Ivi wapiga kura kujadili utendaj usioridhisha wa wabunge wao, ni dhambi?,au kwa sabab anaeonekana kusemwa ni-m4c basi hapo hamna mada????mh!!!!,kaz ipo!
Jamani kinachoelezwa kama ni kweli HM ashauriwe na waliokaribu naye, mambo mengine ni madomadogo, ni vema kama mfalme amekaa vibaya akaambiwa.
CHADEMA kubalini kupokea ushauri ili huyo mbunge wenu wa kawe aendelea kutawala..... badala ya kutukana ..tatizo lenu hamtaki kupokea ushauri kwa mambo yanayohusu chama chenu..mnajiona muda wote mko sawa... ukweli uko wazi mdee hakuna alichokifanya hadi muda huu zaidi ya kupiga kelele bungeni kwa mambo ya jumla jumla tu..... mi nawambia ukweli 2015 wabunge wa upinzani hasa CHADEMA ni wa chache sana watakaorudi kuwa wabunge .... ushauri pokeeni ushauri huu haitajiki hata laki tano kwenda kufanya mkutano na wananchi kwenye maeneo ya wananchi wenye matatizo , yani kufanya mkutano kusikiliza kelo za wananchi nalo linahitaji ela za CCM???.AU USAIDIWE NA SERIKALI???. JITAZAMENI UPYA CHADEMA WENZENU WANATEKELEZA AHADI NINY MNAENDELEE NA MAANDAMANO SASA SIJUI 2015 MTASEMA TULIFANYA MAANDAMANO 100 AU TUMEJENGA ZAHANATI..KAZI MNAYO
Wakuu issue si kukubali kukosolewa.
Kama mtu una akili utajua nani anakupa ushauri kwa kuwa ana nia ya kujenga na yupi ana nia ya kukupaka matope.
Suala la Halima Mdee, kama wapiga kura wake wana nia ya kumshauri kwa wema na si kumpaka matope, email yake ni hii:
hmdee@parliament.go.tz wanaweza kumwandikia. Namba yake ya simu ni hii:
+255 713 569823 nayo wanaweza kumpigia. Namba hizi za wabunge na email zao si siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya bunge.
Kusema hivyo haina maana kuwa watu wasitumie jukwaa hili kukosoa wabunge, bali watoe constructive criticisms, sio kuja na malicious intentions.
Suala hili limevaliwa njuga sana na watu wachache ambao wanapost threads nyingi mfululizo humu kuelezea jambo hilo hilo hata kama wamejibiwa.
Mfano halisi ni
MAFILILI mwanzishaji wa thread hii.
Tarehe 06.03.2012 alianzisha thread hii: Mbunge wetu Halima Mdee, njoo utuokoe Kunduchi Machimboni Nanukuu sentensi ya mwisho: "tulifikiri wewe utakuwa Mbunge bora kumbe AFADHALI wakati wa RITA MLAKI alikuwa karibu na wapiga kura."
Tarehe 18.05.2012 alianzisha thread hii: Mheshimiwa Halima Mdee Kulikoni???
Tarehe 14.06.2012 alichangia post hii: Note red coloured text
By MAFILILI
Halima Mdee + John Mnyika = Hodari wa kupiga maneno, UFUATILIAJI ni ZERO. Wabunge hawa wameshajijua 2015 hawarudi mjengoni hivyo wanashughulika na mambo yao binafsi kuliko kusikiliza na kufanyia kazi kero za wananchi.
Wananachi wa ubungo wanajuta kumpa kura Mnyika, wa Kawe wanasema afadhali enzi za Rita Mlaki alikuwa msikivu na mfuatiliaji
Tarehe 1.7.2012 alianzisha thread: Mheshimiwa Halima Mdee Karibu Tegeta Namanga
By MAFILILI
Pole kwa majukumu ya mjengoni Dodoma, mie mpiga kura wako nachukua fursa hii adimu kukuomba uje sehemu husika, Tegeta Namanga utukisikilize namna tunavyoteseka kuishi nje katika kipindi hiki cha baridi baada ya nyumba zetu kubomolewa na Big Bon, tafadhali njoo haraka!
Tarehe 15.09.2012 ameanzisha tena thread hii Kipindi kigumu jimboni Kawe
Na ninanukuu maneno ya mwisho ya Mafilili: "Kwa kweli wakazi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi tete tunamkumbuka RITA Mlaki ambaye alikuwa karibu na wapiga kura."
Utaona kwenye thread ya tarehe 06.03 yeye ni mkazi wa Kunduchi Machimboni, wakati tarehe 01.07 yeye huyohuyo ni mkazi wa Tegeta Namanga. Hii inaashiria uongo.
Na pia angalia hayo malalamiko ya kuhusu Namanga, wakati huyu
MAFILILI analalamika wako wana Kawe wanaoshukuru tarehe 11.07.2012, na kwa kuwa tayari ametudanganya kuhusu makazi, ni rahisi kusema hata hii ya Tegeta Namanga anasema uongo, anamlaumu kwa kitu ambacho mbunge alitekeleza wajibu wake:
Napenda kumpongeza mbunge wa jimbo la Kawe mheshimiwa Halima James Mdee kwa jinsi alivyokuwa bega kwa bega na wapiga kura wake wa maeneo ya Tegeta Namanga waliovunjiwa nyumba zao na mwarabu mmoja mwenye sheli ya mafuta.Tuna amini kuwa utapigania haki zao mpaka zipatikane na huyu mwarabu awalipe fidia wananchi kwa uharibifu aliowafanyia.Wabunge wengine hasa wa magamba igeni mfano huu wa kuwa karibu na wapiga kura wenu hasa waoapnkuwa na matatizo.
Kwa hiyo pamoja na kujibu na kuonesha amefanya nini kama tulivyofanya kwenye post # 76 na nyinginezo, ni muhimu kurudia tena nia ya wanaopost si kumwangalisha ili atekeleze wajibu wake vizuri, bali ni kumpaka matope.
CCM wanataka bunge ambalo 100% ya wabunge ni CCM. Ikitokea tukarudi huko, bunge litapoteza ile kazi yake kuu ya kusimamia serikali. Mpaka sasa tunaona hawa akina Halima Mdee ndio wanaibua hoja kubwa za kuikosoa na kuwajibisha watendaji wabovu wa serikali. Wabunge wa CCM walio wengi kazi yao ni kupigia makofi mawaziri hata kama wanaongea upuuzi.
Mafilili na wenzake wanatamani sauti hii ya kutetea wananchi inyamaze, na bila shaka wao wanafaidika na kitu, ndio maana kila mara Rita Mlaki amekuwa anatajwa.
Tutafakari,