Kiongozi wa machifu Tanzania ataka Serikali iwatambue rasmi machifu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,905
Kiongozi wa machifu Tanzania ataka serikali iwatambue rasmi machifu akisoma risala mbele ya Rais Samia kwenye Takashi la Utamaduni Mwanza

Je anataka ukatili na serikali za kikabila urudishwe?

machifu.jpg
 
Katika vitu ambavyo Nyerere alitumia akili sana ni kuvunjilia mbali uchifu, wangetuvuruga kwa ukabila na hivyo project ya kujenga utaifa kufeli
Namsikiliza huyu Rais amekubali ombi lao na amesema anaandaa kikao akutane na mchifu Tanzania nzima 🤣 🤣 🤣 🤣🤣

Amesema pia anandaa na tamasha la machifu Tz, watashindania kombe linaloitwa Hangaya, ambalo ni Jina la Kisukuma alilopewa Samia likimaanisha nyota

Huyu mama nilidhani kwa kuwa ni mzanzibari (Mswahili) hataendeleza haya mambo ya ukabila, kumbe sikuwa sahihi
 
mzaramo yupi? Dar kuna wazaramo pure? wengi walishaingia ndoa za mchanganyiko hawajui hata lugha yenyewe ya kizaramo

Ulishawahi au sikia mtu akiongea kizaramo kwenye daladala yeyote? ukisikia watu wanaongea kilugha kwenye daladala ni makonde,wamakua,wachaga,wanyakyusa ,waha na wasukuma na wanyamwezi

Hata mitaani si rahisi kumkuta mtu akiongea kizaramo
 
Back
Top Bottom