Kipindi kigumu jimboni Kawe

mbona mr.ii anaendelea kuimba??????....y iwe nongwa kwa mh:ngonyani????
 

Mkuu MAMMAMIA nadhani Halima mwenyewe anaweza kuja kujibu haya madai hata kama ni ya kipuuzi ili kuwaweka sawa wale waliopotoshwa na taarifa hizi, ama msaidizi wake anaweza kuja kutolea ufafanuzi, vinginevyo wakaazi wa jimbo la kawe najua tunao wengi hapa JF wanaweza kushuhdia ni mambo gani mbunge wao aliahiodi na ameyatejkeleza kwa kiwango gani.

Natarajia kukutana na Halima kesho kutakuwa na mkutano Kigamboni na yeye ndiye anatarajiwa kuwa msemaji mkuu, niatamfikishia salamu hizi ili atoe taarifa ya kazi alizofanya so far ili kukomesha huu upotoshaji unaofanyika hapa.
 
Last edited by a moderator:
Watu wanakimbilia ubunge kutafuta riziki na kutengeneza maisha yao.wadanganyika wasioelewa wanakimbilia kutoa kura.

Haf muwe mnajifunza mbunge hana nguvu ya kuleta maendeleo ccm na serikali yake ndo wanajukumu la ulinzi na usalama wa wanamadale yani nakwambia halima wala cdm kwa sasa bado hawana mamlaka ya kuwapoka watz maeneo yao wala atutumii ilani ya cdm kwa hiyo uwezi mlaum mdee kwa sasa ipigie cdm 2o15 uone kama kutakuwa na malalamiko kama yenu hata majimbo yatakayo chukuliwa na magamba kina majimarefu
 
Asante sana Mwanaukweli kwa kutupeleka kwenye chanzo hcho hapo juu. Nimeingia na niliyokutana nayo mengi ndio yale yale, "Mnamlaumu Mdee hakufanya kitu mbona hamuulizi nani na nani wa chama hiki au kile". Watu tunashindwa kutoa hoja; hoja kama hii ni kukataa kujituma kiakili na kuwa mtumwa wa kujituma.

Nimeona hii makala ya Privatus Karugendo na nimedondoa hiyo hap chini kwa faida ya mleta mada na wengine wenye imani kama zake. Zaidi nawaomba wenye hoja dhaifu kidogo wasome kwenye nyekundu na blue:

 
Nadhani si halima mdee tu, majombo yote ya upinzani dar-es-salaam yako hoi. Huyu bwana wa ubungo ndo bomu la ffu. Alidiriki kumwita rais mdhaifu lakini ukweli ukiondoa miradi ya rais jk ya barabara, maji na upimaji viwanja mbunge mnyika hakuna anachoweza kujivunia kuwafanyia wananchi wa ubungo zaidi ya kugawa bodaboda kwa wale vijana waliompigia kampeni. Tunakaribisha mtu yeyote kutoka chama chochote mwenye ubavu tumpe tafu tuondoa hii minyororo ubungo. Yeye akafanye kazi makao makuu ya slaa huko kinondoni. Hatujawahi kuwa na mbunge dhaifu ubungo tangu enzi za wakina derek brycon. Hata kawe wana afadhali
 
Mbunge wa ubungo wakati wa kampeni tuliambiwa alipata A zote form six lakini tumeangalia kwenye mtandao wa baraza la mitihani tunaandaa protest. Alipata three dhaifu na hwkuchaguliwa kwend chuo kikuu labda kama alijipeleka kwenye masomo ya jioni. Huyu bwana hapana
 
Uwezo wa kufikiri na kupata ufumbuzi vinategemea na uwezo wa ubongo wa anaye fikiri!
Huwezi kuruka mkojo uka kanyaga mavi ukajisifia!
kuwa una macho mazima!
Huwezi kuotesha bagi ukavuna mchicha!
Pesa zilizo ibiwa kwenye migodi na mafisadi huzioni ma majaga ya kusafirisha wanyama hai kwa ufisadi pesa ambazo zingetosha kukuondowa ujinga leo unakuja kutufanya wavivu wa kufikiri.endelea kukanyaga mavi baba Aluta...... m4c daima
 
Mwita Maranya Mkuu, kwanza nikiri kuwa hata mimi nilitaka kuburuzwa na nia mbaya ya mleta hoja. Naomba upitie, na hasa ninamuomba MAFILILI apitie post yangu nambari #65 hapo juu au kurejea post ya #80 ya Mwanaukweli hapa HAPA badala ya kuumizana vichwa na watu wasiotumia akili kutetea hoja zao.
 
Last edited by a moderator:
kwani amemaliza siku zake??????????????????????/ mnajuaje si msubiri? ni mwanamke yule khaa!
 

Hii siyo kweli, Ubungo tunaijua na wabunge waliopita Ubungo tunawajua. Mnyika anafanya kazi nzuri kuliko mbunge yeyote DSM (muono wangu). Mnyika yupo karibu sana na wananchi wake kwa kuwasikiliza na kufuatilia masuala mbalimbali ya utekelezaji. Hata hiyo miradi ya JK inafanyika kwa push kubwa ya Mnyika. pole bro upenzi wa vyama anakupofusha usione ukweli.
 
We kweli akili magamba!!!....unamuona Halima Mdee zigo lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe...lakini wakati huo huo humuoni DHAIFU alivyo zigo kwa wapiga kura na kujisaidia mwenyewe, mafisadi wenzake, wageni wanaojifanya wawekezaji na familia yake!!!! Ama kweli Nyani haoni......

Mie nilidhani utajibu hoja unakuja na uzezeta ule ule, pamoja na kukubali kuwa Mdee ni zigo bado hujionyeshi katika hoja, badala yake unavamia wengine. Hizo fitna acha unayemwita dhaifu kwa sababu baba yako Mnyika kasema nawe kuwa kasuku butu. S itashangaa akisema vingine nawe utaukasuku maana huna ya kwako, nawasikitikia wazee wako.
 
Kigoma mwulize Zitto kama si Dubai ya Tanzania sasa, wewe mbona kilaza?
 
Kuna mengi ambayo ameyafanya huyu mbunge:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.

2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.

3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.

4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.

5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.

6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.


7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.

8. Amekuwa anakutana na wananchi na kusikiliza kero zao na kupata maoni yao. Angalia video hii

9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.

10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.

11.
Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.

12. Ameshiriki
unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.

13. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.

Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.

Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha.

Nahisi nyuzi nyingi zinaletwa hapa kwa sababu wanataka kuona juhudi za makusudi za kumkwamisha zimefanikiwaje.

By the way, kati ya wabunge wote wa Dar hakuna ambaye amezorota kama Abas Mtemvu. Mbona haanzishiwi threads nyingi kama Mdee? Na kuna thread ipo nimejaribu kwa makusudi kupost ili iwe juu tuone kama kweli watu wako objective lakini hakuna anayepost kitu kule.

Fikiria vema!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu MAMMAMIA tayari majibu yameanza kupatikana kama unavyoona hii post ya Mwanaukweli. Sasa wafitini sijui watakuja na single gani tena.

 
Last edited by a moderator:
Kutoka thread hii : https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-mbunge-wa-kawe-mheshimiwa-halima-mdee.html

Kuna post hii

Ni kati ya mashahidi wa moja kwa moja akishuhudia jinsi wanvyoguswa na mbunge wao. Yuko karibu na wananchi.
 
Mkuu MAMMAMIA tayari majibu yameanza kupatikana kama unavyoona hii post ya Mwanaukweli. Sasa wafitini sijui watakuja na single gani tena.
Nimependa sana hii, lakini bado wananchi tunapaswa kuelewa kuwa si jukumu la mbunge kufanyakazi za maendeleo kwa kutumia mshahara wake, isipokuwa ametengewa kiasi fulani na serikali kwa ajili hiyo, wala kupita nyumba hadi kuuliza watu wameamkaje na kuhudhuria misisba kama mbunge bali kama jirani katika eneo lake.

Katika yote yaliyotajwa, hilo la kuchangia mawazo bungeni na kuishauri serikali ndio wajibu wake, sasa kama yupo wa kulaumu ni serikali na watendaji wake, hasa viongozi wa chama cha serikali, kinapokataa kufuata ushauri wa mbunge au kwa makusudi kufanya hujuma jimbo kwa mbunge huyo ama kwa ufisadi au kwa lengo la kumpaka matope mbunge husika.

Hongera Mdee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…