Kipi bora... Kuweka pesa Bank au kuwekeza kwenye viwanja

bank ukiweka 1m ukikaa mwaka utakuta laki 8 makato kila mwezi!viwanja mkuu hata magari hayana maana

bank hazina faida katika kutunza fedha kwa muda mrefu coz kuna gharama za uduma nyingi mno kama kuangalia salio,kutuma pesa,makato ya mwezi ,huduma za malipo kama luku n.k.
Hivyo basi ukiweka Tsh. 100000 baada ya mwezi mmoja utakuta pungufu ya 100000 hivyo nakubaliana na kuhifadhi pesa kwa kununua ardhi coz haiozi,kupotea wala kuhamishika na thamani yake inapanda kila kukicha.
 
Nimesoma comments za wadau hapa lakini bado swali moja la msingi sijaona linajadiliwa. Wewe ni mfanyabiashara? Na ni mfanyabiashara kwenye sector gani, land?

Cardinala rule number one kwenye biashara ni liquidity. Investment utakazokuwa nazo basi ni vema utilie maanani 'liquidity'. Ardhi zinapanda bei, but how long it takes turn land into cash kama uko kwenye biashara? And can that business wait mpaka uuze hiyo land na ku-inject cash?

Cardinal rule number 2, dont put all your eggs in a single basket. Ardhi zinapanda bei, vipi kama haikupanda kama ulivyotarajia? diversify your investment vinginevyo unaweza kujikuta unakula hasara.
 
Kitu ambacho ni bora zaidi ni kuwekeza fedha zako katika sehemu ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji. Na sehemu hiyo si nyingine isipokuwa ni Mbinguni alipo MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
 
Nadhani hapa tumefanya kosa ku-equate mambo mawili tofauti.., Kununua ardhi ni uwekezaji (investment) wakati kuweka pesa bank ni akiba (savings) hivyo basi ni bora kuhakikisha at any given time pesa zako zinafanya kazi (yaani shilingi inazaa thumuni n.k.) kuliko pesa kukaa bila kufanya kazi..

Lakini mtu inabidi uwe na cash at any given time (au kitu ambacho liquidity yake ni rahisi) kwa ajili ya matatizo madogo madogo, kama kufiwa shida za hapa na pale kuugua au kununua kitu haraka haraka (investment nyinigine n.k.) Pia kumbuka kwamba the higher the risk the higher the return na never put all your eggs in one basket.., ndio ardhi huwa inaongezeka thamani daily ila inaweza kutokea tsunami au some environmental catastrophe ambayo ikapelekea ardhi yake kuwa untainable au haina faida. Hivyo basi kujibu swali ni bora pesa yako kuinvest na sio kuiweka tu ila ukishainvest yale mabaki (percent ndogo sana) jiwekee akiba ili kuweza kutumia hio pesa kama ikitokea tafrani ya aina yoyote.., na kuna guarantee kubwa ingawa inflation na kadhalika itafanya pesa yako kushuka baada ya muda ila ni vigumu kuwa wiped out.., na kuweka hii akiba simaanishi kuiweka yote kwenye fixed deposit naamanisha kuweka tu na kuwa unatoa kwa matumizi
 
Kitu ambacho ni bora zaidi ni kuwekeza fedha zako katika sehemu ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji. Na sehemu hiyo si nyingine isipokuwa ni Mbinguni alipo MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
Ya Kaizari mwachie Kaizari
 
Heshima kwenu wakuu wangu.

Wakuu naombeni maoni yenu.

Kwa mfano mtu una pesa ambazo utahitaji kuzifanyia jambo fulani miaka mitano ijayo.
Kwa kawaida watu huifadhi pesa bank ila nimefikiria nikaona kwamba say una 50,000 leo,ukiziweka bank baada ya miaka mitano hata kama zitaongezeka,zitaongezeka kidogo sana.

Pia baada ya miaka mitano kitu ambacho unaweza kukifanya kwa 50,000 leo hutaweza kukifanya kwa pesa hizo hizo miaka mitano ijayo,namaanisha thamani ya pesa yetu inapungua kwa kasi sana.

Je badala ya kuziweka 50,000 zangu bank niamue kununua viwanja katika maeneo ambayo najua wakati wowote naweza kuviuza viwanja hivyo na kupata pesa zangu.

Nimeona faida ya kuziweka pesa zangu kwenye viwanja itakua ni;
Bei ya ardhi inapanda kila siku,kama leo nitanunua kiwanja kwa elfu ishirini kwa mfano,miaka mitano ijayo naweza nikakiuza kwa elfu thelathini na tano au zaidi.

Pia nitauza kiwanja kulingana na thamani ya pesa ilivyo katika miaka hiyo.

Haya ni mawazo yangu tu ila sina utaalamu katika haya ninayofikiria,hivyo ningeomba mnaojua kwa uhakika mambo haya mniambie kama mawazo yangu ni sahihi au ninakosea.

Natanguliza shukrani.

Viwanja hivyo usipoviendeleza kisha vikachukuliwa nini kitatokea?
 
Nimevutiwa sana na hoja yako pamoja na michango iliyotolewa. Na mimi nimeona nitoe mchango wangu wa mawazo. Nadhani uliposema kuweka pesa benki ulimaanisha kuweka kwenye akaunti ya muda maalamu kwa kiingereza huitwa ' Fixed Deposit Account". Hiyo ni investment na ina faida zifuatazo:

1. Haina risk- Yaani ni risk free investment. Ukiiweka na ukakubaliana na benki juu ya riba yako basi mwisho wa huo muda wewe utarejeshewa pesa yako pamoja na riba yake.

2. Haumizi kichwa yaani kufanya business management. It is a do nothing investment.

Hasara zake

1. Mabenki yanatoa riba ndogo ambayo haiendani na kiwango cha mfumuko wa bei. Wakati mfumuko wa bei waweza kuwa 25% benki itakupa riba ya 6%.

VIWANJA
Kwa kawaida ardhi uwa inapanda thamani.

Faida
1. Waweza kuuza kiwanja hata mara tatu ya bei uliyonunulia

Lakini kwa Tanzania viwanja vina risk zake nazo ni:

1. Waweza nunua kiwanja kumbe kina mgogoro na ukajikuta muda wote wa uwekezaji wako wewe upo mahakamani as a bonafide buyer lakini hauna ruhusa ya kuuza mpaka kesi iishe.

2. Waweza tapeliwa

3.Serikali yaweza pata mwekezeji na ukashindwa hata kukiuuza maana hakuna a knowlegeable buyer atakubali kuingizwa mjini

4. Waweza nunua kwa bei kubwa lakini kiwanja kikashuka thamani. Sasa hapa utajiuliza inakuwaje kiwanja kishuke thamani? Ndiyo kiwanja chaweza shuka thamani. Chukulia mfano sheria ya ardhi Tanzania ni kwamba eneo la makazi unapewa right of occupancy ya miaka 33. Na wewe wakati unanunua tayari eneo hilo lilikuwa na miaka 25 toka hati hiyo itolewe. Baada ya miaka 5 eneo hilo litakuwa limetimiza miaka 30 na hivyo bado miaka 3 tu. Mnunuzi mjuzi hawezi nunua eneo hilo. Tunasema ardhi inapanda thamani lakini kwa sheria ya ardhi ya tz ni tofauti na hiyo principle kwasababu mtazania hapewi haki ya kumiliki ardhi bali anapangishwa. Inaitwa 'right of occupancy" siyo " ownership". Kitaalamu ardhi ya Tanzania katika mahesabu watu wengi hukosea wakarecord kama land na huwa hawafanyi amortization. Lakini wanaojua huiita " prepaid lease" na ufanya amortization kulingana na lease tenure.

