Kiruhuo Mawoko..

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Wandugu,
kuna hii kitu kwa wachaga inaitwa "Kiruhuo Mawoko" yaani "kifungua mikono"
Kwa wasio wachagga: ni ile fedha/mali yako ya kwanza pindi uanzapo kazi/biashara unayowapatia wazazi ili kufungua mikono yako kupokea bara nyingi zaidi kwenye kazi uifanyayo.
Na kimila ni mshahara wote wa kwanza au kama ni mkulima tunaeza sema mavuno yote ya kwanza.

My questions are;
1. Is it still viable to date? -katika hali ya sasa ya kimaisha na kiuchumi.

2. Kama ulitoa mara ya kwanza ulipoanza kazi, je unapobadili kazi do u still give the first produce?

3. Of what benefit is it really?
 
Unapoanza kazi/biashara kiaafrika unashauriwa kipato chako cha kwanza uwanunulie chochote wazazi wako na wote waliokusaidia kukufikisha hapo.
Mentor usilalamike wazazi wako wali sacrifice sana kukufikisha hapo.
 
Sielewi makabila mengine, lakini mkuu Bishanga naungana na wewe kuwa utaratibu huu ni mzuri kwa ajili ya kupata baraka za wazazi au ndugu waliowezesha kufika hapo ulipo. Itakuwa si jambo jema kupokea mshahara wako wa kwanza au pesa yako ya kwanza ktk biashara yako then pesa hiyo ukaenda kugonga Valuer, Jack Daniel's au kutafuta changudoa.
 
Kwani wazazi wako walipotumia pesa zao kukusomesha wao wali-benefit vipi?! Usiwe mbinafsi kupitiliza.
 
zaidii ya mamaa angu..hakunaa nduguu aliee nisaidiaaa,so nisipooo kujaliii nduguu usiniamind hukunisaidiaa kipindi na somaa kwa shidaaaa
 
Unapoanza kazi/biashara kiaafrika unashauriwa kipato chako cha kwanza uwanunulie chochote wazazi wako na wote waliokusaidia kukufikisha hapo.
Mentor usilalamike wazazi wako wali sacrifice sana kukufikisha hapo.

Nashukuru Bishanga, ila swali ni je, unawapa yote kama mila invyoelekeza au ndo kama ulivyosema unaweza ukanunua sukari kilo tano ukawapeleka wazazi??!

Sielewi makabila mengine, lakini mkuu Bishanga naungana na wewe kuwa utaratibu huu ni mzuri kwa ajili ya kupata baraka za wazazi au ndugu waliowezesha kufika hapo ulipo. Itakuwa si jambo jema kupokea mshahara wako wa kwanza au pesa yako ya kwanza ktk biashara yako then pesa hiyo ukaenda kugonga Valuer, Jack Daniel's au kutafuta changudoa.
Patience....thanks! ivi unaweza ukaugawa vipande vipande pia kwa ndugu wengine? nilifundishwa unatakiwa kutoa yote..
 
Last edited by a moderator:
Unapoanza kazi/biashara kiaafrika unashauriwa kipato chako cha kwanza uwanunulie chochote wazazi wako na wote waliokusaidia kukufikisha hapo.
Mentor usilalamike wazazi wako wali sacrifice sana kukufikisha hapo.

Nashukuru Bishanga, ila swali ni je, unawapa yote kama mila invyoelekeza au ndo kama ulivyosema unaweza ukanunua sukari kilo tano ukawapeleka wazazi??!

Sielewi makabila mengine, lakini mkuu Bishanga naungana na wewe kuwa utaratibu huu ni mzuri kwa ajili ya kupata baraka za wazazi au ndugu waliowezesha kufika hapo ulipo. Itakuwa si jambo jema kupokea mshahara wako wa kwanza au pesa yako ya kwanza ktk biashara yako then pesa hiyo ukaenda kugonga Valuer, Jack Daniel's au kutafuta changudoa.
Patience....thanks! ivi unaweza ukaugawa vipande vipande pia kwa ndugu wengine? nilifundishwa unatakiwa kutoa yote..
 
Last edited by a moderator:
Kwani wazazi wako walipotumia pesa zao kukusomesha wao wali-benefit vipi?! Usiwe mbinafsi kupitiliza.

da Lizzy siwi mbinafsi ndio maana nkauliza ili nipate majibu sahihi...kwani nikiwapa kamshahara ka mwezi wa kwanza ndo kitalipa all what they have done to me?
 
Last edited by a moderator:
Dogo mmoja nilikaa naye akamaliza chuo salary ya kwanza kilo mbili alimpa bibi yake na faza wake anafanikiwa ile mbaya hata majuzi kanipa kilo nne baada ya kukwama mahali. kwakweli .kiruuo mawoko. inalipa.
 
Nashukuru Bishanga, ila swali ni je, unawapa yote kama mila invyoelekeza au ndo kama ulivyosema unaweza ukanunua sukari kilo tano ukawapeleka wazazi??!

