Kipigo cha Mwanafunzi, Watanzania acheni unafiki

Kipigo cha Mwanafunzi, Watanzania acheni unafiki

Ndugu Oscar Pius umenitoa chozi!!!umeandika jambo ambalo kwa mwelewa ukitoa siasa atalifikiria kwa kina na kutumia upeo kuliko mihemko ya jamii!!
Tukio hili la kupigwa mwanafunzi ni kila sehemu linajadiliwa!!Upande gari au vijiweni ni mjadala wa walimu hawa!!walimu wanaonekana kituko!heshima haipo tena!!Walimu wataheshimiwa na nani wakati serikali haiwatetea wala kuwalinda!??.anaonekana kama kibaka mtaaani!mtu asiyekuwa na maana!!!
Hivi hawa wakubwa walitokea wapi!!hivi kwa kadhia kama hiii matamko kila korna,mjadala kila sehemu mpaka BBC!!Huyu mwalimu si binadamu!?Alishushwa mbinguni!?hivi kwa hali kama hii tutakuwa na walimu wa kesho!?maana wanaonekana ni jamii ya watu wasiokuwa na maana!Inauma sana!!Walimu wamekosea kuchukua taaluma ya ualimu!???hivi wasingechukua taaluma hii kungekuwa na walimu!?Hali ngumu wanaokutana nayo ni wao wanajua!!!Mzazi ameshindwa kumlea mtoto wake then akiadhibiwa na mwalimu ni kosa!!
Tujaribu kutumia jicho la tatu kulitathimini jambo kama hili na siyo kutumia mihemko na siasa ili kutafuta sofa!!!!!
INANIUMA SANA
 
ACHA KUPIGA NA KUUA PIA IKIBIDI-KWANI VITANI HUENDA KUFANYA NINI?
Hata hujui tofauti kati ya polisi na wanajeshi? Ulishaona wapi polisi wakienda vitani? Polisi, wanajeshi na magereza wote ni askari lakini wana kazi tofauti!
 
Mazingira ya kazi kama siyo rafiki unapiga kazi chini unaendelea na ustarabu mwingine,may be kwa kuwa ualimu wenyeye niwa division iv na zero ndo maana wanalialia
Hizo ni dharau sasa kwa walimu.
Ingekuwa ni serikali ungeitwa "mchochezi"
 
Mleta mada ameonesha makosa yanayofanana, na jinsi moja lilivyoonekana ni kubwa sana na kupewa uzito kuliko jingine. Ni kweli mafunzo yao hayafanani, lakini unafikiri askari anafundishwa kupiga raia aliye chini ya ulinzi wake?

Yes kwani hua huoni mazoezi yao.
 
Hata hujui tofauti kati ya polisi na wanajeshi? Ulishaona wapi polisi wakienda vitani? Polisi, wanajeshi na magereza wote ni askari lakini wana kazi tofauti!
WEWE UTAKUWA UMEZALIWA BAADA YA TETEMEKO LA KAGERA
 
Askari wamefundishwa kupiga mtuhumiwa alicheni ya ulinzi?Acha kuleta unafiki wako hapa!

Pata muda ufuatilie mafunzo ya askari kuanzia CCP then ufananishe na Mafunzo ya Ualimu vyuoni. Walimu wanafundishwa psychology, pia namna ya kudili na wanafunzi mbalimbali wakorofi, wapole nk. Child Development and psychology nk ni baadhi ya masomo wanayosoma walimu vyuoni. Polisi wanafundishwa namna ya kudili na watu wakorofi kwa kutumia nguvu nk
 
Mimi nilinusurika kichapo nikiwa na wiki tatu toka niajiriwe 2013 toka siku hiyo sikuwahi gusa mwanafunzi kwa tatizo LA nidhamu mpaka mwaka Jana mwishoni nilipoamua kuachana na ualimu.
 
WEWE UTAKUWA UMEZALIWA BAADA YA TETEMEKO LA KAGERA
Ndio ujue kwamba mimi sio wa kawaida kama wewe. Ndani ya miezi isiyozidi miwili tangu kuzaliwa ninajua kuandika na kusoma! Wewe hujui hata tofauti ya polisi na mwanajeshi!
 
Point unayo mkuu. Kwa kuongezea: "Kipigo cha Dr. Ulimboka ndani ya nchi hii ambayo ni kisiwa cha amani."

Hivi hili la walimu ni kubwa kuliko matukio
mengine nchini? Ukitaka kujua kunya anye kuku akinya bata kaharisha basi chukua tukio hili linalovuma sasa nchini kuhusu walimu mafunzoni waliomuadhibu mwanafunzi huko mbeya.

Kila mtu anasema lake kila raia anasema lake
kisa kuna jina mwalimu, nauona ukandamizaji na udhalilishaji, hili si kubwa kuliko mengine
yaliyopo na yaliowai kuwapo nchini..

Leo media ndio mjadala, nimeamka asubuhi
mada ni hii redioni, kwenye tv, magazeti na hukowhasapp na kwingineko ndio usiseme.
Hivi waandishi wa habari mna weledi kweli?

Hivi Kipigo cha mtoto ambae hata hajajeruiwa ni kikubwa kuliko watafiti waliouwa Dodoma?
Ni kikubwa kuliko Kifo cha Mwangosi mikononi
mwa Polisi?
Mbona mijadala haikufika hapa, wala
hatukumuona mawaziri watatu mpaka wanne
wakisimama ndani ya masaa machache baada
ya uvumi/tukio kutoa matamko na hukumu kwa
watuhumiwa?

Hivi hili limewauma sana serikali kuliko
mengine? Kwanini haikuwa busara liende kwa taratibu za kisheria mpaka mahakamani walimu hawa waliokuwa mafunzoni wapewe haki yao na chombo cha kutoa haki?

Siwezi sema walichotenda walimu hawa ni sawa lakini je hatua za hukumu pia zipo sawa?
Tunasikia hadi vyuo wameshafukuzwa, je hii ni
hukumu ya haki?

Mbona scorpion aliemtoa mtu macho sijasikia
hata waziri mmoja akisema auwawe? Au
alichofanya scorpion, wale wanakijiji wa dodoma kuwauwa watafiti ni zuri kuliko hili?

Watanzania tuache mihemuko, na ndio maana
nchi hii ina wanafiki wengi, wasioweza kuhoji
wala kuchanganua wapo kumfurahisha fulani
wapate vyeo, fulani nae yupo kutoa tuzo kwa
kila mnafiki.
Lazima ifike wakati tuishi ndani ya haki na
kweli.

Wengine wanasema yani katoto kadogo vile
walimu watano? Mbona hamuulizi yani vi walimu viwili tu vilivyopo mafunzoni mawaziri watatu na
waandishi wa habari wote wamesimama? Na
wakiungwa mkono na Watanzania kibao

Hali halisi zilizopo Mashuleni:
Wengi hamjui hali halisi zilizopo mashuleni,
walimu wenzangu wanajua sana tena vema hali
halisi mashuleni, na hali mbaya ya utovu wa
nidhamu mashuleni, ambayo imeletwa na serikali ya kuchanganya siasa na taaluma.

Wanafunzi wanajua wana haki kubwa sana
mashuleni kuliko walimu, kama hamjui mlijue
hilo, siku hizi watoto hawafukuzwi mashuleni
maana siasa za wanasiasa na sera za serikali
zinasema watoto wabembelezwe wamalize
shule.

Ndio maana michujo na mitihani kama ya kidato cha pili haipo, lengo ni amalize shule hayo mengine si ya muhimu kabisa kabisa
Viboko na adhabu za kawaida ni haramu shuleni,

serikali haina msimamo thabiti, waraka wa
adhabu uliopo hauna mwanya wa kutoa adhabu
za maonyo kwa wanafunzi, leo linatokea hili
nchi inasimama, kweli?

Nitoe mifano halisi mwaka jana kuna walimu
walikuja mafunzoni shule nnayofundisha,
wanafunzi wawili wakamshika matiti mwalimu
wa kike alipokuwa darasani, mwalimu
alifadhaika sana. Tukatoa adhabu kwa hawa
watoto ya suspension (kurudishwa nyumbani) na viboko vinne kila mmoja.

