Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Knuni za definition zinakataza kurudia neno linalokuwa defined katika sehemu ya definition inayolielezea neno hilo.

Nikukuuliza "akili ni nini?" unatakiwa unielezee akili ni nini kwa maneno mengine.

Ukiniambia "akili ni akili" wakati hilo neno akili ndilo ambalo silijui, nahitaji ufafanuzi nilielewe, utakuwa hujafafanua kitu.

Mbona mnaandika kama ng'ombe msiojua kitu?

Mtu akiniuliza, nimeona umetumia hili neno "schadenfreude", sielewi ni nini manaa yake hapa ulivyolitumia.

Schadenfreude ni nini?

Nikimjibu "schadenfreude ni schedenfreude" wakati yeye anataka ufafanuzi kuhusu hilo neno "schadenfreude" atawezaje kujua zaidi maana ya hilo neno, wakati hilo neno ndilo ambalo kaomba ufafanuzi walo?
Una akili ama huna akili? Swali hili linazeeka bila jibu! Kama jibu langu kwako la AKILI sio AKILI... Weka jibu sahihi hapa...
 
Mkuu kumbe medicine unaijua una maana gani kuuliza swali kama hili?
Akili ni uwezo wa kuelewa jambo,kufikiri na kukumbuka
Ndio ktk medicine kipengele cha hx taking huwa tuna test mental status na si akili kama mtu yupo conscious na utaona anaulizwa kama yupo oriented to time,place na person na pia ataulizwa short and long memory,
Lakn unaposema mtu hana akili una maana gani maana akili yenyewe ipo muda wote kwa maana hiyo huwezi sema mtu hana akili bora useme mtu hana uwelewa au ufikiri au useme mtu ana matatizo ya akili psychotic disoder,epilepsy
At least umejaribu kujibu sasa kuwa akili ni uwezo wa kujua jambo... Nakupongeza sana kwa hili... Ila kwenye maelezo yanayofuatia umechanganya na vitu vingine sio tatizo sana...
Pia umesema kuwa haiwezekani kusema kuwa mtu hana akili kwakuwa ipo muda wote (mengine yaliyofuatia ni maelezo tu yenye mchanganyiko mwingine) lakini bado sio mbaya.... Na nikushukuru sana kwa majibu yako
Sasa tuendelee na mjadala.... Naomba kuuliza swali/ maswali mengine?
Je kipimo cha akili ni kipi?
Je tunaweza kuishika akili na kuiona kwa macho?
Je akili ina rangi uzito na ujazo?
Jibu kwa weledi na maarifa yako bila kuweka ma link ya Wikipedia na wazungu... Kama tumesoma na kuelimika tujaribu kuchambua jambo wenyewe bila utegemezi wa maandiko ya wafu, tukiw na hii tabia tafsiri yake ni moja tu kwamba hatujiamini kwa majibu yetu na tunaamini walichokiandika wao na huu ndio mwanzo wa kumuabudu mtu
 
Kuna watu washanijibu akili ni nini. Nikawajibu nina au sina akili kwa muktadha wao.

Mmoja kasema akili ni kutambua uwepo wa Mungu.

Nikamwambia kwa muktadha huo sina akili. Kwa sababu sitambui uwepo wa Mungu.

Mwingine akaniambia akili ni uwezo wa kupambanua mambo positive na negative. I am paraphrasing.

Nikamwambia kwa muktadha huo akili ninayo kwa sababu nimeweza kudadavua dhana ya kuwepo kwa Mungu kwa "proof by contradiction" iliyoanza kama nakubali Mungu yupo (positive) nikaichambua dhana ya kuwepo Mungu nikaona contradictions ambazo hazijibiki. Nikaishusha na kuikataa (negative)

Sasa hapo utaona watu wawili tofauti wame define akili kwa namna mbili tofauti, na wote nimewapa majibu yao kwa mujibu wa muktadha walioutoa katika definition ya akili.

Sikuogopa kuwajibu.

Majibu yapo wazi kwenye uzi huu huu. Kila mtu anaweza kuyasoma.

Kwa hiyo hii dhana ya kwamba Kiranga anaogopa kujibu, Kiranga hataki kujibu si ya kweli.

