OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,677
- 120,360
Kipima Joto kinaendelea usiku huu.Swali ni kuwa Marekebisho mbalimbali ya Kodi na tozo katika bajeti mpya?Kutokana na maswali mengi ya wananchi kukosa majibu toka kwa mtu wa TRA,mtangazaji Jackline Siremi anatoa taarifa kuwa mwalikwa wa TRA hakuweza kuja studio kutokana na ratiba ya zake kuingiliana!Mdau mmoja amepiga simu na kusema kuwa jambo la 18% kwenye mialama limekosa majibu,hata mwakilishi wa TRA akihojiwa Channel 10 alikuwa akijichanganya sana jambo ambalo linatafsirika kuwa wamekimbia kipindi.
Wachambuzi wametia shaka kuwa VAT kwenye miamala haikuwa shirikishi kwa wadau na ndio maana hakuna maelewano!Rais wa mawakala wa forodha anasema TRA imeshindwa kutoa elimu ya kodi.Amelaumu sana watalaam serikalini kutokuwa tayari kupata maoni ya wadau nje ya mfumo wa serikali kutokana na kujiona wanatosha kwa kila kitu!Wachangia wote kwa njia ya simu wamesisitiza kuwa VAT inamlenga mlaji
Wachambuzi wamehitimisha kuwa kwa TRA kukimbia vipindi kama hivi, ambavyo vingetumika kutoa ufafanuzi, inaleta tafsiri mbaya sana kwa wananchi kwamba kuna uwezekano wa TRA imefanya makosa kwenye maamuzi yao. Wamesisitiza rais asikie kilio hiki na TRA wasiogope kutumbuliwa wamuone na rais ili kupata utatuzi wa jambo hili
Aidha wabunge (ambao ni wabunge wa CCM, baada ya ukawa kukatazwa kuongea)wamelaumiwa pia kwa kushindwa kuwawakilisha wananchi ipasavyo na kushindwa kuishauri serikali