Usiku ule ule wakamvizia mwalimu mwingine wa kiume alie mafunzoni alieonesha kuguswa na tukio wakampiga mawe na akapasuliwa juu ya jicho.

Hivi katika mazingira haya unafanya nini? Nani
ana wajibu wa kumlinda mwalimu dhidi ya
watoto na jamii iliooza? Sisemi wanastahili
kipigo kiasi kile ila nataka kila anaesoma hapa
achukue nafasi ya Mwalimu. Na ajiulize kama
yeye ni mwalimu angejiteteaje na wapi?

Sisi tunakutana na mengi msioyajua, watoto
hawa ni wala bange, anakuja shuleni asubuhi
kala bangi, kanywa viroba na anakuona
mnalingana, huwezi kumwambia kitu, unaweza
kuwa unafundisha yupo bize na kipenzi chake
wanafanya yanayowapendeza, ukichukua hatua
hata ya kupeleka ofisi ya nidhamu basi wewe ni
mnoko bifu zinahamia mtaani/kijijini mnakoishi.

Na kadri mtoto mmoja anapoharibikiwa na shule inashindwa kumfukuza (kwasababu ya Siasa)
wanaiga waliopo nyuma yake. Tunaishi katika
vijiji na miji ambapo walimu ni adui namba moja wa jamii kama tu mwalimu huyo ataonekana ana deal na nidhamu vema. Hata kesi utazushiwa za uongo.

Nitoe mfano mwingine, wiki tatu zilizopita
nilikuwa na adhibu watoto waliochelewa namba
nikiwa zamu, nilipofika kidato cha nne niliadhibu wote isipokuwa mtoto mmoja nilipomfikia akasema sitaki, mie huwa sichapwi, nikatoka nje lakini nimefedheheshwa sana.

Chukua nafasi yangu alafu uamue, ukimwangalia ni mtoto wa kumzaa kabisa ama mdogo wako wa mwisho, vipi ukiwa na hasira katika mazingira kama hayo?

Ndio maana nasema watanzania tunakurupuka
na kuongea bila kutazama pande zote hili
hukumu ya haki ipite.

Walimu wanastahili haki yao lakini pia ni wakati
walimu walindwe dhidi ya watoto wakorofi ama
serikali iweke mazingira ya adhabu na watoto
walioshindikana.

Wapo walimu waliokwisha zira kabisa wao
wame declare kufundisha tu hata mtoto apande
juu ya bati hawatamgusa kwakuwa mtoto
analindwa kuliko mwalimu, hivi mtoto
aliekushika matiti utaendelea kufundisha akiwa
hapo shuleni?

Yapo mengi siwezi kuandika yote ila walimu
wanajua vema sana mambo haya, wanajua
kadhia zinazowakabiri usiku na mchana, kupigwa mawe mitaani, kurushiwa mayai viza, kuzushiwakesi vijijini kwakuwa tu anachukua hatua za nidhamu haya watu hawayaoni,

Mnaona tu kilichomkuta mtoto ambae hata hajalazwa hospitali.
Kesi za mimba hasifiki mbali kwakuwa walimu
uamua kuachana nazo, maana jamii
inakubaliana wanayamaliza na mwalimu
unaefatilia utakiona cha moto.

Ninyi watanzania huko mitaani, bar, na makazini kwenu hamshikani mashati kwa hasira za ubinadamu? Mbona kwa walimu owe kioja?

Hivi la walimu ni dhambi kuliko la Scorpion
alietoa macho watu na hakupewa hukumu ya
hapohapo kafikishwa kwenye vyombo vya
sheria?
Mwalimu ni mwanadamu kama walivyo wengine wote.

