Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 46,998
- 32,441
KIONGOZI wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (chadema) Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ( jina linahifadhiwa) anashikiliwa polisi akidaiwa kufuja Sh 600,000 fedha za mfuko wa Elimu wa wakazi wa Kazamoyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa Elimu, Mtaa wa Kazamoto, mjini mdogo wa mererani, Sokoto Mbuya alisema kiongozi huyo alifuja fedha hizo akiwa mweka hazina wa kamati hiyo na alipewa Sh 1.045 milioni walizopata kutokana na michango ya wananchi wa mtaa huo ambao kila mkazi alichangia Sh 500.
Alisema walimpa fedha hizo awe nazo kutokana na nafasi yake ya mweka hazina wa mfuko huo na walitoa Sh 445.000 kwa ajili ya kununulia vifaa vya shule ya msingi Endiamtu na fedha zilizobaki akawa anawazungusha wajumbe kuzitoa. kamanda wa polisi wa mkoa wa manyara, Parmena Sumary, alidhibitisha kukamwatwa kwa katibu huyo wa Chadema.
SOURCE: MWANANCHI MEI 26, 2011