Kisa cha Eric (RIP) wa Mombasa Kisauni, nyuki na supu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,547
729,367
Pata picha hii uko kwa mama ntilie sufuria la supu ya nyama (ya ng'ombe?) inachemka! Mara linakuja kundi la nyuki, haliendi popote halimdhuru yoyote lakini linaenda moja kwa moja kwenye sufuria la supu inayochemka..! Nyuki? Na moto? Mbaya zaidi wanaanza kufyonza chumvi!Nyuki na chumvi? ?Hapana..! Nyuki yake ni sukari sio chumvi.

Eric akaisoma ile hali akamwambia mama yule mama mama akaenda kununua udi na kuvukiza wale nyuki.Eric akasema hawa sio nyuki wa kawaida ngoja nikawaletee ndimu, akachukua bodaboda na kupata ndimu za ulanguzi.

Iko hivi nyuki wa kawaida hapendi vitu vichachu hasa ndimu, lakini zile ndimu za Eric wale nyuki walizigombea, kuhoji kwa Eric ndio kumepelekea mauti yake yule mama na mzee mmoja waliahidi kumkomesha na ndani ya saa 24, Eric aliaza kuugua huku tumbo likiwa limedinda akapelekwa kwenye maombi lakini ikashindikana.

Eric ni marehemu nyuki hawapo tena nyuki wa supu nyuki wa chumvi nini kipo nyuma ya hili saga? Uchawi ushirikina au nini? Nyuki na moto ni tofauti nyuki na chumvi haviendani nyuki na ndimu ni bila bila hawa walikuwa marafiki.
 
nadhani hiyo haikuwa nyama harisi itakuwa kiini macho tu. japo fungu ni gumu kulielewa
 
Nyuki walikuwa wana fanya utafiti hao hawana lolote wala msi wahusishe na uchawi.
 
hao nyuki waeza kua wananchi waliokata tamaa ya maisha .so wanaamua kuvamia chakula cha walio nacho ( mama ntilie) na huyo Mzee,etc,Yale majiziiiiiii,sababu wananjaa wanabugia hata ambavyo sio stahili kwao( watziii) wamekata tamaa.huyo mama ntilie anajaribu kutumia mbinu kuwatimua nyuki,Dodoma& ccm and jk vs jpm saga!!, mauti yanamkuta erick alipojaribu kuhoji.erick ni Nani?( ).nmejaribu kudadavua kwa akili yangu fumbo hili.fasihi tamu sana.
 
Mkuu Mshana Jr unajua maisha yamekuwa magumu sana, hv tunavyoongea kilo ya sukari ni shilingi 3000 mp 4, sahani ya chips pale kwa Edo Namanga nayo imepanda bei.......tena na ww unataka tuumize vichwa kutafakari na kufumbua hii kitu......pls brother, fanya ufafanuzi.
 
Kisiasa zaidi...
 
Noted sifongo
 
Eti leo nimeskia eti mombasa watoto wadogo wa kiume hawatumwi dukani kabisa ila wanaotumwa ni watoto wa kike wadogo hata usiku wanaoenda dukani ni watoto wa kike tu.kunani mombasa watoto wa kiume wafungiwe ndani hvyo hawatakiwi ht kutoka nje.ajabu huku kwetu bongo mtoto wa kike ndo analindwa balaa
 
Back
Top Bottom