Kipengele cha dini na sensa

unajua serikali haina dini,,lakini wa tanzania wana dini zao....ushauli wako ni zaifu sana.. hauna mashiko.

Protox hapo hata kama waislamu mtaita mapepo na majini yote kutoka Makka na Madina kipengele cha dini hakitakuwa kwenye sensa. Na zikipatikana takwimu zisizo sahihi ninyi ndo mtakosa huduma na kuendeleza malalamiko yasiyo na tija. Pole sana
 
Ubalikiwe sana! sio kusudio langu...naomba ladhi kwa hili. mufti wangu.....Pia naomba unisaidie nani ataanzisha vita pindi kipengele cha dini kikirudishwa kwenye sensa?.>>>Uingereza wana mahakama ya kadhi, vipi tz? waislam nijirani zetu tuwapende kama ...lilelinalo wasibu tuwenapamoja.ugomvi hapa ni baina ya waislam na serikali siona na wakristu,.
vema ndugu, kote huko kadhi haijawekwa na serikali bali utaratibu maalum ya waislamu wenyewe, hapa bongo nyie mnataka serikali isio na dini iweke kadhi iili ipate nini? serikali ya JMT inawahudumia watz wote kwa ujumla, kadhi ili mkamate watu wanaokula siku za mfungo wenu wa kulazimishana? Dini/imani ni uhuru wa mtu, kufanya vile anavyoonainamfaa sio kulazimishana! Allah mwenyewe anakataza Bin-Adam kumwua Bin- Adam mwenziwe na kama atafanya hivyo HAKIKA DAMU yake nayo itamwagika, mathalan mvao wa HIJAB, mtu unavaa mpaka kupe hazionekani ndo nini? huko Bagdad na kwingineko hijab zinatumika kubeba mabom, vaa kanzu yako vizuri uonekane usoni maisha yaende. ALLAH AKBAR huku unafanya yasiompendeza MWENYEZI MUNGU? NJOO KWA YESU UPATE AMANI HACHA KUFUNGWA NA MAPOKEO YA MWANA-ADAMU, MMMH SHEIKH WANGU?
 
hakuna kipengele cha dini hakuna kuhesabiwa... huo ndio msimamo.. mtajihesabu wenyewe.... na wasaliti wa waislam bakwata
 
Kwasababu unajua mnavyoendesha serikali yenu na sasa mnaguswa pabaya. Mi nahisi hii amani ya kudanganyana siku moja haitakuwepo kabisa, huu ni ufedhuli sana.Angalia ulivyo na confidence za kutukana watu eti majini kutoka makka! Wewe shetani mkubwa kabisa. Nani alikwambia makka kuna majini?

Protox hapo hata kama waislamu mtaita mapepo na majini yote kutoka Makka na Madina kipengele cha dini hakitakuwa kwenye sensa. Na zikipatikana takwimu zisizo sahihi ninyi ndo mtakosa huduma na kuendeleza malalamiko yasiyo na tija. Pole sana
 
unajua tusiwalaumu sana hawa wanaotaka kipengele cha dini kiwepo....hebu tuelezeni kwa nn kiwepo,kitakuwa na faida gani kwa watanzania kikiwepo, na nyie waislamu mtafaidika vp??

msilete habari ya kwa kuwa TBC1 wametangaza au
wakatoliki wametangaza......

nataka kujua faida yake,may be inaweza kuwa nzuri na ss tukawaunga mkono badala ya kuwapinga.....
ni vyema pia tukawasikiliza tuone km ina faida
 
Jumamosi iliyopita nilihudhuria kongamano la taasisi ya kiislamu lililofanyika kwenye msikiti wa Alfaruq mkoani Shinyanga.Mengi yalizungumzwa katika kongomano hilo ikiwa pamoja na kutoa msimamo wa baadhi ya waislamu kupinga kuhesabiwa sensa na kuto kumtambua kadhi mkuu pamoja na makadhi 15 walioteuliwa na Mufti mkuu wa Tanzania.

Kwa upande mmoja serikali inatuhumiwa kuukandamiza Uislamu kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA),wamefika mbali zaidi kwa kuhoji hata nafasi za uongozi wa Taifa letu kwa misingi ya udini.Si nia yangu kujaribu kuzungumzia udini lakini hali hii imechochewa zaidi na chombo cha habari cha serikali kwa kutoa takwimu za kupika juu ya idadi ya Waislamu,Wakristo na Wasio na dini.

Chombo cha umma cha habari kinapotumika kama chambo cha kupika takwimu ni hatari kwa mustakabli wa taifa,kiasi cha Waislamu kutaka kujua nini hasa nia ya serikali kutaka kuwaminisha wananchi wake kwa takwimu hizo za kubumba.Ajabu na kweli leo katika kipindi cha jambo Tanzania,mkurugenzi wa TBC alitumia fursa hiyo kukanusha na kusema takwimu hizo hazikuwa sahihi na kuomba radhi kwa waumini wa dini yakiislamu.

Kwa kitendo hiki cha kuomba radhi ilihali hali ya hewa imekwisha chafuka na Waislamu kutishia kuto kuhesabiwa sensa inaiweka wapi umakini wa serikali iliyo sikivu.

