nakubaliana na ww mtoa mada. kwanza niseme nalaani ukatili ulofanywa na wanafinzi wa ualimu, sijawaita walimu kwasababu bado wapo mafumzoni napengine dio maana wakatoa adhabu ambayo tunaikemea sote. Hivo tukio hili nimoja kati ya mengi wanayofanyiwa watanzania wengine. Fikiria mafisadi, madaktari wazembe wasababishao vifo, askari makatili, jkt, ukatili dhidi ya albino, na mengine mengi ya namna hii. lkn hakuna matamko mazito na mengi kutolewa kama tukio hili.
Nimeshuhudia wizara tatu zote zikishindana kutoa maelezo, wakati mafisadi wanakwapua mabilioni ya umma na kuumiza wanyonge hakuna matamko.
Leo unaamua kufukuza chuo wanafunzi wa ualimu badala badala ya adhabu mbadala, na unajiapiza hawatasoma tena!, hii si sawa. Bimafsi wangekuwa walimu kamili ilikuwa sawa kuwafuta kazi, hawa ndio maana wako mafunzo kwa vitendo hawajaiva bado wanapikwa na makosa na mapungufu lazima wawe nayo. kama taifa tulipaswa tuwarekebishe ili baadaye waje kuwa walimu wazuri.
Hivi tukio alilofanya scorpion kutoboa macho mtu mbona matamko hayakuwa mazito?, je wahanga wa tetemeko mbona mipango haikamiliki kwa uzembe wa watimishi kufanya tathimini hovyohovyo ilihari wahanga wanateseka na tathimini inarudiwarudiwa, je Mwangosi mbona wengine walipandishwa vyeo?. haya ni baadhi tu
Ushauri wangu vijana hawa walipaswa waadhibiwe na vyuo vyao kama vile kuwasimamisha masomo kwa mwaka mmoja au kufuta hiyo field mpk mwakani.
Mtizamo wangu vijana wamefanya ukatili lkn serkali pia imewahikumu kikatili mno.