Tatizo nitajibu vipi swali ambalo halijafafanuliwa?

Hao wawili wamefafanua akili ni nini na nimewajibu. Kwa mujibu wa ufafanuzi wao.

Sasa kwa nini Mshana hataki kusema akili ni nini nimjibu?
Nakujibu kwa mara ya 15 akili ni akili kama kuna jibu nje ya hapo liweke hapa bila maneno mingi
 
Baadhi hawajakujibu, kuna wengine wamejibu au kuelezea maana ya akili kwa wanavyoelewa wao. Na mimi nikiwa mmoja wao.

Unamaanisha nini unaposema "mnaliogopa" na "...swali gumu sana kwenu..."? unawalenga akina nani hapo?
Mimi nimeshamjibu zaidi ya mara 15 kuwa AKILI ni AKILI...
kitu cha kwanza nimejibu
Kitu cha pili je jibu langu ni sahihi ama sio sahihi?
Kitu cha tatu kama jibu langu sio sahihi... Jibu sahihi ni lipi? Hapa ndio anapopakimbia
 
Mshana na watetezi wake.

Waambie kwamba swali jepesi tu mbona wewe umejibu na tumeendelea na mjadala hujapata kidonda wala kutokwa damu?

Wameusimamisha mjadala kwa swali ambalo halina uzito wowote.

Ndiyo maana nasema hawana hoja.
Mshana na watetezi wake...! [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3].... Hawana hoja! [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kiranga hajawahi kukimbia changamoto wala swali.

Kama hajui jibu atakwambia tu hajui.

Sio kamaMshana, unamwambia ajibu akili ni nini, anajibu akili ni akili, bwahahaha.

Nakujibu hivi.

Naweka maneno nilivyoyaandika Kiingereza, halafu natafsiri Kiswahili chini.

Usije kuomba tafsiri ya lugha ya kabila yenu tu hapa.

Kiingereza

By convergence, the mathematics needed to resolve the nature and beginning of the universe in the singularity at the big bang, according to the best known current theories, can be narrowed down to reconciling Einstein's Relativity, which deals with the science of the very big/heavy and quantum theory, which deals with the very small.

This is because, at the singularity, all the matter of the universe is condensed into an infinitesimally small space -the primordial beginning of our spacetime, necessitating a conundrum of the very dense/ large mass (Einstein's Relativity)in an infinitesimally small space (Quantum Physics).

Without coming up with the mathematics of reconciling Relativity and Quantum Physics, which has not been done todate, the beginning of the universe will remain unknown.

Tafsiri ya Kiswahili

Kwa kujongea kwenye kukutana, hisabati zinazohitajika kutatua asili na mwanzo wa ulimwengu katika ajabu la mwanzo wa ulimwengu lililotokea kwenye Mshindo Mkubwa, kwa mujibu wa nadharia nzuri kabisa zinazojulikana sasa, zinaweza kubanwa zaidi ndani ya maafikiano kati ya nadharia ya Einstein ya Uwiano, ambayo inafanya kazi na sayansi ya vitu vikubwa sana/ vizito sana, na Nadharia ya Kwanta, ambayo inahusika na vitu vidogo sana.

Hii ni kwa sababu, kwenye maajabu ya mwanzo wa ulimwengu, mada yote ya ulimwengu ilibanwa katika eneo dogo isivyomithilika - mwanzo wa sili wa eneomuda wetu, kusababisha kizungumkuti cha mada iliyo ngumu/ kubwa (Uwiano wa Einstein unahusika hapo) iwe kwenye eneo dogo sana (Fizikia ya Kwanta inahusika)

Bila ya kupata hisabati zitakazotatua kitendawaili cha kuunganisha Uwiano wa Einstein na Fizikia ya Kwanta, kitu ambacho bado hakijawezekana kufanyika mpaka leo, mwanzo wa ulimwengu utabaki haujulikani


Sasa kinatofauti gani na maneno niliyokuwa nimetafsiri mimi?

Mbona maneno quran na biblia sa hivi hayako kwenye tafsiri yako?

