Kama nimejenga nyumba kwenye kiwanja si changu, kunivunjia nyumba au kuniambia ninunue hicho kiwanja kipi bora?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Wakati mwingine busara huwa inaitajika unapotoa maamzi. mediation inaweza kutumika .kwani kuna faida gani unapovunja nyumba ya mtu hata kama kiwanja si chake?

Wewe mwambie kiwanja si chake then akikubari mwambia nunua kiwanja hiki.ziko taasisi zenye kuthaminisha viwanja na majumba, Hivyo mhusika au mtuhumiwa ataweza kununua kiwanja hicho au nyumba hiyo kwa thamani halali iliyopangwa na wathaminishaji.unabomoa ghorofa ya mabilioni ili upate faida gani?

Kwanza Serikali inakosa mapato kupitia ubomoaji huo kwa sababu let us say ni nyumba ya kibiashara pale watu walikuwa wanaingiza hela na serikali inapata kodi sasa nyumba umevunja hapo serikali inapata nini?
 
Kipi Bora kwako au?
Kiwanja hakitegemei watu wa tahmini mtu akiamua kuuza ni yeye kuamua bei yake ambayo huangalia vitu vingi mfano wako watu wako tayari kununua kwa bei ambayo ni juu mara mia kuliko tathimini

Huwezi lazimisha mtu akuuzie kwa bei ya watathimini wako.

Akiona hailipi anakwambia toa jengo lako niachie kiwanja changu sitaki kukuuzia after all umenisumbua sana wewe.Ondoa takataka yako hapo Acha uwanja wangu wazi
 
Tena hao wavamizi wa viwanja vya watu wanakuwaga na kauli chafu mimi kuna mmoja kamega kiwanja changu namsubiria amalize ujenzi ili nivunje vizuri 🤨
hahahaaaaa.kazi ipo kwa kweli.

serikaliinatakiwa ipime viwanja vyote vya makazi na kuviweka kwenye satelite na iwepo sheria kwamba unapotaka kukunua kiwanja ,nenda ofisi za ardhi uapte maelekezo .
 
hahahaaaaa.kazi ipo kwa kweli.

serikaliinatakiwa ipime viwanja vyote vya makazi na kuviweka kwenye satelite na iwepo sheria kwamba unapotaka kukunua kiwanja ,nenda ofisi za ardhi uapte maelekezo .
Mimi huyu mgomvi wangu kabla hajaanza ujenzi serikali ya mitaa wameshamfata na vipimo anajifanya kichwa ngumu kwa akili yake anajua nimepotezea .
 
Back
Top Bottom