujiamulia kufanya baadhi ya mambo bila Kumjulisha na kumhusisha Rais au Mfalme? Hiyo ndio mada yetu Bila Shaka na hapo ndipo kisa cha Generali Yoabu na Generali Abineri kinapokuwa sehemu ya andiko hili.

Abineri alikuwa ni Mkuu wa Majeshi katika Utawala wa Mfalme Sauli katika Yuda.
Yoabu alikuwa Mkuu wa Majeshi kwa Mfalme Daudi kabla na baada ya kutawazwa kuwa Mfalme.

Baada ya Mfalme Sauli Kufariki, Abineri anaendeleza kiapo chake cha utii kisha anasimamia zoezi la kutawazwa ishbosheshi mtoto wa Sauli ili awe Mfalme. Zoezi linakamilika.
Lakini Abneri na Mfalme mpya ndiye Ishbosheshi wanapishana kisa Abineri kulala na Rispa aliyekuwa Suria (mchepuko) wa Mfalme Sauli, babaye Ishbosheshi.

Abineri anaamua kwenda kwa Daudi Kufanya makubaliano kuwa Abneri atamsaidia Daudi kuichukua nchi ya Yuda yote kuanzia Benyamin mpaka Hebroni. Ilimradi Daudi ampe uhakikisho wa usalama wake na maslahi mengine ya kiuchumi na kisiasa. Wakakubaliana.

Abineri akatoka.
Huku nyuma Yoabu hakuwepo, anakuja anapewa taarifa na baadhi ya usalama waliopo ikulu ya Daudi. Kuwa Mkuu wa majeshi wa Sauli, Abineri alikuwepo hapa.
Akaambiwa kila kitu.

Yoabu kwa hasira akaenda kwa Daudi akamuuliza kulikoni Abneri aje pale. Basi akamlaumu Sana Daudi. Kumbuka Daudi ni mfalme lakini bado hajachukua nchi yote. Kajichimbia Huko Hebron na ameahidiwa na Abneri kuwa ataichukua mpaka Yuda.

Yoabu akatoka akiwa na majeshi yake akimfutia nyuma Abneri. Walimpomfikia. Yoabu akamuua Abneri kwa kumvizia wakati wanazungumza.

Sababu kubwa za Yoabu Kumuua Abineri ni kulipa kisasi cha Mdogo wake ambaye Abineri alimuua kwenye vita zilizopita siku za nyuma. Vita vya waisrael wenyewe kwa wenyewe. Ambapo Majeshi ya sauli yakiongozwa na Abineri yakipigana na majeshi ya Daudi yakiongozwa na Yoabu. Wote hao ni waisrael.

Sababu pili ni kuhofia nafasi yake isijekuchukuliwa na Abineri. Ili kukata mzizi kabla haujakomaa ndio Yoabu anaamua kumalizana na Abineri kabisakabisa

Daudi anapata taarifa roho inamtoka.
Inamtoka kwa sababu Mfalme Daudi alifanya mapatano na Abineri na moja ya makubaliano yao yalikuwa Kumlinda Abineri.

Fikiria Wakati Ule Mbowe katoka kufanya maridhiano na Samia alafu wakati Mbowe anaondoka kurudi nyumbani kabla hajafika anakula Chuma. Unafikiri Samia angekuwa kwenye hali ipi?

Yoabu kajichukulia sheria mkononi, bila kumhusisha Mfalme Daudi, kafanya aliyofanya Daudi anakuja kupewa taarifa tuu.

Ukisoma vizuri kisa hicho kinaeleza Daudi alikuwa akimhofia Sana Yoabu.
Lakini alimuweka Kiporo kwamba alikuwa na kinyongo naye. Ndio maana Siku Daudi amezeeka anamuachia nchi Suleiman mwanaye, moja ya KAZI aliyompa ni Kumuua Yoabu. Hakutaka Yoabu afe Kifo cha asili.

Kisa hicho kinawahusu vyombo vya Usalama na shughuli zao.
Kinaonyesha kuwa kuna matukio mengine hayawi kwa amri ya Raia au mfalme Bali hutokea kwa maslahi ya viongozi wa vyombo vya dola. Huku matukio mengine yakiwa yanatokea kama ajali kazini.

Lakini mengi yakiwa ni kwa amri ya mtawala.

Acha nipumzike sasa. Muwe na amani.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Laana ilianza toka watu wa Israel walipotaka kuwa na mfalme. Waliambiwa Sifa za mfalme zitakuwaje na wakatii. Leo sishangai wanachokifanya watawala wetu maana kiliandikwa. Na maandiko hutumia kwa njia Moja au nyingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom