Nzuguni one
JF-Expert Member
- Dec 23, 2019
- 1,158
- 482
Yote kwa pamoja na vzr
Unadhani tatizo ni nauli basi, sio kweli!
Ukitaka kuamini hilo, siku usafiri na mtoto halafu mlipie nauli kamili kisha tulia.
Utaona venye watu wanamtazama kwa jicho la kuitamani siti yake, wapo wataodiriki kumfokea awapishe kabla wajue kama amelipa nauli kamili.
Mzazi utaonekana unamkingia kifua mwanao na kwamba unamfunza utovu wa nidhamu, pengine itakulazimu kutoa maelezo ya kuwa ‘siti imelipiwa’ kila itapotokea kuna mwamba anajisogeza.
Ni ubinafsi tu au kutokujali watoto wetu.
Mwendokasi hazina ushenzi huo
Watoto wa mwendokasi wana enjoy maisha
Hapo unahamia kwenye upande mwingine, kuwa unathaminiwa kwa kile ulichonacho lakini jamii yetu hatuwezi kuishi kwa mambo kama hayo,Swala si heshima wala upendo
Suala ni nauli 200
Mwanafunzi akilipa nauli ya mtu mzima hakuna anayehangaika kumsimamisha!!!
Ni kweli huwa nawaonea huruma sana watoto hawa, huchoka nao kama sisi watu wazima ila mfumo wetu wa ulipaji nauli ndio unawagharimu.
Mzazi kama unaweza mpe mwanao nauli ya mtu mzima tu.
Upendo ukitangulia na hekima hufuata, burasa pia na hata heshima.. Upendo ni muhimili mkubwa sana unaojitegemea, vingine vinategemeana,Ndugu zangu!
Nipo kwenye usafiri wa umma almaarufu daladala. Basi kuna watoto, ngoja niite wanafunzi kwa mujibu wa nauli yao lakini hawajavaa sare za shule. Miaka 8-10 hivi.
Basi, gari halijajaa vema kuna viti kadhaa konda anaendelea kuita abiria. Mara gari likaanza kuchapa mwendo huku wale watoto wamesimama japo viti vipo wazi.
Hakuna anayeshangaa, hata kwangu sio jambo geni. Ila imenipa muda wa kuwaza kidogo.
Hivi, hii tabia ya kuwainua watoto wasikae ina misingi gani?
Kama ni heshima, tunadhani ni kwa ridhaa ya mtoto au tunamlazimisha atuheshimu?
Ikumbukwe mtoto yupo kwenye umri wa kujifunza, mfano huyo mwanafunzi. Anahitaji zaidi kuoneshwa upendo ili ajisikie faraja, mfano hapo anatoka shule kama ni kuchoka naye amechoka vile vile.
Hii kwa wengi imekuwa kawaida na hakuna anayejali, hata ikitokea amekaa atafurumushwa na konda na abiria watamshangaa mtoto kakosa adabu!
Hii imekaaje?
Tunataka kupewa heshima, tunasahau yatupasa kuonesha upendo... ukisimama mtoto akae hupungukiwi na kitu.
Kipi muhimu, kipi kianze? Kwangu upendo kwanza, kwako Je!
Wasalaam,
Ncha Kali.
Hapo hujamjibu sawia,Tafuta hela kaka![]()
Mtoto mdogo kistaarabu kabisa unatakiwa upishe kiti mkubwa wako akae, umri unavyoenda nguvu pia hupungua sasa kwa kijana mwenye nguvu kabisa unaweza simama hata masaa matatu bila kuchoka unaweka ligi ni mtu mzima kweli? Upendo ndiyo kila kitu.
Ni mitazamo isiyo na upendo kabisa, kuwa na hela haiwezi ikakunyima kuwa na upendo, hata kama unalipa laki moja kwenye siti ila kama una upendo unaweza ukampisha mtu mzima ukamwambia akae, utapungukiwa nini hasa?Kuna wakati huwa natembea na mwanangu tena ana 4yrs namlipia nauli hakuna anayehoji, labda akitaka kukaa ataomba ambebe!!!.
Zamani ndio tulikuwa tunasema kwaajili ya heshima lakini sasa kitu ni nauli bwana.
Wapo wanafunzi wanalipa ya mtu mzima wala hawasimamishwi....wala konda hahoji apishe mzima.
Ila wanawake sishangai hii kitu ni hulka yenu kabisa kwa baadhi yenu,Dereva huwa anatangaza wanafunzi pisheni wakubwa wakae.


Hapo hujamjibu sawia,
Hela ndiyo inaweza kukufanya ukaishi maisha mazuri lakini ni vitu vya muda tu kuna wakati unaweza ukawa nazo na wakati mwingine usiwe nazo,
Ila sasa upendo ni dawa upendo ni nguzo ya mambo yote, ukiwa na upendo kila kitu duniani kitakua chako, utaheshimika, utapendwa utabarikiwa, utaisha maisha ya furaha hata kama mfukoni huna kitu,
Tujifunze sana kuthaminisha utu kuliko mali za duniani, kwanza mali za duniani ni mali ya bwana
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila wanawake sishangai hii kitu ni hulka yenu kabisa kwa baadhi yenu,
wewe uliokaa unaweza ukamuona mwanamke mwanzako ambae ni mjauzito kasimama tena tumbo kubwa na anasimama kwa shida kabisa kwenye daladala huwa hata hampishi, ni mpaka wanaume unakuta tunanyanyuka na kumpa nafasi/kiti, sijui mpoje nyie watu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo unahamia kwenye upande mwingine, kuwa unathaminiwa kwa kile ulichonacho lakini jamii yetu hatuwezi kuishi kwa mambo kama hayo,
Mtoto mdogo kistaarabu kabisa unatakiwa upishe kiti mkubwa wako akae, umri unavyoenda nguvu pia hupungua sasa kwa kijana mwenye nguvu kabisa unaweza simama hata masaa matatu bila kuchoka unaweka ligi ni mtu mzima kweli? Upendo ndiyo kila kitu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mitazamo isiyo na upendo kabisa, kuwa na hela haiwezi ikakunyima kuwa na upendo, hata kama unalipa laki moja kwenye siti ila kama una upendo unaweza ukampisha mtu mzima ukamwambia akae, utapungukiwa nini hasa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Upendo upo kwa kumpisha mtu mzima tu?
Hoja ya mtoa mada je hawa watoto hawapaswi kupendwa kwa kuachiwa viti wakae na mkubwa asimame?
Upendo huu bongo hiii....tunaopigana vikumbo kugombea siti? Au foleni?
Tena nyie wanaume ndio kabisaa utakuta unawapush wanawake bila kujali....au utaona wenzio wako kwenye foleni ila utapitiliza mbele...!!!
Upendo bado sana TZ yetu.
Weeeee Englishfigure, hebu ngoja kwanzaKila jambo hutazamiwa kwa namna yake, hapo umesema wanawake sasa mwanamke yupi unamzungumiza hapo, je ni wa miaka 18Upendo upo kwa kumpisha mtu mzima tu?
Hoja ya mtoa mada je hawa watoto hawapaswi kupendwa kwa kuachiwa viti wakae na mkubwa asimame?
Upendo huu bongo hiii....tunaopigana vikumbo kugombea siti? Au foleni?
Tena nyie wanaume ndio kabisaa utakuta unawapush wanawake bila kujali....au utaona wenzio wako kwenye foleni ila utapitiliza mbele...!!!
Upendo bado sana TZ yetu.