Kipi ni bora - Useja au kuoa/kuolewa?

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Mar 6, 2022
2,398
2,593
*USEJA - hii ni ile hali ya mtu kuishi bila ndoa.

Swali: Kwa dunia ya Sasa na maisha ya sasa yalivyo kipi ni bora kuishi maisha ya useja au kukubali kuoa/kuolewa?

- Kwangu Mimi maisha yaliyo bora ni kuishi kwenye useja.

- Vipi kwenu nyie wanajamii majibu yenu ni yapi [ useja au kuoa/kuolewa ].
 
*USEJA - hii ni ile hali ya mtu kuishi bila ndoa.

Swali : Kwa dunia ya Sasa na maisha ya sasa yalivyo kipi ni bora kuishi maisha ya useja au kukubali kuoa/kuolewa ?

- Kwangu Mimi maisha yaliyo bora ni kuishi kwenye useja.

- Vipi kwenu nyie wanajamii majibu yenu ni yapi [ useja au kuoa/kuolewa ].
Huyu hapa Mtume Paulo akimwaga nondo za kufa mtu kuhusu hili suala.

Screenshot_20220710-121300_Swahili%20Bible%20Offline.jpg
 
Useja unachosha jumlisha upweke.
Hapa tu nishachoka upweke sasa sijui kukaa maisha yote kiseja kama nitaweza.
Mi nishajua tu kukaa kiseja siwezi ila ndio hivo sasa bahati mbaya ndoa zinanipitia kushoto.
Duuh! Pole yako
 
*USEJA - hii ni ile hali ya mtu kuishi bila ndoa.

Swali : Kwa dunia ya Sasa na maisha ya sasa yalivyo kipi ni bora kuishi maisha ya useja au kukubali kuoa/kuolewa ?

- Kwangu Mimi maisha yaliyo bora ni kuishi kwenye useja.

- Vipi kwenu nyie wanajamii majibu yenu ni yapi [ useja au kuoa/kuolewa ].
Useja ni sawa na upweke tu.... Ndoa ni bora.
 
Kikubwa tafuta kujua ni nini mapenzi ya Mungu kwako. Muombe Mungu akufunulie ni kwanini alikuleta duniani., maana hakuna mtu aliyejileta nwenyewe duniani. Tumekuja duniani kwa mapenzi ya Mungu, hivyo hatuna budi kutafuta kuyajua ili tuyaishi.

Ndoa ni kitu kizuri kwa kuwa ni Mungu mwenyewe aliyeanzisha ndoa pale kwenye bustani ya Edeni., Adui shetani ndiye aliyekuja kuharibu taasisi hii nyeti na kufanya ndoa ionekane kuwa kitu kisichofaa.

YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI
 
Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁰ Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
¹¹ Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
¹² Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
 
Itategemea na calculation za kila mtu na pia ujue unachokifata na ukubaliane nacho.
Upande wa ndoa ukipata utakaeendananae utafurahia nje na hapo utaona useja ndo dili!..
Ktk kuchagua itategemea na muhusika.
Naomba aliye hack hii ID aendelee kuitumia zaidi hongera sana.
 
Back
Top Bottom