Huyu jamaa tangu juzi aliingia katika mtego fulani baada ya mimi kumuuliza maswali kadhaa,akasema hivi "Binadamu hana chanzo sababu yeye ni chanzo cha vingine" muda huo huo akaja kusema "Ulimwengu ndio chanzo cha kila kitu" ,akamalizia kwa kisema hivi "Kwahiyo hupaswi kuhoji juu ya chanzo cha kila kitu". Nikamkumbusha juu ya kujipinga kwa kauli zake hizo mbili. Akabisha sana mwisho wa siku akarukia katika kauli ya mchangiaji mwingine isemayo "Hakuna chanzo cha chanzo" ,mimi nikaja kumwambia hivi "Kanuni ya chanzo kisichokuwa na chanzo ni sawa na mimi kusema hivi kila kitu kina chanzo isipokuwa Mola pekee".
Kazi sasa ndio ikaanzia hapo na yeye akadakia na kusema hivi "Kila kitu kina chanzo isipokuwa Ulimwengu".
Mimi kwa kuokoa muda nikamwambia hivi "Sawa nimekubali jibu lakini sijakubali juu ya usahihi wa jibu lako". Akawa ana bisha kwa kusema hivi "Kwanini useme jibu langu sio sahihi wakati nimetumia kanuni yenu ?". Nikamwambia sis wenye kanuni ndio tunakwambia sio sahihi sababu kanuni hii ni hasa na maalumu kwa Mola pekee,kwa maana kwa kingine haikubali,kama unaona ina kubali jibu maswali yafuatayo,kuna maswali yapo post # 4288 nilimuuliza ili atuonyeshe ya kuwa kwanini Ulimwengu uwe ndio chanzo cha kila kitu. Maswali hayo mpaka kesho kutwa hajayajibu na nina jua hawezi kuyajibu. Kwa ufupi ni hivyo.
Hata wewe kweli ukiambwa kanuni ni "Kila kitu kina chanzo isipokuwa Allah pekee" ukaja ukasema "Kila kitu kina chanzo isipokuwa Ulimwengu", utakuwa sawa kweli ?