Kama maneno quran na biblia hayakuwepo lakini wewe kwa kutaka uonekane uko sahihi 'ukayachomekea' ina maana unafanya 'misleading' kwa makusudi kabisa au unakuwa unatoa matango pori ambayo umesoma moja kwa moja kwenye vitabu vya watu.


Nakubaliana na wewe hakuna binadamu anaejua kila kitu HAKUNA HAKUNA.

Kama ambavyo wewe na wanasayansi ambao unawaamini AMBAO WANA UHAKIKA KABISA KWAMBA

" Bila ya kupata hisabati zitakazotatua kitendawaili cha kuunganisha Uwiano wa Einstein na Fizikia ya Kwanta, kitu ambacho bado hakijawezekana kufanyika mpaka leo, mwanzo wa ulimwengu utabaki haujulikani"

NA HIVYO HIVYO BILA KUWA BILA KUPATA HESABU (JAPO MIMI NAAMINI JIBU LINAWEZA KUTOKA KWENYE FIELD NYINGINE MFANO SAIKOLOJIA) AMBAZO ZITAKAZOTATUA KITENDAWILI CHA MUNGU, HADI SASA HIVI UWEPO WA MUNGU HAUJULIKANI KISAYANSI.

SASA KAMA WATU WALISHAITANGULIA SAYANSI KWENYE MAMBO MENGI KWA NINI NISIAMINI KWA MACHALE/SELF REALIZATION/TAHAJUDI KWAMBA MUNGU YUPO.

WEWE ENDELEA KUSUBIRI KWANTA ZA EINSTEIN ZIGUNDULIWE NA ZITAKAZOTHIBITISHA MUNGU YUPO

CC Mshana Jr Kiranga
 
Una hakika?
Kiranga hakika ninini? Kumbuka bila imani hakuna hakika! Sasa kama wewe si mwamini hiyo hakika umeijuaje? Mungu ni mwema sana... Katikati ya maandishi ya mtu unamuona Mungu akijidhihiri ndani yake
 
Msaidie kujibu kwanza swali kongwe! Hivi na maarifa yenu yote mnayojivunia kuwa nayo (kama ni kweli) mpaka leo hii mmeshindwa kabisa kujibu kama mna akili ama hamna? HILI LAWEZA KUWA AJABU KUU NANE LA DUNIA....
Nijibu wewe kama una AKILI ama huna nitakupa ushahidi Adam kuwa binadamu wa kwanza!
Nimeulizwa AKILI ninini nimejibu ni AKILI.. Kama hili sio jibu sahihi naomba nipewe jibu sahihi... Hapa pia hakuna kitu!

Hawataweza kukujibu kamwe.

Kuna tofauti kubwa sana ya mtu anaesoma vitabu vya watu na kuchukua kila kilichomo bila kuchambua na yule ambae anafanya WITHIN JOURNEY FROM UNKNOWING TO THE KNOWING

 
Mimi nimeshamjibu zaidi ya mara 15 kuwa AKILI ni AKILI...
kitu cha kwanza nimejibu
Kitu cha pili je jibu langu ni sahihi ama sio sahihi?
Kitu cha tatu kama jibu langu sio sahihi... Jibu sahihi ni lipi? Hapa ndio anapopakimbia

Mbona yeye Kiranga hatoi hizo maana za akili anazosema zipo?
Azitoe basi kwa afya ya mjadala huu
 
Waungwana,Waheshimiwa saana Mshana jr na Kiranga,pamoja na wajumbe wengine wa barza /baraza,
Nina maswali madogo ya nyongeza,
1) Mna Elimu?
2)Elimu ni nini?
3) Kati ya maswali hayo mawili ,lipi lapaswa kuwa la kwanza kujibiwa?
NB: Tusisahau maswali makuu mawili ya huu mjadala ( Una Akili? Na Akili ni nini?)
 
akili ni ubongo,oxygen not going to the brain,means u r dead,hutambui kama ulisoma ABC lol
 