Patience....thanks! ivi unaweza ukaugawa vipande vipande pia kwa ndugu wengine? nilifundishwa unatakiwa kutoa yote..
nchini Finland faini ya traffic offence ni asilimia ya kipato chako na sio flat rate kama elfu ishirini za bongo.Nia na lengo la faini hiyo ni kumfanya anayelipa ajisikie kalipa.Sasa mkuu uanze kazi exim bank mshahara dola elfu mbili ndo wazazi wako uwape kilo ya sukari from your first salary? hapana,si sawa.
 
da Lizzy siwi mbinafsi ndio maana nkauliza ili nipate majibu sahihi...kwani nikiwapa kamshahara ka mwezi wa kwanza ndo kitalipa all what they have done to me?
gesture Mentor gesture,ni sadaka tu ile na sio malipo,huwezi kulipia kilio chako kilichowalaza wazazi wako macho wakatembea kiliomita tano porini usiku wa manane kukupeleka hospitali umezidiwa homa,haina malipo hiyo.
 
Last edited by a moderator:
hiyo ni kama fungu la kumi unatoa kwa kushukuru msaada wao kwako ,na c kulipa na wakiseme 2úwalipe hakuna atakayeweza coz ni jambo ambalo linalohusisha ubnadam na hakuna anayeweza kukip pay 4 dat servc in comn7 common
 
Dogo mmoja nilikaa naye akamaliza chuo salary ya kwanza kilo mbili alimpa bibi yake na faza wake anafanikiwa ile mbaya hata majuzi kanipa kilo nne baada ya kukwama mahali. kwakweli .kiruuo mawoko. inalipa.
Mamndenyi ......... najua unanisema kwa mafumbo hapa............Nilishasema nitakununulia kaniki mwakani..........
 
Last edited by a moderator:
mi nafikiri huwezi toa yote bhana.
mfano mshahala lak 5 ndo umepokea kwa mara ya kwanza
umeitoa yote kwa mpigo utaishije kwa mwezi unaofuata?
mi najua mshahara wa kwanza unatoa % fulan unawapa wazazi then inayobaki unapanga chumba, godoro kitanda nk.
Then mishara inayofuata waweza kuunganisha 2 ukapata 1 then ukapeleka kwenye familia au ukoo kama shukrani.
Sherehe ya shukran inafana unapokuwa ushazichanga kiaina , "kula pombe mpaka ujinga ukutoke"
 
gesture Mentor gesture,ni sadaka tu ile na sio malipo,huwezi kulipia kilio chako kilichowalaza wazazi wako macho wakatembea kiliomita tano porini usiku wa manane kukupeleka hospitali umezidiwa homa,haina malipo hiyo.

Touching...
Me remember the time niliungua na chakula (nilikalia ndizi zikitokota jikoni), mama ran like crazy, some kilometre or less kutafutia mimi some herbs, usiku wa saa 4, na kijiji ain't got this Ngeleja's stuff by the time.
Will I ever be able to pay back such a sacrifice? No way me gonna pay this, gotta call mama this morning.
 
Last edited by a moderator:
@Mphamavu, ulipokalia sefuria haikuathiri uwezo wako wa ile haja kubwa unayopenda kuiongelea? Lol
Mentor kakangu, hata Biblia inasema kuhusu malimbuko. Utapeleka kilicho kinono kwa Mungu na kwa wazazi. Mzazi sio lazma aliekuzaa tu, ila hata aliekulea kwa sehemu kubwa pia.
 
Afu King'asti mchokozi!
Usiniambie unafanya illusion kwamba mfupi ndo alogundua ngazi?
Nope, kipindi hiko nilikuwa na kalio la haja, si unajua mambo ya mapokopoko manjali maugali makila kitu, madhara ya rojo yaliishia kwenye housing to, thanks God hayakufika kwenye mother body.
 
Last edited by a moderator:
Nawashukuru wote Mphamvu, Lizzy Bishanga King'asti edwin monyo Mtambuzi Ndechumia....thanks a lot. Naomba kusummarise mlichokisema kama nimewaelewa vyema: "Kuruhuo mawoko iwe a percentage of your salary NOT ALL YOUR FIRST SALARY" is that right? Pili ni jambo ambalo linanitatiza sasa hivi: Je, kama mwanzoni nilikuwa nafanya kazi Jubilee Insurance (my first job) na nilitoa actually mshahara wangu wa kwanza wote na sasa nafanya kazi Barricks...je, kuna haja tena ya kiruhuo mawoko, in the sense ya the first product of all your stock??! Halafu, swali la nyongeza, what if nikiitoa percentage ya mshahara wa kwanza na kuwasaidia maskini (the needy)..? badala ya kuwapelekea wazazi ambao kwa kweli haitawasaidia chochote maana ni waajariwa/wafanyabiashara wenye kujiweza sana kiuchumi? si unaweza kusema asante kwa ka kilo tano ka sukari (..hata kama ninafanya kazi Barricks!?? Bishanga!???)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom