Hivi huu ulikuwa ushirikina au mazingaombwe?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Tukio hili lilitokea Mombasa Kenya miaka 7 iliyopita...
Asubuhi moja mama mmoja muuza supu mtaani akiwa kainjika sufuria lake la supu ya nyama upenuni ikiendelea kuchemka, mara ghafla lilitokea kundi la nyuki na kuzingira sufuria la supu na kuanza kufyonza supu ya moto
Hili halikuwa tukio la kawaida kwakuwa kwanza nyuki hawapatani na moshi na moto..lakini vilevile vile vyuki hawapatani na chumvi..ni nyuki wa kishirikina pekee ndio wanaweza kutumia hivyo vitu

Kijana mmoja barobaro maarufu sana pale kitaa akajitoa woga na kutafuta ndimu...ili atest uhalisia wa wale nyuki...kama wangeikimbia ndimu basi hakuna shida lakini kama wangekula ndimu basi hapo kulikuwa na shida kwakuwa nyuki na ugwadu ni vitu viwili tofauti kabisa

Kwa mshangao wa wengi nyuki waliokuwa wamezingira sufuria la supu inayochemka na kufyonza kwa raha zao ...ghafla walihamia kwenye vipande vya ndimu iliyoletwa na bwana Erik yule kijana barobaro... Mama muuza supu alikasirika sana japo alikana kuwajua nyuki hao na asili yake

Taharuki ilianza pale baada ya masaa machache bwana Erik kuanza kuugua ugonjwa wa ajabu huku kende na uume vikiwa vimevimba hasa...
Majirani walijaribu tiba ya kila aina ikiwemo maombi nk lakini Erik alifariki kabla ya kutimiza masaa 24

Walokole wanakosea sana. Haiwezekani gafla bin vuu mtu ambaye amwamini au hakuwahi kumwamini Yesu na yamkini aliutukana wokovu damu ya Yesu kufanya kazi kwa mtu huyo. Huko ni kujipendekeza na kutaka utukufu kwa wanadamu ili waonekane maji yao ya upako yana nguvu. Liwe funzo kwa wote.

Jina la Yesu ni ngome kwao wamwinio Yesu na kutii injili yake ila ni kinyume chake kwao wapingao.
 
daah, dunia ina mengi mkuu. nakumbuka nikiwa mdogo amewahi kuja mgeni nyumbani akawa hali chakula anakwenda kuwinda panya na kuwala wakiwa wabichi. Nilivyogundua niligoma kulala nae chumbani kwangu cha ajabu nilikuwa nikilala nashtuka yupo kanasa ukutan kama nge mulemule chumbani.
 
Mmh wapi huko? Ilikuwa mwaka gani hii?
 
daah, dunia ina mengi mkuu. nakumbuka nikiwa mdogo amewahi kuja mgeni nyumbani akawa hali chakula anakwenda kuwinda panya na kuwala wakiwa wabichi. Nilivyogundua niligoma kulala nae chumbani kwangu cha ajabu nilikuwa nikilala nashtuka yupo kanasa ukutan kama nge mulemule chumbani.
Try n error...sometimes kuna miujiza hutokea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom