Tanzania inamhitaji ‘Nyerere’ sasa kuliko wakati wowote

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
324
909
Mchana, Oktoba 14, 1999, wimbo wa Taifa unasikika redioni na runingani. Kila mtu wima kwenye redio na televisheni. Miaka 24 imepita, sijasahau tangazo.

Rais aliyekuwa madarakani, Benjamin Mkapa, mkono wake wa kulia aliketi Makamu wa Rais, Dk Omar Ali Juma na kushoto Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye, alitangaza kifo cha Mwalimu Julius Nyerere.

Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa, alisafiri kwenda London, Uingereza, kwa ukaguzi wa afya. Alitembea mwenyewe. Kwa miguu yake, alipanda ngazi za ndege bila usaidizi. Safari ya Hospitali ya Mtakatifu Thomas.

Mkapa, Rais mwenye nidhamu ya mawasiliano kwa umma. Alitoa taarifa mara kwa mara kuhusu maendeleo ya kiafya ya Mwalimu Nyerere. “He is recovering slowly”– “Anapona taratibu,” Rais Mkapa alinukuu ripoti ya madaktari.

Siku ya mwisho ya Septemba 1999, taa nyekundu iliwaka. Mwalimu Nyerere aliwekwa wodi ya uangalizi maalumu (ICU). Msamiati uliotawala vyombo vya habari hususan magazeti ni “hali ya Baba wa Taifa”.

Wingu la wasiwasi likatanda. Nchi itabaki salama bila Mwalimu Nyerere? Hakutatokea vita? Muungano wetu je? Hayo ni maswali yaliyochukua nafasi, kipindi cha kuiwazia Tanzania bila Mwalimu.

Mkapa, alitambua wasiwasi wa wananchi. Alipotangaza kifo cha Baba wa Taifa, alieleza kuwa Mwalimu Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume, walijenga misingi ya umoja wa kitaifa. Aliwatuliza wananchi. Naam, nchi ilivuka salama.

Hofu kuwa Tanzania ingevunjika vipande vipande bila Baba wa Taifa ina matawi mengi. Kwanza ni hadithi kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa na nguvu za ziada.

Hadithi ya fimbo yake kuwa aliisahau mezani, alipokuwa anafanya mkutano, na hakuna aliyeweza kuiinua, vilevile ujazo mwingi wa simulizi kuwa fimbo ya Mwalimu, ilifanikisha chochote alichohitaji.

Ni fimbo kutoka Ufipa. Ndivyo veterani wa siasa, Paul Kimiti, alinisimulia. Wafipa walimpa Mwalimu zawadi ya fimbo kutambua kuwa ni mtoto wa kichifu. Mwana wa Chifu Burito.

Hadithi zenye kuwakweza viongozi na kuwavika ujasiri na uziada, ni kawaida Afrika. Lee Njiru, Mkuu wa Habari wa Jomo Kenyatta, amesimulia alivyoogopa kukutana na Rais huyo wa kwanza wa Kenya.

Njiru ameandika kwenye kitabu chake “President’s Press Man&– “Mwanahabari wa Rais”, kuwa zamani alisikia Kenyatta alikuwa na nywele kwenye ulimi, macho yenye kuwaka moto hadi kwenye paji la uso na aliweza kujua unachowaza bila kumtamkia. Hadithi hizo, zilimfanya apate hofu kukutana naye mara ya kwanza alipokwenda kuripoti kazini.

Hadithi hizo zilivuma zaidi kipindi hicho cha mawasiliano ya kijima. Siku hizi televisheni na Tehama kwa upana wake, vilevile elimu na ujuvi mwingi wa watu, huwezi kuwachota na kuwafunga kamba kama zamani.

Mwalimu Nyerere, pamoja na hadithi nyingi za uongo na kweli, haiba yake ni mtaji. Mzalendo, jasiri.

Maisha yake yote alijipambanua kama baba wa nchi. Aliituliza nchi ilipohitaji utulivu. Alizima majaribio yaliyoonesha dalili za kugawa Watanzania.

Tanganyika na Zanzibar, kisha Tanzania. Kwa makosa na usahihi, aliutetea Muungano hadi alipovuta pumzi ya mwisho. Tamka kila sifa kuhusu Mwalimu Nyerere. Shika hili kwa mkazo. Ni Baba wa Taifa kwa haki.

Mkataba wa DP World
Mkataba wa Ushirikiano baina ya Tanzania na Dubai kuhusu bandari, umetusogeza mahali tenge. Hakika, nchi ipo tenge. Tunakosoana kwa udini. Utanganyika na Uzanzibari ni hoja inayojengwa kwa ujasiri na fahari.

Hakuna wa kusimama kukemea mijadala ya mgawanyiko. Sasa ni fahari Mtanganyika kumshutumu Mzanzibari.

Wazanzibari wapo kimya, ila dhahiri wahafidhina wa visiwani wanapenda mjadala, kwani unachokonoa agenda ya kuvunja Muungano.

Aliwahi kuning’ata sikio Dk Idd Mandi, mwanazuoni wa sheria na mwalimu wa Shule ya Sheria Tanzania, kwamba Wazanzibari, hasa wahafidhina, walichekelea serikali tatu, maana zilikuwa jirani na kuvunja Muungano.

Dk Mandi alikuwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Sikutegemea kauli ya Profesa Palamagamba Kabudi kwamba anaogopa mno Watanganyika watakapoanza kudai Tanganyika yao, ingetimia haraka hivi. Mjadala ni mkataba wa bandari. Makosa na usahihi wake, ghafla ajenda inayorukiwa ni udini, Utanganyika na Uzanzibari.

Mwalimu Nyerere, bila cheo chochote, ila kwa kutambua yeye ni Baba wa Taifa, alisambaratisha vuguvugu la G55. Wabunge wa Tanganyika, walioanzisha hoja ya kudai Tanganyika.

Zanzibar haikuwa shwari. Vuguvugu za kujitenga zilirindima kwa ujivuni na fahari kubwa. “Sisi Wazanzibari”. Mwalimu Nyerere hakutulia Butiama au Msasani, kuacha mambo yaende segemnege.

Alifanya mkutano wa kihistoria Kilimanjaro hoteli, siku hizi inaitwa Hyatt Regency The Kilimanjaro. Mwalimu Nyerere alikumbusha, upande wowote ambao ungeanza chokochoko za kujitenga, usingebaki salama.

Ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu. Mwalimu Nyerere alitahadharisha. Mla nyama ya mtu hatoacha.

Ataendelea. Alilenga kukumbusha kuwa Tanzania baada ya kuvunjika Muungano itabaki vipandevipande.

Mwalimu alisema, Zanzibar baada ya Muungano ni Unguja na Pemba, kisha kuna Wazanzibari na Wazanzibara.

Vilevile Tanganyika baada ya Tanzania, yatazuka ya ukanda na ukabila. Ni kanuni ya kula nyama ya mtu.

Hutaacha!

Hivi sasa, Waislamu kwa ujasiri mkubwa wanatoka hadharani na kudai ukomo wa mkataba wa Kanisa na Serikali. Wanasema mjadala wa bandari, agenda nyuma yake ni udini.

Ni kipindi ambacho nchi inamhitaji zaidi baba wa kukemea. Awafanye watu wajadili hoja kwa kuheshimu misingi ya umoja wa kitaifa. Mkataba wa Dubai na Tanzania kuhusu bandari, ujadiliwe kwa upungufu au ubora wake. Si kutazama chimbuko la watu.

Kauli kwamba Samia na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ni Wazanzibari na wanauza mali za Watanganyika, haikupaswa kutamkwa. Tuupinge mkataba kwa ubovu wake. Tuutetee kwa uzuri wake.

Kukosekana kwa baba wa kunyamazisha kauli za uchonganishi na ubaguzi, inasababisha nione kwamba Tanzania inamhitaji Mwalimu Nyerere sasa kuliko wakati wowote. Nani avae viatu vya Mwalimu?

Namkumbuka Mkapa, mwanafunzi hasa wa Mwalimu Nyerere. Nyakati za kumtukuza Rais John Magufuli, alisema bila hofu kuwa “ipongezwe Serikali ya CCM, sio Magufuli.” Alithubutu kukemea mtu mmoja kujazwa kila sifa.

Mungu amrehemu Jaji Augustino Ramadhan. Alisema mbele ya Rais Magufuli kuwa “amani ni tunda la haki, kwamba Serikali itende haki, amani itajitengeneza yenyewe. Huwezi kuhubiri amani, wakati hutendi haki.

Mwalimu Nyerere mwingine?
Marais wastaafu walio hai, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wawili, Jakaya Kikwete na Ali Hassan Mwinyi.

Walikuwepo wakati Mwalimu Nyerere akiituliza nchi vipindi vya vuguvugu za utengano. Hawaigi?

Je, wanaogopa kuwa kuna watu hawatawasikiliza au watazodolewa? Mwalimu Nyerere hakuwa akipingwa?

Alisimama na kujenga hoja kwa ujasiri mkubwa kwa sababu aliamini yeye kama baba, hilo lilikuwa jukumu lake kurudisha watu kwenye mstari.

Hata Kikwete kwa nafasi yake, hapaswi kuogopa kupingwa. Asimame akemee matamshi ya kuwagawa Watanzania kwa dini zao au Utanganyika na Uzanzibari. Mwinyi anaweza kupewa msamaha wa umri.

Imefikia mahali, mtu akisimama kupinga mjadala wa bandari, linatazamwa jina lake, je, lina uhusiano na dini gani? Vivyo hivyo akitetea. Kisha inagawanywa kuwa wapingaji ni wa dini hii na watetezi ni wa dini ile. Hii ni mbaya sana.

Mwalimu Nyerere alikula sahani moja na Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe, ilipogundulika alikuwa na rasimu ya Katiba inayotengeneza mazingira visiwa hivyo kujitenga. Iweje sasa ni ufahari mkubwa kushutumiana kwa Utanganyika na Uzanzibari?

Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar. Rais wa Tanzania kwa vile ametoka Zanzibar, akifanya uamuzi bandari ya Dar es Salaam, anakuwa Mzanzibari muuza Tanganyika. Anaposimamia ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)na Bwawa la Umeme la Julius Nyerere, ni Mtanzania. Hii ni mbaya sana.

Tanzania inahitaji sana baba, mithili ya Mwalimu Nyerere, asimame bila kuogopa kuzomewa, awarudishe wananchi kwenye mstari sahihi wa kujenga hoja. Ujadiliwe mkataba. Upingwe au utetewe wenyewe.

Majaji wakuu wengine wastaafu walio hai, Barnabas Samatta na Chande Othman hawaoni mpasuko wakasimama na kukemea? Kati yao hawezi kupatikana wa kuthadharisha juu ya hili?

Hulka ya kutazamana usoni na kubaguana, ni mbaya. Ile kamati ya amani ya viongozi wa kidini ipo wapi?

Inahitajika sasa kuliko wakati wowote.

Heshima ya Utanzania ni ile hali ya kuishi bila ubaguzi wa dini na makabila. Kwa nini sasa?

Nilifurahi mno kesi ya kupinga Mkataba wa Tanzania na Dubai, ilipofunguliwa Mahakama Kuu, Mbeya. Nikatamani kuona shauri linaendeshwa wazi (open court), tuone mnyukano wa kisheria, Watanzania wajionee na watofautishe maziwa na tui la nazi.

Mara, wanasheria waliofungua kesi, wanafanya mikutano na waandishi wa habari na kutoa mashambulizi makali kuhusu mkataba.

Je, huko sio kuingilia uhuru wa mahakama na kutengeneza mazingira ya kuathiri hukumu, yaani prejudice?
By Luqman Maloto

Via Mwananchi newspaper
 
Kuna jamaa tulikua naye anadai Nyerere ndiyo chanzo cha Taifa kufika hapa bado naitafakari Ile kauli wakati mwingine Kikwete anaonekana upatu shujaa kwa udhaifu aliofanya Nyerere katika mifumo ya Nchi.
Yeye kama aliteleza ni wajibu wa wengine sasa kuweka mambo sawa ila ni kama kila mtu anafurahi kuja na lake na kuondoka
 
Huyu jamaa aisee
 
Yeye kama aliteleza ni wajibu wa wengine sasa kuweka mambo sawa ila ni kama kila mtu anafurahi kuja na lake na kuondoka
kuna mazuri mengi alifanya, ila kuna mabaya mengi pia alifanya na ndio tunahangaika nayo hadi leo, kwasaba hiyo, hatutakiwi kuendelea kumlaumu bali kupokea kijiti na kuendelea kuanzia hapa tulipo kwenda mbele. lawama hazitatusaidia.
 
Kweli kabisa
Sio kukaa na kusema tu mtu fulani angekuwepo kama vile nyie mliobakia wote vichwa havifanyi kazi
 
mali za watanganyika zinauzwa,wewe dalali wa dp world unakenua meno.

hatuwezi kubali bandari yetu igaiwe kwa waarabu milele.
 
Back
Top Bottom