Sababu ya kutokuona matunda ya Kumwamini Yesu

Sababu ya kutokuona matunda ya Kumwamini Yesu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,232
Reaction score
1,741
Mk 4:18-19 SUV
[18] Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, [19] na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai.

Kila mmoja aliyemwamini Yesu Kristo anatamani kuona matunda ya kimwili na kiroho ya kuokoka kwake au ya kuamini kwake.

Tuna mtazamo mingi hapa, wapo wanafikiri ukishaokoka au ukisema wewe ni mkristo basi unakuwa na maisha fulani magumu na yasiyo na mwelekeo wowote.

Kile tunatamani kukiona kwenye maisha yetu baadhi yetu tunaweza tusikione kama tulivyosikia au tulivyoambiwa au tulivyosoma kwenye biblia.

Wengine wanaweza wakawa na mafanikio makubwa kimwili na kiroho, ukimwangalia kwa macho ya mwili unaona kabisa amependelewa na Mungu kuliko waamini wengine kutokana na mafanikio makubwa aliyonayo.

Kipi kinatutofautisha waamini? Sababu zipo nyingi ila kwa mujibu wa maandiko ni wale watu wanaolisikia neno, wakaliamini, na kulitendea kazi au kuliishi kama walivyolipokea.

Tunapishania hapa, wapo tunasikia neno na kuliacha hapo hapo, wapo wanalisikia neno na kulifanya la kwao na kuliishi, hapo utaanza kuona ndani ya kundi moja yanagawanyika makundi mawili tofauti.

Unaweza ukawa umekariri maandiko mengi sana yasiwe na matunda yeyote kwenye maisha yako, ishu sio umekariri maandiko mangapi, ishu unaliishi hilo neno?

Neno linamtengeneza mtu sahihi, linaunda tabia mpya ndani ya mtu, linamfanya mwamini awe na imani ndani yake, anaweza kufanya mambo ambayo hayapo kwenye historia ya ukoo wake, na hakuna aliyewahi kufikiri ataweza hilo.

Ikiwa tu huyu mwamini atalisikia, kulisoma, kuliamini neno, na kulifanyia kazi katika maisha yake atapokea mabadiliko mapya.

Mk 4:20 SUV
[20] Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia.

Umeanza kuona tunatofautiana wapi waamini? Mwenye mafanikio ndani ya wokovu na asiye na mafanikio? Na aliye ndani ya ukristo ila anaenda kutafuta msaada kwa miungu mingine?

Mafanikio ninayoyazungumza hapa ni ya pande mbili, yaani kimwili na kiroho, mtu anaweza akawa amefanikiwa upande mmoja na mwingine akawa vibaya, hii inategemeana na vile anamtazama Mungu katika maisha yake.

Tunapaswa kuliamini neno kwa usahihi, kulichukua na kulitendea kazi katika maisha yetu, tuliishi kama linavyotuelekeza, tuwe na uhakika tutakuwa waamini wenye matunda mema kwenye utumishi na maisha yetu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Kama wewe ni mchungaji Hongera Ila kama ni muumini pole sana.
 
Kama wewe ni mchungaji Hongera Ila kama ni muumini pole sana.
 
Yos 1:8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom