Kipanya anamchokoza mtu

Hahhaaaa hapo anamaanisha huyo dereva alieshikilia camera kuwa ameshakula huo mhogo hadi kaota kitambi na kashiba ila hao wanaopiga makasia anaowaongoza wananjaa hivyo jamaa yeye anajua yuko nao sambamba kumbe huko nyuma wananjaa wanamegua taratibu huo mhogo
 
Hii falsafa
Huto kaa uielewe kamwe.

Falsafa pi ni siyo ielewa??Kuna maneno JKN aliyaongea straight hakuficha kitu.Asiyetii na kuilinda Katiba na SHeria alizoapa kuzilinda hatufai arudi kwao akachunge ng'ombe
 
Mmh. We umeangalia katuni ipi??

Hihi ninayomuona nahodha kajitahidi kutafuta mpaka kiona mbali ili asipotee??

Na yeye ameanza kula muhogo hana tofauti na wale wenzake aliowapakia kule nyuma
 
Hahahahaah hujaelewa, sehemu walioko hao panya wadogo haijaliwa, ila sehemu waliopo waongozaji ndio imeliwa, ukiangalia kwa makini, utaona hao panya wadogo wanajitahidi nao wale ila wanashindwa(may be sababu hawana meno), ila bahari imetulia(sisi watanzania) mtumbwi utazamishwa na hao wanaongoza.
 
Nahodha anaongoza kwa darubini kali na hatafuni chochote
Lakini abiria sasa(raia/waongozwaji) wanaitafuna botihogo (nchi) bila kujali matokeo hasi ya ulaji ama ubadhirifu wao.
kwa juu mbele ya nahodha pametefunwa
 
Mwendesha mtumbwi ni mmoja tena yuko nyuma na anaonekana amejimegea kipande cha muhogo huku hao wa katikati wakionekana kutojuwa wanakoelekea.Na jamaa hapo mbele akionekana ni mlaji tena alieshiba vizuri akiwa hana muda na hawa waliopo kati ama abiria

Kifupi wanaoongoza nchi ndyo wanaojitafunia muhogo tanzania huku wakiwaacha abiria watanzania wakiwa hawana muelekeo wowote na hawajui wapi nchi yao inakoelekea huku wakikabiliwa na njaa na matatizo lukuki

Lakini swali la kujiuliza huyu anaendeesha muhogo Tanzania anautafunaje muhogo Tanzania?
 
na hayo maji yana maana gani..kama ni ishu ya kula mhogo?
 
almost there
 
Hii inaitwa kama umelianzisha Bora tufe wote.

Sent using Iphone 7+
 
Hahaha....ila yeye katafuna kwa juu hajaharibu , wanaoharibu ni wale wanaotafuna pembeni
Mkuu, anaendelea kujitafunia yani hapo kuongoza ni kama chai, mkate ni huo mtumbwi, ataupararua hadi mwisho
 
Kizazi cha panya. ..kina kula hata kinachowawezesha kusafiri

Sent from my TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…