Ukweli utasimama daima.
Mzalendo wa demokrasia
 
Hakika nimeamini Tanzania inaongoza kwa Unafiki Duniani na Mbinguni. Siungi mkono tukio la yule mwanafunzi wa Mbeya kula kichapo lakini nashangazwa sana na matamko yasiyoisha.
Kinachoonekana pale ni unyanyasaji wa kijana mwanafunzi akipokea adhabu kali kuliko kawaida.
Kama ni hivyo je, ni mara ya kwanza kuziona adhabu kama hizo zikitolewa?
Nimeweka hapa vidio ya askari wetu wakitoa kipigo kitakatifu kwa shabiki wa UKAWA. Kama walimu walivyomchangia kijana yule ndivyo askari kama watano hivi wakimhangia kijana asiye na silaha yeyote. Amekula mateke na virungu vya haya? Hakuna taasisi hata moja ya serikali imewahi kukemea askari kwa upiganji huu. Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa kimya.
Kama ambavyo walimu wamesitishiwa mikopo kwa nini askari hawa hawakufukuzwa kazi?

ACHENI UNAFIKI WATANZANIA WENZANGU

Wewe ndiyo mnafiki hhuyo anapigwa na polisi alipewa onyo kwamba nguvu ya dola itatumika kumlazimisha atii sheria iliyopo na kinachofanyika pale ni mapato ya ukaidi wake kwa dola.
Kuhusu mwanafunzi kuna sheria inayomzuia mwalimu kutoa kipgo kama kile yule mtoto alisema anaumwa na wale walimu wako pale kama wazazi na ndiyo maana hata wazazi wanaopitilizA Vipigo kwa watoto wao na pia hushitakiwa. Polisi anayo mamlaka siyo ya kukupiga bali pia kukutoa roho bila kushitakiwa Mwalimu hana idhini hiyo na kipigo alichokuwa akitoa cha ngumi hakuambiwa mwanafunzi ampige ngumi na yeye akapiga ngumi ni upumbavu kulinganisha tatizo la wale walimu wanafunzi na polisi wakiwa kazini. Wauwaji wa dodoma mbona serikali imeshawashughulikia kama huamini nenda kamsalimie yule mjomba wako pale kijijini atakuambia kuna serikali Tanzania au hakuna. Ngumi alizopigwa yule mtoto ndiyo unafananisha kipigo cha huyo mwenda wazimu aliyekaidi amri ya polisi???? APIGWE TU TUMIA AKILI NA SIYO KUTUITA WATANZANIA WOTE NI WANAFIKI
 
Point unayo mkuu. Kwa kuongezea: "Kipigo cha Dr. Ulimboka ndani ya nchi hii ambayo ni kisiwa cha amani."

YULE ALIPIGWA KUMALIZA MGOMO WA MADAKTARI BAADA YA HAPO NANI ALIGOMA TENA VITU VINGINE HAVIHITAJI DEGREE KUJUA KAA KIMYA.
 
Hivi najiuliza ingekuwa yule dogo yupo JKT then akaonesha utovu ule wa nidhamu kumkwida afande kingetokea nini. Mimi sioni walimu mnacholalamika wakati mmerahisishiwa kazi, kwani kutoa adhabu kwa toto lisilotaka shule kuna allowance? Mwanafunzi asipoandika inabatilisha degree/diploma yako? Mwanafunzi akikosa nidhamu mshahara hauingii? Japo siungi mkono adhabu kama za Mbeya daya lakini kwa kilichotendeka na mrejesho hakitumi ujumbe mzuri kuhusu mahusiano ya walimu, serikali na wanajamii. Kila mwalimu sasa ni MNYAMA na hakuna anayegusia suala la nidhamu ya hawa watoto wao ambao wengi wameshindikana. Anyway JKT ipo, so suala la mafunzo ya nidhamu watalikuta huko.
 
okw-boban-sunzu, Kwa taarifa tu polisi kumpiga mwanachama wa Ukawa kivyovyote vile ni Amri halali ya Waziri Mkuu pinda ilitolewa bungeni akisema kama watu hafuati Amri PIGA. Kwa Mwanafunzi ni Makosa kwa sababu kuna code of conduct ya walimu na lazima ifuatwe. Ushauri mwambie Tundu Lisu aende mahakama kuhusu hii amri ya waziri mkuu iondolewa
 
Watu wanajaji tu vitu bila kujua tukio lile la Mbeya liliyokea kwenye mazingira ya aina gani...
Alafu hawa watoto tunavyowadekeza na kuwalea kisiasa ipo siku watakuja watuvue nguo hadharani...
 
Back
Top Bottom