Kipima Joto ITV,VAT kwenye miamala:TRA watoa udhuru

Tatizo ni ccm
Tatizo kubwa ni wananchi wajinga ambao huwa wanawachagua ccm
 
  • Thanks
Reactions: J C
Kipindi nimetazama, kuna mmoja wa katikati yule alikuwa anajing'atang'ata tu kwa lengo la kutetea serikali ambayo haiteteeki kwa kosa walilofanya.
 
Wewe FYATU ------Wabunge wa upinzani walifukuzwa bungeni na Mama Yenu Naibu Speaker......Wenye macho na masikio wanajua...Mbunge wa upinzani akiongea, anaambia kaa chini......Walienda bungeni kuwa Mabubu?

Mama Yenu alitumwa akaminye demokrasia ili nyie viola za muongezewe kodi bila kujitambua......labda wewe unapata ugali wa shikamoo
Ningeiona busara yenu kama mngetoka nje kugomea hiyo VAT au sintofahamu zinazofanana na hizo ...lakini kusema mmemsusia Naibu Spika wala haina mantiki....ni ubinafsi tu unawatafuna.
 
Mie mwenzenu hawa jamaa zetu kila wakiboronga basi siku hiyo nyumbani watoto hula pilau na mapochopocho kibao
 
  • Thanks
Reactions: J C
Waliotia aibu zaidi ni ukawa ambao wametumwa na wananchi wao kwa maagizo ya Lowasa wanatoka nje na kuwaacha wananchi bila ya uwakilishi
Hebu kama una akili njema ambazo hazijaathiliwa na gambaz toa mbadala wa nini wangefanya Ukawa kuendelea kukaa bungeni kwa mbinyo ccm waliowapa?. Ama mngeanza kulaumu kuwa haya yote yalipita UKAWA wakiwa bungeni ili kuhalalisha uozo wa chama cha magambaz.
 
Wachambuzi wamehitimisha kuwa kwa TRA kukimbia vipindi kama hivi, ambavyo vingetumika kutoa ufafanuzi, inaleta tafsiri mbaya sana kwa wananchi kwamba kuna uwezekano wa TRA imefanya makosa kwenye maamuzi yao. Wamesisitiza rais asikie kilio hiki na TRA wasiogope kutumbuliwa wamuone na rais ili kupata utatuzi wa jambo hili
Ingelikuwa katika watu waliostaarabika nadhani TRA wangejitolea kufanya promo na kulipia gharama za kipindi wiki moja kabla ili kipate ufanisi wa juu kabisa. Maana ilikuwa ni 'golden chance' kwao kuweza kuelezea kile ambacho 'hatuelewi' lakini kitendo cha TRA nzima kuingia mitini huku kipindi kinafanyika Dar es Salaam yalipo makao makuu yao na mita kama 50 tu kutoka kwenye taasisi yao (ITA - Chuo cha kodi) ni wazi hapa hatuna uongozi ya kusimamia ukusanyaji kodi.
Ndio maana labda rais kaweka pembeni suala la 'usalama' na kufikiri ku-outsource wataalamu wa kukusanya kodi kutoka Rwanda na hatupaswi kumlaumu katika hili!
 
Kuna mchangiaji Lipiga simu alinichekesha eti alisema TRA eti nao hawajashirikishwa.ndio maana wanashindwa kutetea hoja.
 
Kila kodi duniani mlipaji ni consumer. Hakuna kodi ambayo mlipaji siyo consumer.
Mlipaji kodi yeyote yule ndiye mtumizi.

Kwa kutumia "Substraction Method", VAT inakuwa included kwenye final price na hulipwa na retailer.

 
Ningeiona busara yenu kama mngetoka nje kugomea hiyo VAT au sintofahamu zinazofanana na hizo ...lakini kusema mmemsusia Naibu Spika wala haina mantiki....ni ubinafsi tu unawatafuna.


Kama ilivyo haki kwa binadamu yeyote kuvuta oxygen vivyo hivyo ni haki ya kila mmoja wetu kutoa maoni yake bila kujali yanawafurahisha au kuwaudhi wengine mradi asivunje sheria. Nawe unayo hiyo haki!

UKAWA walitoka bungeni baada ya kuona 'wanawavuruga' wenzao kujadili kwa umakini masuala muhimu ya nchi. Waliobaki wakapata muda mzuri wa kujadili na walichokuja nacho ndicho hiki. Je, ni busara kwenda mbele au kurudi nyuma!?
 
Jamaa wanachekesha eti wanajitoa Ufahamu.wanajifanya hawajui VAT nani anatakiwa alipe wanasema hao wanyonge wasilipe maana yake hawataki kujua Application za VAT.hii kodi hua haichagui uwe mnyonge utalipa tu
 
Shida kubwa sana ya nchi yetu ni mfumo. Haya tunayoyaona yanajadiliwa na kulumbaniwa yalipaswa kujadiliwa na kulumbaniwa BUNGENI na Wabunge na sisi kuletewa final product.

Kwa kuwa Bunge letu sasa limekuwa jumuiya ya CCM, kule bungeni mijadala imekoma badala yake watu wazima wanafunga safari kwenda kuwaombea wananchi wao MINARA YA KUMBUKUMBU ZA PUSH UP huku masuala ya msingi yakikosa mtu wa kuyajadili na yakaishia kuamuliwa kwa NDIOOOOOOOO.

Kodi ni suala la kisheria na sio mahaba. Uchumi wa nchi unaweza kuathiriwa vibaya au vizuri na maamuzi yeyote yale yanayohusu kodi na utekelezaji wake. VAT sio neno geni, tunalifahamu na limetung'ata kwa muda...kuna nini leo hii VAT ianze kuchagizwa kwa kuombewa tafsiri mpya kunusu anguko la maamuzi yaliyofanywa na watunga sera wa upande uliopewa dhamana?

Yaani Bunge sasa ni taasisi ya 'ndio mzee' na hoja ni kusifiasifia kila kitokacho kwa anayepaswa kusimamiwa badala ya kusimamia. Hivi, nyie wabunge wa CCM mnajisikiaje tunapoanza kufanya kazi yenu? Nawasema nyie kwa sababu, ni nyie ndio mliokabidhi 'kiti' kwa serikali, sasa serikali inaongoza bunge na hamna wa kuikosoa kiasi ukosoaji unakuja kufanywa na wananchi baada ya sera kupita.

Nafikiri sasa ndio Watanzania waone nchi hii bila upinzani inafananaje. Haya mambo bwana yalipaswa kujadiliwa bungeni. Hakuna chujio kule sasa tumeletewa juice ya pilipili tuinywe kwa mahaba
mkubwa,hivi mfumo ni nin?hizi hoja zinazo anza na mfumo huwa zinakanganya sana
 
Mjadala huu umewapa aibu ya mwaka Wabunge wa CCM waliopitisha sheria hii pasipo kujadili kwa kina na kutafakari wao walipiga makofi tu na kutamka naunga mkono 100%,
Aibu ni kwa kiti,wala sio wabunge,kwan hukuona walivokuwa wakivutwa mashati kuingia ndani?
 
Back
Top Bottom