Kipima Joto ITV,VAT kwenye miamala:TRA watoa udhuru

hivi kwani wabunge wa upinzani,hawakuchaguliwa kipindi hiki?au wanakazi zao za nje muhimu zaidi..najaribu kuwaza kwa sauti
Kwa akili zako hizi,utakuta wewe ndio unalipa kodi mara tatu tatu na wala hujui,sababu kichwani kweupe,nime jiridhisha na hii post yako
 
Tusubiri wataalam wa kodi kutoka Rwanda Huenda tukapata ufafanuzi juu ya hili la VAT
Kwa kumbukumbu zangu, haina haja ya kwenda Rwanda, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mzee BWM ndiye muanzilishi wa VAT kwa Tanzania. Anaweza kuulizwa kuhusu miamala ya fedha ni VAT INCLUSIVE au VAT EXCLUSIVE. Kama ni Inclusive, basi Benki zilipe(ingawa lengo la VAT hasa ni kuongeza thaman ya bei ya bidhaa/huduma)! Na kama ni VAT EXCLUSIVE, basi KISHERIA, mwananchi anatakiwa alipe.
 
Kwenye hii issue inaelekea kuna communication breakdown kati ya wadau-serikali (wizara, TRA), bunge, na mabenki(Benki kuu na Bank za Biashara).

Mabenki inavyoonekana wametafsiri vizuri kile kilichopitishwa na ndio maana Gavana anawaunga mkono. Bunge sijui kama walielewa wanachofanya kwani ndio wamepitisha kitu ambacho si sawa. Lakini tatizo kubwa ni kati ya TRA na serikali.

TRA ndio wakusanyaji wakubwa wa kodi kwa hiyo wanatakiwa wajue maana ya neno vat na mchakato wa kukusanya. Imekuwaje washindwe kumueleza waziri ya kwamba anachotaka sio vat? Na Bunge wameshindwaje kujua tofauti ya dhamira ya serikali (watoa huduma walipe kodi na si wananchi) na sheria ya VAT? Kulikuwa na mawasiliano kiasi gani kati ya TRA na Wizara kwenye hili?

Au hakuna anaetaka kumueleza mfalme (serikali) kwamba ingawa dhamira yao ni sawa kiuchumi lakini haiendani na sheria yetu ya VAT.

Nafikiri ndio maana TRA walikwepa kikao cha jana-wanajua wameshalikoroga (kama walishirikishwa) au serikali sio sikivu mpaka sasa wamekwaa kizingiti. Labda hili itabidi lirudi tena bungeni kama issue ya simcard.

Je wabunge wa UKAWA wangeweza kuliona hili? Sijui-lakini kwa majukumu ya upinzani ambayo hujumuisha kutafuta matobo katika miswaada ya serikali kwa darubuni kali zaidi, inawezekana wangeliona hili.
 
mkubwa,hivi mfumo ni nin?hizi hoja zinazo anza na mfumo huwa zinakanganya sana
MFUMO = Namna.

Hapa kwetu, Bunge sio chombo cha kuisimamia serikali. Hapa kwetu bunge linaamrishwa na serikali na lenyewe linabaki kulalamikalalamika tu. Kwa mfano, wakati wabunge wanaona jambo fulani si zuri kwa jamii, still wanaiconsult serikali kupata mawazo badala ya kutoa mwongozo.

Huyu unayemuona akikalia kiti cha spika, katoka serikalini. Leo hii ataweza kuisimamia serikali?

Mbunge wa upinzani anauliza swali, anatokea mbunge wa CCM kujibu hilo swali na vijembe juu as if limeulizwa Lumumba. Huo ndio mfumo usio rasmi wa bunge letu. Na haya tunayoyaona ni matokeo ya huo mfumo wa Bunge lisilo na madaraka.
 
Kwa akili zako hizi,utakuta wewe ndio unalipa kodi mara tatu tatu na wala hujui,sababu kichwani kweupe,nime jiridhisha na hii post yako
mkuu hili povu lote la nini?nimeuliza wabunge wa upinzani walikuwa wapi wakati wa hili linaendelea..si ungejibu tu!au wanatutea kwa nje?ikiwa jinalao tu wa-bunge; ilibid wawe ndani,ndio maana nauliza mkuu
 
MFUMO = Namna.

