Kipi kinakupa Sababu ya kuoa?

Kipi kinakupa Sababu ya kuoa?

Kuna jamaa alikua na ile "mentality" ya mimi sioi nawatia mimba tu nakua na watoto, kweli bhna alitia mimba wanawake watatu, kwahyo akawa na watoto 3 kila mmoja na mama yake. Akawa anatoa mahitaji fresh kote, sasa kama mnavyojua wanawake hua wanachukulia mtoto kama "Collateral" ili kupiga pesa kwa baba mtoto hasa kama haishi nae, leo huyu mara mtoto anaumwa mara yule hela ya nguo mara huku chakula kimeisha jamaa kuja kupiga hesabu pesa kibao zinaenda kwa hao wanawake mpk anakopa.

Akaanza kupiga chenga kutoa hela za matumizi, kilichokuja kutokea wale wanawake sijui waliambiana au vipi walikuja kumbwagia watoto wote mshkaji na jamaa alikua anaishi single room kisela tu na mbaya zaidi wazazi wake wako mbali na lile eneo hana ndugu yoyote. Ndugu wako Mara yeye anapiga kazi zake Mbeya. Akawa anawaacha kwa jirani ye anaenda kazini, nae jirani alishindwa maana alikua anampiga hela balaa, jamaa ilibidi aache kazi na ilifika kipindi alisepa kwao na maisha yalikua magumu sana.

Nadhani somo lilieleweka, tusjwachukulie poa hawa wanawake, siku yakija kukukuta kama ya mshkaji ndio utaona dunia ikoje. Kama hutaki kuoa, usizalishe mabinti wa watu. Kausha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom