Kipima Joto: Kuokoa anguko la Elimu nchini, nini kifanyike?

Geeque

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
936
316
Bongo Radio Inakuletea kipindi cha Kipima Joto LIVE kupitia ITV: Mada ya leo inasema: KUOKOA ANGUKO LA ELIMU NCHINI. JE, NINI KIFANYIKE? Tusikilize sasa kupitia http://www.bongoradio.com/128kbps.html

Kama unatumia simu za Android au iphone basi download Tunein Radio app na Unaweza kutupata. Pia tunapatikana kupitia Nokia Radio kwa wale wote wenye simu za Nokia.

Ahsanteni,
Bongo Radio Team.
 
Mbatia ni kichwa! Hakupewa nafasi ya kusikilizwa!
 
Bongo bwana mh!! Kaazi kweli kweli!
Walimu wana mgomo baridi!!

Kenya mpaka raha wazir wa elimu anachekelea kutangaza matokeo
 
Kwa hiyo Wizara ya Elimu wamegoma kushiriki kwenye kipindi hiki muhimu
 
Mbungealiyewasilihahoja ya elimu nakuleta kizazaa bungeni na siri kufichuka baada matokeo yaform4 kutoka. Anazungumzia swala la elimu............
 
kuna mambo hapa - ushahidi wa picha na namba za watahiniwa kuchanganywa - mungu wangu madudu gani ya necta haya
 
Kwa hiyo Wizara ya Elimu wamegoma kushiriki kwenye kipindi hiki muhimu

Masako amesema U-mangi meza umezidi Tanzania! Lakini angekuja mtu kama Mulugo asingeweza lolote katika mjadala huu!
 
mzungumzaji wa ccm asema waziri hana sababu ya kujiuzulu.....
Kama kwaidda maccm hamna kitu vichwani....
Laiti ungemsikiliza huyo dr...diwani wa ccm.....
 
Huyu Doctor msemaji wa mwisho amenisikitisha. Kweli mtu ukishakuwa CCM hata kufikilia kwako kunapungua. Anasema baraza la mitihani wajiuzulu lakini waziri asijiuzulu kwani hao baraza la mitihani si wanawajibika kwa huyu huyu waziri?
 
bujigu bado anaendelea kuwandanganya wananchi, eti anasema baraza la mitihani ni kichaka cha wahuni,
aanataka ndalichako ajiuzuru
 
Bado siasa zinatawala katika kila jambo wanashindwa kuweka machafu ya Wizara kwa uwazi kabisa,kitendo cha Wizara na watawala wake kutokuwasikiliza Walimu ni kutokuwajibika....Waziri na Naibu wake lazima waondoke!.......Uongozi ni team work na sio kiburi na majivuno.
 
kuna mambo hapa - ushahidi wa picha na namba za watahiniwa kuchanganywa - mungu wangu madudu gani ya necta haya
mtasingizia sana lakini ukweli ni kuwa mmedharau mwalimu naye amewadharau basi ngoma droo? chezea walimu wewe! by the way vipi mahakama yenu haiwezi kurebesha matokeo kidogo kuwapa angalau ARV kama vile wakati wa mgomo wa walimu?
 
Huyu Doctor msemaji wa mwisho amenisikitisha. Kweli mtu ukishakuwa CCM hata kufikilia kwako kunapungua. Anasema baraza la mitihani wajiuzulu lakini waziri asijiuzulu kwani hao baraza la mitihani si wanawajibika kwa huyu huyu waziri?

huyu jamaa hata form four hakusoma udoctor kaupata wapi?
 
Mbatia anasema huo unaoitwa mtaala unasema lengo la elimu ya chekechea ni kumwezesha mtoto kukua kiuchumi pia. Anashangaa umakini uko wapi mpaka watu wanataka mtoto wa chekechekea akue kiuchumi!! Kazi kweli kweli!
 
mtasingizia sana lakini ukweli ni kuwa mmedharau mwalimu naye amewadharau basi ngoma droo? chezea walimu wewe! by the way vipi mahakama yenu haiwezi kurebesha matokeo kidogo kuwapa angalau ARV kama vile wakati wa mgomo wa walimu?
hii kitu ni complex haina jibu moja na la moja kwa moja
 
Back
Top Bottom