Kipima joto ITV: Kauli ya Mwalimu Nyerere juu ya maswala ya udini na ukabila

Nimefurahishwa sana na kiongozi wetu mkuu wa Waislam wa mkoa wa DSM.Sheikh Alhad Mussa Salim ni jembe kweli kweli.Mungu Ambariki.
 
Kumfananisha Sheikh Salum na Ponda ni kumkosea adabu. Sheikh Salum ni kiongozi mahiri nadhani watu wengi tunakubaliana katika hili, na hata wasiokuwa waislamu bado wanamkubali sana.

Mwita Maranya,
Nakushauri jikite tu kwenye mjadala ukianza kuleta mambo ya kuwafananisha Masheikh yupi bora na yupi sio bora utaleta mjadala mwingine.
 
Last edited by a moderator:
MwanaJF omarilyas anazungumza vizuri sana chanzo na mazingira ya udini kwamba inaanzia katika level ya kifamilia. Badala ya kufundisha mazuri ya dini zetu badala yake watoto wanafundishwa ubaya wa dini nyingine hivyo kujenga chuki kwa watu tangu wakiwa wadogo kuwachukia wa dini nyengine.
Kwamba waislamu wanafundishwa ubaya wa ukristo na wakristo wanafundishwa ubaya wa uislamu.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mzee Darus Abeid anakumbusha kisa cha mwalimu Nyerere kukemea udini mwaka 1958 pale alipomkemea mjumbe wa kamati kuu ya TANU sheikh Takadir hadi wananchi wakasusia duka lake lililokuwa kariakoo.
Nimekumbuka masimulizi ya sheikh Mohamed Said

ina maana JKN naye kumbe alikemea udini kama alivyokemea JK.?
 
Last edited by a moderator:
Hata hivyo huyo shekh atakuwa mnafki kwa sababu anajua jinsi nyerere alivyofuta jumuiya ya kiislamu ya afrika mashariki na kupendekeza iundwe bakwata
 
Mwita Maranya,
Nakushauri jikite tu kwenye mjadala ukianza kuleta mambo ya kuwafananisha Masheikh yupi bora na yupi sio bora utaleta mjadala mwingine.

Mkuu Ritz nilikuwa najibu hoja ya Chilli lakini pia kutumia haki yangu ya kutoa maoni juu ya hawa viongozi wawili ambao ni maarufu hapa nchini na wana wafuasi wengi ndani na nje ya dini zao.
Nadhani utakuwa mfuasi wa sheikh ponda na ni haki yako kwahiyo usijisikie unyonge kumtetea mahali popote.
 
Last edited by a moderator:
naona maoni ya wadau wengi katika mitandao ya facebook na twitter kwa kadri masako alivyosoma, wanamponda mwalimu, kuwa ndiye alikuwa muasisi wa udini na ukabila anzia jeshini mapaka mashuleni.. duuh kazi ipo kweli haya maswala yamefika mbali sana, na kwa maoni yangu naona huu ufa unazidi siku hadi siku.
 
wakuu tujikite katika mjadala, tuachane na maswala ya ufuasi wa dini tafadhali haya mambo ni ya hatari sana
 
shekhe anafunguka, anasema kuna chembe chembe za udini kati yatu, anasema udini ni hari ya mtu kumnyima mtu haki yake kisa ni dini tofauti na wewe, lakini anasema kama mtu anaililia dini yake au anaipenda dini yake huo si udini, anasema mtu apewe kazi kwa sababu ya uwezo wake wala si kwasababu ya dini yake

yap MTU APEWE KAZI KWA SABABU YA UWEZO WAKE NA WALA SI DINI YAKE.
Huyu jamaa anamlenga nani hapa....au anamlenga ZITO na sintofahamu ndani ya chama chake nini.?
 
Mkuu Ritz nilikuwa najibu hoja ya Chilli lakini pia kutumia haki yangu ya kutoa maoni juu ya hawa viongozi wawili ambao ni maarufu hapa nchini na wana wafuasi wengi ndani na nje ya dini zao.
Nadhani utakuwa mfuasi wa sheikh ponda na ni haki yako kwahiyo usijisikie unyonge kumtetea mahali popote.

Mwita Maranya,
Mie sio mfuasi wa Sheikh yoyote dini yetu ni haramu kumfuata mtu tuna muongozo wetu...wewe sio muislam huwezi kujua Sheikh msafi kwa Waislam hata kama una tumia haki yako itumie vizuri mie siwezi kukuambia Mchangaji Mtikila au Kakobe ni bora kuliko Pengo mie sio Mkiristo naweza kuwaona wote sawa tu, wala mie sipo hapa kumtetea Ponda nakufahamisha tu jikite kwenye hoja ya msingi utachafua mjadala.
 
Last edited by a moderator:
naona maoni ya wadau wengi katika mitandao ya facebook na twitter kwa kadri masako alivyosoma, wanamponda mwalimu, kuwa ndiye alikuwa muasisi wa udini na ukabila anzia jeshini mapaka mashuleni.. duuh kazi ipo kweli haya maswala yamefika mbali sana, na kwa maoni yangu naona huu ufa unazidi siku hadi siku.

Wengi wao kama si wote waliochangia wakimponda mwalimu ni walewale wa upande ule uliokuwa unaendesha mahubiri ya chuki dhidi yake kwahiyo mimi binafsi sishangazwi na maoni yao.
 
mhhh shekhe anasema sasa mambo haya yamefika hata katika shule za chekechechea eti mtoto anapewa pipi anaambiwa ni from jesus, halafu anasema amtoto anapewa mkate uliongua mtoto anaambiwa huo ni from muhamad, dahaaa wadau kama yamefika hapo kazi ni kubwa kuliko tunavyodhani, anasema sasa kuna udini katika elimu na kazi
 
Mkuu ritz na nini naona umekwazika kaka, turudi katika mjadala na tuangalie nini cha kufanya kurekebisha hili, hv mkuu kwanini viongozi hawakemei haya
 
Mmeona ,mwita umesema umemkubali shehe.
Unamsikia.
AJIRA ZINATOLEWA KWA KUFUATA DINI YA MTU.
Nyerere hakua malaika.
Mkuu mwita mpaka hapo bado unamkubali huyo shehe au umebadili mawazo.
 
Back
Top Bottom