Elections 2010 Kipindi cha pata-pata WAPO RADIO FM

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
leo nimefanikiwa kusikiliza kipindi cha PATA PATA katika radio ya WAPO FM 98.0. Kulikuwa na wasikilizaji wanatuma ujumbe wa maandishi kuhusu taarifa zilizokuwa zinatolewa. katika kipindi nilichokuwa nasikiliza jumla ya sms 12 zimesomwa na zililenga katika maeneo matatu:-
  1. zilizokuwa zinasema Dr. Slaa songa mbele, Tutawang'oa mafisadi = 9 = 75%
  2. Zilizosema Upinzani hauwezi kushinda kiti cha uraisi bila kuungana =1 = 8.3%
  3. Zilizoungamkono kitendo cha jeshi kutoa tamko hapo juzi = 2 = 16.7%
  4. Zilizosema JK Juu = 0 = 0%
Mbarikiwe, Amen
 
watu si kwamba wana maslahi kwa slaa au wanamchukia kikwete ila hali ya maisha na ahadi zisizotekelezeka...wakati waTZ wana maisha magumu tunawashudia vigogo na watoto zao wakiishi maisha ya peponi..kisha 2naambiwa tanzania maskini..kikwete ilikuwa apumzike awapishe wengine nao wafanye kitu ili yeye abaki na heshima yake badala ya kulazimisha ushindi wakati anaijua hali halisi...
 
leo nimefanikiwa kusikiliza kipindi cha PATA PATA katika radio ya WAPO FM 98.0. Kulikuwa na wasikilizaji wanatuma ujumbe wa maandishi kuhusu taarifa zilizokuwa zinatolewa. katika kipindi nilichokuwa nasikiliza jumla ya sms 12 zimesomwa na zililenga katika maeneo matatu:-
  1. zilizokuwa zinasema Dr. Slaa songa mbele, Tutawang'oa mafisadi = 9 = 75%
  2. Zilizosema Upinzani hauwezi kushinda kiti cha uraisi bila kuungana =1 = 8.3%
  3. Zilizoungamkono kitendo cha jeshi kutoa tamko hapo juzi = 2 = 16.7%
  4. Zilizosema JK Juu = 0 = 0%
Mbarikiwe, Amen

Wapi Maaria Sugu??
 
Malaria sugu, Hao kumi wamewakilisha wenzao wengi ambao walitamani kutuma maoni hayohayo ila wamepigika ile mbaya simu credit ni -10
 
leo nimefanikiwa kusikiliza kipindi cha PATA PATA katika radio ya WAPO FM 98.0. Kulikuwa na wasikilizaji wanatuma ujumbe wa maandishi kuhusu taarifa zilizokuwa zinatolewa. katika kipindi nilichokuwa nasikiliza jumla ya sms 12 zimesomwa na zililenga katika maeneo matatu:-

  1. zilizokuwa zinasema Dr. Slaa songa mbele, Tutawang'oa mafisadi = 9 = 75%
  2. Zilizosema Upinzani hauwezi kushinda kiti cha uraisi bila kuungana =1 = 8.3%
  3. Zilizoungamkono kitendo cha jeshi kutoa tamko hapo juzi = 2 = 16.7%
  4. Zilizosema JK Juu = 0 = 0%
Mbarikiwe, Amen

wape moyo!!
 
Pamoja na kwamba mwenye WAPO radio kujaribu kumbeba Jk, hapo majuzi alimfanya mgeni rasmi kwenye sherehe fulani hivi, habebeki. Nasema habebeki kwa sababu watu hawawezi kukubeba huku ukiwapiga na njaa na umaskini. Ccm imetengeneza matabaka Tz, kiasi kwamba kuna tabaka la walio chacho wachache na wasionacho walio wengi. Ubaya hapa sii kwa watu kuwa nacho, hapana! Ubaya ni pale wale wachache walionacho wamekifisadi kutoka kwenye hazina ya wale wengi wasio nacho.
JK USIHOFU KUPUMZIKA KWA AMANI, KWANI TUTAKUPA HESHIMA YA RAIS ALIYEKUBALI MAGEUZI. LAKINI UKIUTAKA URAIS KWA GHARAMA YA DAMU TUTAKUTANGAZA KUWA ADUI NAMBA MOJA WA TAIFA LILILOKUA LA AMANI AFRICA. HUTASAMEHEKA KATIKA ULIMWENGU HUU WALA ULE UJAO.
 
Mfumo wa kututia umaskini tulio wengi na kuwatajirisha sana wachache haukubaliki kamwe..
Tunataka mfumo wakutugawia sawa ikiwa unafanya kazi halali...
 
leo nimefanikiwa kusikiliza kipindi cha PATA PATA katika radio ya WAPO FM 98.0. Kulikuwa na wasikilizaji wanatuma ujumbe wa maandishi kuhusu taarifa zilizokuwa zinatolewa. katika kipindi nilichokuwa nasikiliza jumla ya sms 12 zimesomwa na zililenga katika maeneo matatu:-
  1. zilizokuwa zinasema Dr. Slaa songa mbele, Tutawang'oa mafisadi = 9 = 75%
  2. Zilizosema Upinzani hauwezi kushinda kiti cha uraisi bila kuungana =1 = 8.3%
  3. Zilizoungamkono kitendo cha jeshi kutoa tamko hapo juzi = 2 = 16.7%
  4. Zilizosema JK Juu = 0 = 0%
Mbarikiwe, Amen

Wandugu kuweni makini na hizi reference zenu. Redio wapo haiwezi kuwa reference ya kujipia moyo wa matumaini ya kisiasa. Sanasana habari kama hizi zinazidi kuligawa taifa na kugawa kura katika misingi ya dini na sio mbadala makini...
 
Pamoja na kwamba mwenye WAPO radio kujaribu kumbeba Jk, hapo majuzi alimfanya mgeni rasmi kwenye sherehe fulani hivi, habebeki. Nasema habebeki kwa sababu watu hawawezi kukubeba huku ukiwapiga na njaa na umaskini. Ccm imetengeneza matabaka Tz, kiasi kwamba kuna tabaka la walio chacho wachache na wasionacho walio wengi. Ubaya hapa sii kwa watu kuwa nacho, hapana! Ubaya ni pale wale wachache walionacho wamekifisadi kutoka kwenye hazina ya wale wengi wasio nacho.
JK USIHOFU KUPUMZIKA KWA AMANI, KWANI TUTAKUPA HESHIMA YA RAIS ALIYEKUBALI MAGEUZI. LAKINI UKIUTAKA URAIS KWA GHARAMA YA DAMU TUTAKUTANGAZA KUWA ADUI NAMBA MOJA WA TAIFA LILILOKUA LA AMANI AFRICA. HUTASAMEHEKA KATIKA ULIMWENGU HUU WALA ULE UJAO.

Hivi kuna chama mbadala ama mgombea wa chama chochote anayeamini katika kuondoa matabaka???

Mwalimu alijaribu hivi sasa mnamkejeli.....kama alishindwa yeye tutegemee nini kutoka kwa wenye kuamini katika ubepari....Tuache kujidanganya, hakuna mwenye nia wala uwezo wa kuondoa matabaka nchini. Na wengi wanaolia kuhusu matabaka tayari wamekaa mkao wa kula for THEIR TURN TO EAT na ndio maana wako tayari kutishia, ku -condone, kujustify ubagazuzi na hata umwagaji damu kama matakwa yao hayatafanikiwa ama kukubaliwa.....
 
Ndugu zangu,
Nawasihi sana,
Tuwe makini na hizi redio stesheni za ajabu ajabu,
Watu wako tayari kupata au kung'angania madara kwa gharama yeyote,
Hata ikibidi kumwaga damu za watu wasio na hatia.
Wamejaribu kutumia ukanda, ukabila wameshindwa,
sasa wanatumia UDINI.
Hii ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Jana nilibahatika kusikiliza radio moja hapa Dar (104.1 fm) ya kiislam.
Nimerekodi yale mazungumzo.
Nimejaribu kuattch hapa nimeshindwa.
Ila kwa kifupi ni kampeni chafu sana.
Pia kuna watu misikitini wanaeneza uvumi kwamba Slaa anasema kuleta mahakama ya kadhi ni kuchafua katiba.
Ndugu zangu watanzania.
Tuwe macho.
Tuwapuuze hawa "mashetani"

Tuwapime wagombea kwa vigezo vya uzalendo wao,
Uadilifu wao,
Ucha Mungu wao,
nk.

Hivi vyama ni vya kupita tuu,
Ila mustakabali wa nchi yetu ni muhimu zaidi na wa kudumu.
 
Ndugu zangu,
Nawasihi sana,

Tuwe makini na hizi redio stesheni za ajabu ajabu,

Watu wako tayari kupata au kung'angania madara kwa gharama yeyote, Hata ikibidi kumwaga damu za watu wasio na hatia.
Wamejaribu kutumia ukanda, ukabila wameshindwa, sasa wanatumia UDINI.

Hii ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Jana nilibahatika kusikiliza radio moja hapa Dar (104.1 fm) ya kiislam. Nimerekodi yale mazungumzo. Nimejaribu kuattch hapa nimeshindwa. Ila kwa kifupi ni kampeni chafu sana. Pia kuna watu misikitini wanaeneza uvumi kwamba Slaa anasema kuleta mahakama ya kadhi ni kuchafua katiba. Ndugu zangu watanzania. Tuwe macho. Tuwapuuze hawa "mashetani"

Tuwapime wagombea kwa vigezo vya uzalendo wao,
Uadilifu wao,
Ucha Mungu wao, nk.

Hivi vyama ni vya kupita tuu, Ila mustakabali wa nchi yetu ni muhimu zaidi na wa kudumu.

Na wapo pia wenye kutaka madaraka hata kama itabidi kumwaga damu na kuligawa taifa....Lets be honest jamani, hii hatari haisababishwi na upande mmoja tu wa siasa ama dini, wote wana hatia nasi sote ni wahanga wa uchu wao
 
jamni kwa mungu kila kitu kinawezekana hata jk kungoka inaweekana kabisa sioni cha ajabu
 
Na hapo WAPO radio walijitahidi kuchakachua, nawajua wale watoto wa Askofu Gamanywa.
 
Wale wanaotaka wanaweza kuamini lakini tuna references nyingi
1. daily news Dr. Slaa aliongoza wakaifunga
2. Radio Free Africa, mpaka Jumamosi DR. Slaa alikuwa anaongoza
3. Jamii Forum, Dr Slaa anaongoza mpaka sasa kwa zaidi ya 69%
4. katika Majira, Dr. Slaa anaongoza kwa zaidi ya 60%
kwa hiyo kupinga kwa mtu yeyote kunapaswa kurejea angalau sehemu mojawapo ya hizi.

Inawezekana baadhi yetu wanaituhumu WAPO kwa sababu ni ya kikristo lakini je vyombo vingineje? Tuwe makini badala ya kukimbilia udini ambao hauna nafasi katika nchi hii.:moony:
 
Back
Top Bottom