Kipi kitangulie, heshima au upendo?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
15,019
28,182
Ndugu zangu!

Nipo kwenye usafiri wa umma almaarufu daladala. Basi kuna watoto, ngoja niite wanafunzi kwa mujibu wa nauli yao lakini hawajavaa sare za shule. Miaka 8-10 hivi.

Basi, gari halijajaa vema kuna viti kadhaa konda anaendelea kuita abiria. Mara gari likaanza kuchapa mwendo huku wale watoto wamesimama japo viti vipo wazi.

Hakuna anayeshangaa, hata kwangu sio jambo geni. Ila imenipa muda wa kuwaza kidogo.

Hivi, hii tabia ya kuwainua watoto wasikae ina misingi gani?

Kama ni heshima, tunadhani ni kwa ridhaa ya mtoto au tunamlazimisha atuheshimu?

Ikumbukwe mtoto yupo kwenye umri wa kujifunza, mfano huyo mwanafunzi. Anahitaji zaidi kuoneshwa upendo ili ajisikie faraja, mfano hapo anatoka shule kama ni kuchoka naye amechoka vile vile.

Hii kwa wengi imekuwa kawaida na hakuna anayejali, hata ikitokea amekaa atafurumushwa na konda na abiria watamshangaa mtoto kakosa adabu!

Hii imekaaje?

Tunataka kupewa heshima, tunasahau yatupasa kuonesha upendo... ukisimama mtoto akae hupungukiwi na kitu.

Kipi muhimu, kipi kianze? Kwangu upendo kwanza, kwako Je!

Wasalaam,

Ncha Kali.
 
Swala si heshima wala upendo

Suala ni nauli 200

Mwanafunzi akilipa nauli ya mtu mzima hakuna anayehangaika kumsimamisha!!!

Ni kweli huwa nawaonea huruma sana watoto hawa, huchoka nao kama sisi watu wazima ila mfumo wetu wa ulipaji nauli ndio unawagharimu.

Mzazi kama unaweza mpe mwanao nauli ya mtu mzima tu.
 
Ni huu mfumo wetu ndio unaoleta yote haya,japo walikuwa na lengo zuri lakini njia iliyotumika imekuwa ni kama mateso kwa hao wanafunzi.

Yaani mwanafunzi ndiye wa kusubiri mpaka gari ijae ndio apande, na kusimama pasi na kujali umbali wa safari.

Bora ingelikuwa nauli ni moja tu halafu suala la kusimama libaki kuwa maamuzi binafsi.
 
Swala si heshima wala upendo

Suala ni nauli 200

Mwanafunzi akilipa nauli ya mtu mzima hakuna anayehangaika kumsimamisha!!!

Ni kweli huwa nawaonea huruma sana watoto hawa, huchoka nao kama sisi watu wazima ila mfumo wetu wa ulipaji nauli ndio unawagharimu.

Mzazi kama unaweza mpe mwanao nauli ya mtu mzima tu.

Unadhani tatizo ni nauli basi, sio kweli!

Ukitaka kuamini hilo, siku usafiri na mtoto halafu mlipie nauli kamili kisha tulia.

Utaona venye watu wanamtazama kwa jicho la kuitamani siti yake, wapo wataodiriki kumfokea awapishe kabla wajue kama amelipa nauli kamili.

Mzazi utaonekana unamkingia kifua mwanao na kwamba unamfunza utovu wa nidhamu, pengine itakulazimu kutoa maelezo ya kuwa ‘siti imelipiwa’ kila itapotokea kuna mwamba anajisogeza.

Ni ubinafsi tu au kutokujali watoto wetu.
 
Mtoto asimame mkubwa akae, mkubwa ale chakula kizuri, mtoto kinachobaki, kwangu haipo hiyo mtoto akipanda dala dala anakaa, na hamna atakaeyemuinua wala kumbeba, na pia kabla ya watu wote kuanza kula/kupakuwa nyumbani kwangu wanaanza watoto, choxhote kinachofanyika na kuhusisha watoto basi ni watoto kwanza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom