Kipi kitangulie, heshima au upendo?

Kipi kitangulie, heshima au upendo?

Ila wanafunzi hasa wa dar wanapata tabu sana maana baadhi yao wanaingia kwenye daladala muda ambao wenzao wa mikoani wanaamka
 
Unadhani tatizo ni nauli basi, sio kweli!

Ukitaka kuamini hilo, siku usafiri na mtoto halafu mlipie nauli kamili kisha tulia.

Utaona venye watu wanamtazama kwa jicho la kuitamani siti yake, wapo wataodiriki kumfokea awapishe kabla wajue kama amelipa nauli kamili.

Mzazi utaonekana unamkingia kifua mwanao na kwamba unamfunza utovu wa nidhamu, pengine itakulazimu kutoa maelezo ya kuwa ‘siti imelipiwa’ kila itapotokea kuna mwamba anajisogeza.

Ni ubinafsi tu au kutokujali watoto wetu.
kuna siku nilipanda daladala na mwanafunzi kachoka hadi anasinzia ila mtu mzima ambaye yupo fit akataka apishwe. Kiukweli nilimlipia nauli ya mtu mzima maana hiyo hali hata mimi naielewa haswa kwa shule zetu za kidumu na mfagio

ila kama unavyosema watu waliniangalia kwa jicho baya na minong'ono ila sikujali
 
Jamii inaliona tofauti, hata akilipa nauli itatafsiriwa kuwa ana jeuri tu!
 
Jamii inaliona tofauti, hata akilipa nauli itatafsiriwa kuwa ana jeuri tu!
unajua vitu vingine inatokana na malezi, tumeshaaminishwa hivyo hata mgeni ambaye ni mtu mzima akifika sebuleni utakuta watoto wote mnampisha ili aongee na wazazi

Ukikuta mtu mzima anafanya kazi hata kama umechoka itabidi umsaidie tu ili ujenge heshima ya familia yako kuwa wana malezi mazuri. ni muendelezo tu huo
 
Ni bora hiyo ya kuwapisha wakubwa ili wazungumze, kuna ile viti havitoshi nyumbani... hili mzazi ndo inabidi akae chini ni uzembe wake.
 
Ndugu zangu!

Nipo kwenye usafiri wa umma almaarufu daladala. Basi kuna watoto, ngoja niite wanafunzi kwa mujibu wa nauli yao lakini hawajavaa sare za shule. Miaka 8-10 hivi.

Basi, gari halijajaa vema kuna viti kadhaa konda anaendelea kuita abiria. Mara gari likaanza kuchapa mwendo huku wale watoto wamesimama japo viti vipo wazi.

Hakuna anayeshangaa, hata kwangu sio jambo geni. Ila imenipa muda wa kuwaza kidogo.

Hivi, hii tabia ya kuwainua watoto wasikae ina misingi gani?

Kama ni heshima, tunadhani ni kwa ridhaa ya mtoto au tunamlazimisha atuheshimu?

Ikumbukwe mtoto yupo kwenye umri wa kujifunza, mfano huyo mwanafunzi. Anahitaji zaidi kuoneshwa upendo ili ajisikie faraja, mfano hapo anatoka shule kama ni kuchoka naye amechoka vile vile.

Hii kwa wengi imekuwa kawaida na hakuna anayejali, hata ikitokea amekaa atafurumushwa na konda na abiria watamshangaa mtoto kakosa adabu!

Hii imekaaje?

Tunataka kupewa heshima, tunasahau yatupasa kuonesha upendo... ukisimama mtoto akae hupungukiwi na kitu.

Kipi muhimu, kipi kianze? Kwangu upendo kwanza, kwako Je!

Wasalaam,

Ncha Kali.
Una bei gani kwenye account?
 
Nimekumbuka enzi zangu nasoma nilikuwa nalipa nauli ya mtu mzima..kupisha mkubwa nipende na si lazima...ingawa katika Jamii yetu tulivyojizoesha utaonekana huna heshima
 
Ni nani huyo, ni mwanafunzi amekosa siti!!
Risiti ilitoka ila daaah jirani akiwasha taa wakati umeacha sabuni kwenye beseni si vizuri Njodo nilimwita ila sikumbuki aliyemtuma mheshimiwa Lugola ni nani kwa kua Wizara imeshatoa muongozo kuhusu vyandarua!
 
Viroba vilipigwa marufuku, serikali sio wajinga... sijui unavipata wapi!

Jiepushe navyo kwa ustawi wa afya yako.
 
Viroba vilipigwa marufuku, serikali sio wajinga... sijui unavipata wapi!

Jiepushe navyo kwa ustawi wa afya yako.
IMG-20190822-WA0087.jpg
 
Ni bora hiyo ya kuwapisha wakubwa ili wazungumze, kuna ile viti havitoshi nyumbani... hili mzazi ndo inabidi akae chini ni uzembe wake.
ndio ujamaa huo brother na mtu unajifunza kutokuwa mbinafsi ila mkarimu. Si unazijua familia zetu hizi hata vyombo vya udongo vinatumika akija mgeni
 
Back
Top Bottom