Hapa kwetu, Bunge sio chombo cha kuisimamia serikali. Hapa kwetu bunge linaamrishwa na serikali na lenyewe linabaki kulalamikalalamika tu. Kwa mfano, wakati wabunge wanaona jambo fulani si zuri kwa jamii, still wanaiconsult serikali kupata mawazo badala ya kutoa mwongozo.

Huyu unayemuona akikalia kiti cha spika, katoka serikalini. Leo hii ataweza kuisimamia serikali?

Mbunge wa upinzani anauliza swali, anatokea mbunge wa CCM kujibu hilo swali na vijembe juu as if limeulizwa Lumumba. Huo ndio mfumo usio rasmi wa bunge letu. Na haya tunayoyaona ni matokeo ya huo mfumo wa Bunge lisilo na madaraka.
kwa hiyo mkuu wanaposema tuondoe MFUMO maanake tuondoe NAMNA,now I see...
 
Unajaribu kufanya mazungumzo, lakini ni mazungumzo ya kipumbavu.

Sidhani kama kuna mtu anaweza kuondoa mfumo...bila shaka ni kuubadili. Namna tunavyoenenda ndio mfumo wetu, haijalishi ni rasmi au siyo rasmi.
 
Kwenye hii issue inaelekea kuna communication breakdown kati ya wadau-serikali (wizara, TRA), bunge, na mabenki(Benki kuu na Bank za Biashara).

Mabenki inavyoonekana wametafsiri vizuri kile kilichopitishwa na ndio maana Gavana anawaunga mkono. Bunge sijui kama walielewa wanachofanya kwani ndio wamepitisha kitu ambacho si sawa. Lakini tatizo kubwa ni kati ya TRA na serikali.

TRA ndio wakusanyaji wakubwa wa kodi kwa hiyo wanatakiwa wajue maana ya neno vat na mchakato wa kukusanya. Imekuwaje washindwe kumueleza waziri ya kwamba anachotaka sio vat? Na Bunge wameshindwaje kujua tofauti ya dhamira ya serikali (watoa huduma walipe kodi na si wananchi) na sheria ya VAT? Kulikuwa na mawasiliano kiasi gani kati ya TRA na Wizara kwenye hili?

Au hakuna anaetaka kumueleza mfalme (serikali) kwamba ingawa dhamira yao ni sawa kiuchumi lakini haiendani na sheria yetu ya VAT.

Nafikiri ndio maana TRA walikwepa kikao cha jana-wanajua wameshalikoroga (kama walishirikishwa) au serikali sio sikivu mpaka sasa wamekwaa kizingiti. Labda hili itabidi lirudi tena bungeni kama issue ya simcard.

Je wabunge wa UKAWA wangeweza kuliona hili? Sijui-lakini kwa majukumu ya upinzani ambayo hujumuisha kutafuta matobo katika miswaada ya serikali kwa darubuni kali zaidi, inawezekana wangeliona hili.
Kukimbia was the best option mkuu. Kwa muungwana, kupewa kazi ya kwenda kusema rangi ya damu ni samawati inalazimu ujitoe fahamu kweli kweli!

Wenzao waliopo bungeni wamejificha, wao wanaitwa hadharani. Kazi ile babu
 
Unajaribu kufanya mazungumzo, lakini ni mazungumzo ya kipumbavu.

Sidhani kama kuna mtu anaweza kuondoa mfumo...bila shaka ni kuubadili. Namna tunavyoenenda ndio mfumo wetu, haijalishi ni rasmi au siyo rasmi.
oky,i got the point...eenh kuubadili "MFUMO" ndio tunafanyaje sasa,tunatoa CCM tunaweka "CHADEMA" ndio hivi mkuu au imekaaje?
 
Hebu kama una akili njema ambazo hazijaathiliwa na gambaz toa mbadala wa nini wangefanya Ukawa kuendelea kukaa bungeni kwa mbinyo ccm waliowapa?. Ama mngeanza kulaumu kuwa haya yote yalipita UKAWA wakiwa bungeni ili kuhalalisha uozo wa chama cha magambaz.
Hakuna mbinyo wowote wao wangekomaa tu na hapo ndiyo wangeona wanatetea wananchi wao.
Kila kitu lazima upiganie ukisusa wenzio wala
 
Kwa hiyo kuna waliokula?

Kichwani kwako kutupu. Hili ni moja tu ambalo CCM imelipitisha bila kuulizana, sasa jiulize nchi hii bila mawazo mbadala ndio itakuwa inaendeshwa hivi?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom