Kipimo cha nchi kuwa na nguvu za uchumi ni kipi?

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Dola moja ya marekani ni sawa na shilling 2326 za Tanzania
Dola moja ya marekani ni sawa na Yeni 11 za japan
Dola moja ya marekani ni sawa na dinar 0.33 za Kuwait

Hela yenye nguvu kuliko zote duniani ni dinar ya Kuwait.Tunaambiwa nchi tajiri kuliko zote duniani ni Luxembourg kanchi kadogo sana hata mkoa wa mwanza ni mkubwa

Shillingi moja ya Tanzania ni sawa na Lira nne za nchi ya Italy kwa maana hiyo ukiwa na shillingi moja tu ya kwetu mutaliano anatakiwa akupe hela zao lira nne ina maana shilling yetu ina thamani kuliko yao na hapo hapo hii nchi ina viwanda vikubwa mno na kiukweli imeendelea mno kuliko sisi

Mambo ya uchumi yanashangaza tunaambiwa Marekani ni taifa kubwa na lenye nguvu za kiuchumi na kijeshi.

Sasa kama ni hivyo inakuwaje tena hela yake isiwe na thamani kama nchi zingine kama Kuwait?

Na je kwanini hela ya marekani ndio kipimo cha fedha zote duniani?

Japan ni nchi iliyoendelea sana kiviwanda na kiuchumi kwanini Yen yake haina nguvu dhidi ya dola?

Je, utajiri wa nchi kipimo chake kiko wapi?

Oneni tena dola moja ni sawa na peso moja ya nchi ya Cuba

Juzi miaka michache nyuma hela ya Zambia ilikuwa chini yetu lakini sasa iko juu kuliko sisi

Wataalamu wa uchumi hebu tupeni shule kidogo kwa hili
 
USA ni nchi yenye uchumi mkubwa sana hapa ni wanaangalia pato lao2la taifa kwa mwaka ambalo ni trillion Za dola 18 ikifuatiwa na uchina yenye dola trillion 14...

Mantiki yake Ni kwamba biashara za ndani na nje zinazofanyika USA zinatengeneza pesa nyingi sana na ili uweze kufikia kiwango icho lazima ufanye biashara na mataifa mengi na Huo ndio ushawishi unaozungumziwa!!

$inatumika kama sarafu yenye nguvu ili kutengeneza standard moja kumbuka kila nchi una sarafu yake...na kwann ni $ inatumika ni kutokana na ushawishi mkubwa wa kibiashara ulionao USA dhidi ga mataifa mengine...

Nimejaribu kujibu kwa namna ninavyoelewa
 
Back
Top Bottom