Ikiwa sheria ya kimataifa ya takwimu za population ya watu duniani ina tamka wazi misingi ya kuhesabiwa ni pamoja na vipengele vya dini ,madhehebu na hata makabila,nini hasa kilichoisukuma serikali yetu kukiondoa kipengele hicho kinacho julikana kimataifa kama si samaki kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe

Tunahitaji serikali makini katika kuyapima mambo ambayo hayataleta mtafaruku wa amani hii tuliyo nayo kupotea.Ile dhana ya udini iliyokuwa ikinadiwa sana kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu sasa imeshika kasi kiasi cha kusababisha busara kupotea.Hatuwezi kuwa na viongozi wasio kuwa na hekima kwa kushindwa kuzuia ya mioyoni mwa na kutukana viongozi wa dini.

Kwa suala hil la sensa ya watu na makazi inabidi serikali ikubali kuwa imeteleza la sivyo tuachane nalo kwa serikali kujiandaa vizuri kuliko kupoteza pesa za kodi ya Watanzania kwa kukusanya takwimu ambazo hazitakuwa na ukweli wowote.Namaanisha kuwa kama serikali kwa kupitia wakuu wa Mikoa imesimama kidete kuwatisha wananchi wake watakao kataa kuhesabiwa una tegemea nini kama si machafuko ndani ya nchi na kukusanya takwimu zisizo sahihi kwa kudanganywa kwa makusudi na wananchi.

Ni bora serikali ikae chini na viongozi hao wa dini zote zilizo hapa nchi na kusikiliza hoja zao za msingi kuliko njia inayo jaribu kutumiwa hivi sasa ya kuwatisha wananchi.Siku zote hoja hujibiwa kwa hoja na si kwa vitisho,kwa staili ya vitisho inaashiria serikali kushindwa kuwaongoza wananchi wake kwa misingi ya kidemokrasia.

Ama kweli nimeamini zimwi likujualo halikuli likakwisha,matokeo haya yote ni ile dhambi ya kubaguana ambayo ikisha kukaa lazima utaisambaza kila kona.Udini uliotumika kama agenda kuu ya uchaguzi leo imezaa matunda na kuigeukia serikali iliyo kuwa dalali mkuu wa kuinadi sera hiyo.

Hekima itumike kuinusuru taifa letu,japo kuwa amani yetu ni ya bandia lakini kuna nchi zina itamani,chonde chonde tunataka amani halisia kuliko kuona viashiria vya uvunjivu wa amani ambao msingi wake mkuu ni serikali yenyewe.

Nawasihi wakae chini watafakari kwa kina na kurudisha vipengele ambvyo vinajulikani katika sheria za kukusanya takwimu za idadi ya watu na hali ya amani itakuwa shwari.Tusingependa Watanzania tuyazoe mabomu,tukiyazoea nchi haitakalika.Tuache hekima ichukue mkondo wake.
 
Sammosses, nakushukuru sana. Sasa ndugu zanguni, hebu someni hiki alichokiandika sammosses kisha mtafakari. Kulikoni. Na mnayo fursa ya kufuatilia zaidi ili tu kujua ukweli wa kinancho endelea. Wasomi wa dini zote, hebu liangalieni hili. Hivi kweli waislamu ni wachochozi au kuna jambo hapa?
 
J.K na kundi lake ndio walipanda sana udini eti Chadema ni cha wakristo sasa wanavuna walicho panda, nawasihi ndugu zetu Waislamu, sameheni tu, hawa jamaa walishashindwa kuongoza nchi, angalieni hatma ya Taifa letu na sio Pinda, J.K Na kundi lao!
 
Ni ukweli usiopingika,rais wetu ana upungufu mkubwa wa washauri,haiwezekani mshauri ana yetegemea na serikali ndiye ambaye ametmuka vibaya kuchafua hali ya hewa kwa kauli zake zisizo na mashiko,samaki huyu tumechelewa kumkunja angali mbichi tukimlazimisha kukunjika mwishowe tuta mvunja
 
J.K na kundi lake ndio walipanda sana udini eti Chadema ni cha wakristo sasa wanavuna walicho panda, nawasihi ndugu zetu Waislamu, sameheni tu, hawa jamaa walishashindwa kuongoza nchi, angalieni hatma ya Taifa letu na sio Pinda, J.K Na kundi lao!

Tatizo kila jambo lina fanywa kisiasa kuliko uhalisia zaidi,ukiangalia makubaliano yao juu ya kuundwa mahakam ya Kadhi,siasa ilitumika zaidi na kupora majukumu ambayo yaltakiwa kuwasilishwa na jumuiya ya maulamaa wa Shura ya maimamu wapatao 25.

Kwa kitendo cha serikali kukubali mtu mmoja japokuwa ndiye kiongozi kuu wa Waislamu Tanzania kuwasilisha uteuzi wa Makadhi bila kufuata utaratibu uliokuwa umekubalika ikiwa ni pamoja na serikali kutoa Ofisa mmoja na wajumbe wawili ndani ya jopo la maulamaa kutembelea nchi zingine zilizo na mahakam za Kadhi kuangalia wanafanyaje kuziendesha mahakama hizo,Waislamu wanaamini kuwa serikali ina sababu maalumu ya kutaka kuwa kandamiza Waislamu
 
Back
Top Bottom