Kiongozi anapochanganya lugha ya Kiswahili na kiingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi anapochanganya lugha ya Kiswahili na kiingereza

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Bobby, Sep 19, 2012.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mimi ni mmoja wa watu ninaokwazwa sana na tabia ya rais Kikwete kuchanganya kiingereza anapoongea kiswahili kwenye hadhila mfano mzuri ni juzi kwenye mambo ya mitaa.Ninakwazwa kwa sababu nyingi chache ni hizi hapa:

  1. Siamini kwamba rais Kikwete kiswahili kinampa shida kiasi cha kumlazimu kuchanganya kidhungu, Kikwete ni mtu wa pwani anajua kiswahili kuliko wengi wetu.
  2. Pamoja na mapungufu yake, siamini kwamba kiswahili hakijitoshelezi ndio maana inabidi Kikwete akisaidie kukiazimia maneno kutoka kwenye kiingereza.

  3. Si watanzania wote wanajua kiingereza kwa hiyo rais anapochanganya kiingerza kwenye hotuba au maongezi yeyote ya kiswahili hawatendei haki watanzania wasiojua Kiingereza.


  4. Watanzania tuko kwenye mkakati wa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya maziwa makuu, afrika ya kati na zaidi ya hapo ndio maana nchi hizo zinajitahidi sana sasa kujifunza kiswahili. Kitendo cha rais kukiabudu kiingereza anarudisha nyuma juhudi zetu hizi. Wito nautoa kwa washauri wa rais wamuombe aachane na tabia hii ya kuchanganya sana kiingereza kwenye shughuli za kiswahili kwani haileti picha nzuri kwa wengine kwani inajulikana sisi ndio waasisi wa kiswahili, ni lazima tuoneshe kukithamini kiswahili chetu.
   
 2. Blaque

  Blaque Senior Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  So rais
  mkuu ni ubinadamu tu angalia wewe umetumia so
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ni ushamba kujifanya unachanya kiswaili na kiingereza
   
 4. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Bobby, nadhani katika hili Mh.Rais tutakuwa tunamuonea kwa sababu:

  1. Sababu ya kwanza uliyoitoa, kuzaliwa Pwani haimaanishi umezaliwa na kamusi mkuu wangu. ..hebu tukumbushane ni wazaramo wangapi wanaongea kiswahili SANIFU???!(NO OFFENCE TO ZARAMO, just making a point)...

  2.Mkuu, nadhani kiswahili hakijitoshelezi sana tu na mifano ipo hai..halafu katika hoja yako mwenyewe ulisema neno la kiingereza "public"..

  3.Ni kweli si watanzania wote tunaojua hiyo lugha ya wageni, lakini haimaanishi kwa wanaoijua wasiiongee...Akiwa kama Rais katika hotuba za mwisho wa mwezi Mh. Rais hutoa hotuba kwa kiswahili(hadi maali pale tu kwenye ufafanuzi wa kiini cha jambo fulani)..ambapo ni kutokana na huko KUTOKUJITOSHELEZA kwa lugha yetu.


  Nadhani,
  Katika hili tutakuwa tumemwonea Mh. Rais, na pia mifumo yetu ukiangalia nchi zenye kutumia LUGHA ZAO, kiuchumi si haba mkuu, kwa kutegemea misaada(lazima tujiweke kwenye lugha hiyo hiyo ya kuombea misaada),

  Pili mitaala yetu ikoje,??hata watoto wetu mashuleni bado lugha yetu WENYEWE ni tatizo kuiongea, ukipingana na hili tazama hata uchangiaji wetu humu jamvini katika lugha, LAKINI ni mara ngapi watu kutoka nje(wageni, "wazungu), huja Tanzania? mara nyingi na wakijia gujifunza kiswahili kile HALISI cha kamusi(utawaona wakitembea na kamusi ndogo) na baada ya miezi kadhaa huongea lugha nzuri kuliko sisi!


  Tatu, tmashuleni hasa sekondari, utakuta kuna vibao vingi vimeandikwa "SPEAK ENGLISH" ,na hata wanafunzi huadhibiwa wakikiuka, je walipokuwa shule za msingi tulishindwa kuweka vibao vinavyohamasisha kuongea kiswahili sanfu na si kile cha mitaani "slang"??
   
 5. K

  Kulya JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 339
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ​It begins with you!
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wewe unashangaa kuchanganya Kiingereza anapozungumza kiswahili?

  Hujamsikia anapozungumza kiingereza anachanganya kiswahili?

  Umemsikia na Membe nae anapozungumza kiswahili? link Mahojiano kati ya bloggers wa DC na Mhe. Bernard Membe - YouTube


  Usifikiri ninawalaumu au kuwacheka hao waheshimiwa, mimi menyewe niko hivyo pia. Mfumo wa luga kwenye bongo yangu huchanganyikiwa kutokana na kasi ya fikra juu ya mada na ugoigoi wa kujitokeza kwa maneno katika luga ninayotumia wakati huo. Basi hujikuta nachanganya luga zote 6 ninazozungumza. :redface:,:loco:,:sleepy:
   
 7. K

  Kipimbwe JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hapa kaonewa wengi huwa tunachanganya
   
 8. B

  Bobby JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mkuu Blaque na wengine ahsante nimehariri ili ujumbe wangu uweze kufika vizuri japo shida yangu haikuwa hasa kwenye neno moja au mawili. Nimeshaona mahali rais anaongea sentensi kwa kiingereza wakati anahutubia kwa kiswahili na si nukuu la hasha halafu wala hatoi tafsiri yake. Na nimemtaja yeye nikijua fika nguvu aliyonayo kama rais kwenye jamii. Wote tunakubali kwamba jambo linapofanywa na rais inaonekana kama ndivyo tunavyopaswa wote kufanya. Mimi ningetarajia yeye awe wa kwanza kujivunia lugha yetu lakini kwa bahati mbaya anaueleza umma kwamba kiswahili hakijitoshelezi au ili uonekane msomi ni lazima uchanganye Kiingereza kitu amabacho si sahihi kabisa. Mfano wa wasomi ambao ninawapongeza kwenye hili ni Profesa Issa Shivji. Wote tunafahamu namna ambavyo huyu mzee anapoongea anajitahidi sana kuhakikisha anatumia kiswahili peke yake labda pale inapobidi sana.
   
 9. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mkuu umenisaidia kutohoa maeneo ambapo fanani amekiuka matumizi sahihi ya kiswahili kama anavyopenda iwe,thanks kamanda
   
Loading...