I Jus don't know why I am falling victim on this.... Very very strange kibao kinanigeukia mimi..
Niliweka mada... Mjadala ukalala lakini mhusika akaibuka na reply yake iliyopelekea mimi kumuuliza kama ana akili ama la! Hakunijibu.. Hakuna na jibu ila akazunguka kwa kuuliza akili ninini nikamjibu akili ni akili... Akasema hili sio jibu nikamuuliza kama hili sio jibu basi aseme jibu la akili ni lipi.. Tangu hapo si yeye wala wafuasi wake wameweza kujibu haya maswali mawili
1. Kama wana akili ama hawana... Swali langu
2.Akili ninini.. Swali la Kiranga
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Akili ni Akili kama anasema sio jibu bas atoe jibu.
Mkuu hapa ndio utajua kuwa Ubishani wao unakwama hoja ila wanaamua tu kubisha kijeuri.
 
Mimi nimeshamjibu zaidi ya mara 15 kuwa AKILI ni AKILI...
kitu cha kwanza nimejibu
Kitu cha pili je jibu langu ni sahihi ama sio sahihi?
Kitu cha tatu kama jibu langu sio sahihi... Jibu sahihi ni lipi? Hapa ndio anapopakimbia

Anataka ujibu jibu analotaka yeye.
 
Mshana na watetezi wake.

Waambie kwamba swali jepesi tu mbona wewe umejibu na tumeendelea na mjadala hujapata kidonda wala kutokwa damu?

Wameusimamisha mjadala kwa swali ambalo halina uzito wowote.

Ndiyo maana nasema hawana hoja.

Mshana Jr amejibu zaidi ya mara moja kwa maana ya kujibu swali ulilomuuliza.
 
Haijawahi kutokea Swali Likajibiaa na Swali hii ni ajabu kwa watu wanajitia wana Ufaham mkubwa kujibu swali kwa swal.

Isiwe shida Swali limejibiwa Kuwa akili ni Akili Mmekataa kuwa hilo sio jibu.... Kwa kukataa inaonyesha kuwa mnamajibu sahihi ya swali tofauti na hilo lililotolewa, Mkiambiwa toeni jibu sahihi basi mmebakia kusema hilo sio jibu.
Kusema 1+1= Sio 2 basi Mnajibu sahihi tofauti na hilo litoeni tupate kujua jibu sahihi.

Hata nikikuuliza Una Roho utaniambia Roho ni Nini. Yani swali linajibiaa kwa Swali.
 
Hauwezi kutaka kujua aina za kitu fulani bila kujua hicho kitu ni nini.

Ukitaka kujua aina za simu lazima kwanza ujue simu ni nini,na mwenye kujua simu ni nini akitaka kujua aina za simu hawezi kuuliza tena simu ni nini.

Sasa nyie mnataka kujua et akili ipi inazungumziwa halafu mnauliza akili ni nini?!!!!!
Kajibu akili ni nini?

Mbna maelezo ya kutaka kujibiwa akili hayatoi?
 
Waungwana,Waheshimiwa saana Mshana jr na Kiranga,pamoja na wajumbe wengine wa barza /baraza,
Nina maswali madogo ya nyongeza,
1) Mna Elimu?
2)Elimu ni nini?
3) Kati ya maswali hayo mawili ,lipi lapaswa kuwa la kwanza kujibiwa?
NB: Tusisahau maswali makuu mawili ya huu mjadala ( Una Akili? Na Akili ni nini?)
Inabidi uelezee kile unachotaka kuuliza ,baadae ndyo uumbane kuwa kwa maelezo haya je kweli kitu hicho unacho?
 
Kajibu akili ni nini?

Mbna maelezo ya kutaka kujibiwa akili hayatoi?
Mbona haueleweki mara useme unataka kujua aina za akili mara tena unauliza akili ni nini!
Hauoni kama unajichanganya?

Hadi sasa haujaeleza ukaeleweka kwamba swali la "una akili?" limekushinda wapi kulielewa?

Hilo neno akili ni neno la kiswahili lenye kutumika kwenye maongezi ya kila siku,ila kama wewe unaona ni neno tata basi unapaswa kueleza jinsi gani hilo neno lilivyo tata kiasi cha kukufanya ushindwe kuelewa kusudio la muuliza swali.

Hauelezi hilo neno kama ni tata au lina maana zaidi ya moja.
 
Back
Top Bottom