NJIA NYINGINE

Kama unayo maarifa ya biashara na unajua ni biashara gani inalipa basi ungechukua hiyo pesa ukaweka kwenye fixed deposit bank, alafu ukarudi tena benki baada ya kuwa umeamua biashara gani inalipa ukakopa pesa kiasi fulani kama 30% ya ulichoweka na security ya mkopo wako ikawa hiyo fixed deposit yako. Ukafanya biashara yako. Gharama halisi ya mkopo wako ni riba ya mkopo toa riba ya fixed deposit.

Mwisho wa yote utachukua pesa yako ukafanyie jambo lako lakini utakuwa pia umejifunza mengi juu ya biashara na hivyo waweza ondokana na kadhia za ajira.

Waweza pia tumia SACCOS ila uwe very selective.

Naomba kuwakilisha
 
nunua viwanja kuna faida sana ila usinunue vya bei mbaya zaidi ya kimoja i.e milioni 100+ hivi hata vingepanda bei kuja kuviuza ni ngumu sana labda uuze kwa bei ile ile uliyonunulia. Tafuta vya kuanzia 50ml kushuka chini lakini maeneo mazuri na yanayotambulika na una uhakika market value yake itakuwa.
mie nimeishafanya ingawa small scale mfano 2007 nilinunua 1.7ml na nimeuza 2011 6.8ml, nilipo 2003 nilinunua kwa 0.6ml sasa hivi ni 10 - 15ml.
Kwasasa anzia na vya 5ml kuendelea, pia angalia uwezekano hata wa kushika mashamba makubwa, kwani unaweza kuyakata na kuuza. Kila la heri mama.
 
Mkuu wangu pmwasyoke nilikusudia iwe hivyo hivyo kama mfano tu.
Ningeweka kiasi halisi labda ningeonekana nina lengo la ku-show off na watu wengine wangeishia kudhihaki badala ya kunipa ushauri.
Kujishusha mara nyingi ni kuzuri.

Una Hekima Ndugu,ulijuaje?!
 
Last edited by a moderator:
dada QK..nakubaliana na mawazo ya baadhi ya watu wengi kuinvest hela kwenye viwanja, ila kwa mtazamo wangu kulingana na hali zetu kiuchumi ukichukulia kwamba tunapata fursa za kupata mapato mara kwa mara lakini si kwa kiasi kikubwa kwa mkupuo mmoja kama walalaheri (mfano unaweza kujikuta unaweza kuingiza au kupata Tsh 10,000 kila siku lakini ukashindwa kupata hela kubwa kwa siku moja kwa njia hizo hizo).. Hivyo kwa ushauri wangu naona ni heri (kwa kuanzia) kuwekeza katika vyama, taasisi na makampuni ya kuweka na kukopa ili baada ya hiyo miaka mitano kwa mfano utajikuta una amana (akiba) ya kiasi kikubwa sana na utakuwa na fursa nzuri ya kuwezeshwa kupata mikopo mikubwa si tu katika taasisi uliyoweka bali hata katika banki na taasisi nyingine kubwa kwa kuwa utakuwa na historia nzuri ya kuweka, tena siku hizi teknolojia imekuwa kiasi kwamba unaweza kuweka amana zako kupitia simu za mikononi....

Kwangu mimi, ni bora kufanya biashara endelevu tofauti tofauti kwa hela unazopata kuliko kununua viwanja na kusubiri viongezeke thamani.

Mkuu wangu nashukuru sana kwa ushauri.
Hizi pesa ninazohitaji kuzisave nina malengo nazo mengine maana tayari kuna biashara ambayo ninaendeleza.
Sihitaji kukopa kwa ajili ya jambo lolote ila hizi pesa ninataka kuzifanyia jambo fulani baada ya miaka kadhaa.Ninachotaka ni njia tu ya kuzisave bila thamani yake kupungua ifikipo kipindi nitakapozihitaji.
Ubarikiwe sana mkuu OGOPASANA.
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma comments za wadau hapa lakini bado swali moja la msingi sijaona linajadiliwa. Wewe ni mfanyabiashara? Na ni mfanyabiashara kwenye sector gani, land?

Cardinala rule number one kwenye biashara ni liquidity. Investment utakazokuwa nazo basi ni vema utilie maanani 'liquidity'. Ardhi zinapanda bei, but how long it takes turn land into cash kama uko kwenye biashara? And can that business wait mpaka uuze hiyo land na ku-inject cash?

Cardinal rule number 2, dont put all your eggs in a single basket. Ardhi zinapanda bei, vipi kama haikupanda kama ulivyotarajia? diversify your investment vinginevyo unaweza kujikuta unakula hasara.

Asante mkuu wangu kwa ushauri na ufafanuzi mzuri.
Nadhani hapa hamjanielewa,kama biashara tayari ninafanya,hizi pesa ninazungumzia shida yangu sio kuzifanyia biashara nipate faida,shida yangu ni kuzihifadhi bila thamani yake kupungua.Sihitaji biashara nyingi nyingi maana akili na nguvu zangu naelekeza kwenye biashara niliyonayo sasa ili iweze kufikia levels ninazo dream.Ubarikiwe mkuu.
 
Naamini nimekuelewa,

yaani unataka kukusanya fedha kwa malengo fulani huko mbele kwa namna ambayo hela hizo ziwe ktk upande ambao zinajiongeza thamani bila wewe kupata presha kubwa sana, kwa hiyo njia mojawapo uliyochagua ili kufikia lengo ni kuweka ktk ardhi ukiamini kuwa huko hela zako zitakuwa salama na zikijiongeza ( ww hutajali rate ya kujiongeza bora ziwe salama na wakati ukifika uzipate) na sio biashara.

Hivi ndivyo nilivyomwelewa mimi huyu mdada.
 
Asante kwa kunielewa mkuu.
Kwa kufafanua zaidi ni kwamba,kwenye ardhi zitakua salama na pia siku yakuuza ili nipate pesa yangu,nitauza kulingana na thamani ya pesa ilivyo kwa wakati huo lakini zingekua bank thamani yake ingepungua.Kiufupi niseme kinachonifanya nisiweke bank ni kuogopa kuwa zitapungua thamani.
Ubarikiwe mkuu Malila.
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu wangu kwa ushauri na ufafanuzi mzuri.
Nadhani hapa hamjanielewa,kama biashara tayari ninafanya,hizi pesa ninazungumzia shida yangu sio kuzifanyia biashara nipate faida,shida yangu ni kuzihifadhi bila thamani yake kupungua.Sihitaji biashara nyingi nyingi maana akili na nguvu zangu naelekeza kwenye biashara niliyonayo sasa ili iweze kufikia levels ninazo dream.Ubarikiwe mkuu.

kama unataka kuweka pesa au fedha benki au kwenye kibubu isipungue thamani labda uanz
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/
 
Asante kwa kunielewa mkuu.
Kwa kufafanua zaidi ni kwamba,kwenye ardhi zitakua salama na pia siku yakuuza ili nipate pesa yangu,nitauza kulingana na thamani ya pesa ilivyo kwa wakati huo lakini zingekua bank thamani yake ingepungua.Kiufupi niseme kinachonifanya nisiweke bank ni kuogopa kuwa zitapungua thamani.
Ubarikiwe mkuu Malila.

Kwa sababu hii ya kuhifadhi pesa ni bora kutumia fixed deposit account. Kumbuka tu kuw kil utratibu wa kuhifadhi fedha una risk zake tofauti ni amount ya risk tu. Risk ya kununua kiwanja ni ugumu wa kuliquidify asset na pi serikali yetu kila kukicha inakuja na plan nyingine. Just imagine ungenunua kiwanja Kigamboni eneo la mrdi, hivi sasa kingekuwa hakiuziki! So to remain liquid with minimal risk and avoid inflation fixed deposit account is the best option in my view...
 
Back
Top Bottom