Kinyume na Ulaghai: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliridhiwa na chombo halali cha Zanzibar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinyume na Ulaghai: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliridhiwa na chombo halali cha Zanzibar!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 7, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]

  My Take:

  Madai ya muda mrefu kuwa muungano haukuridhiwa na Wazanzibari hayana msingi. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali kwani vyombo halali viliridhia pande zote za Muungano.

  Uhalali wake hata hivyo hauzuii Wazanzibar kutaka kujitoa kwani hata leo chombo kile kile kilichoridhia Karume atie sahihi makubaliano ya Muungano bado kipo na kinaongozwa na Dr. Shein.

  Wazanzibar wakitaka wakishawishi chombo hicho kuondoa ridhaa yake ili hatimaye Baraza la Wawakilishi lipitishe utaratibu wa Zanzibar kurudi katika status quo ya April 25, 1964.z
   

  Attached Files:

 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  MMKJ, acha kupotosha watu,

  Msome mwanasheria Pasco

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nimeisoma na haina msingi wa historia; yote anayoyasema ni kweli lakini ana assume (kwa makosa makubwa) chombo halali cha Wazanzibar wakati ule hakikuridhia Muungano. Halafu inaonekana umesoma alichoandika Pasco kana kwamba ndivyo ilivyotokea (as historical fact) wakati alichoandika ni ubunifu tu wa fikra zake.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Anayetaka kubisha abishe tu; hakuna Mzanzibari hata mmoja kwenye Revolutionary Council aliyepinga Muungano!
   
 5. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kwanza wanaojiita wanzibaari asili yao siyo zanzibar....................wengi wao asili yao ni msumbiji katika kisiwa cha pemba............wanadhani udini utawapeleka mbali ...........la hasha hawafiki kokote kule...............waulizeneni taiwan walipotaka kujitenga na uchina nini kilitokea. mwanzilishi wa uamsho ni dk shein kwa taarifa yenu kama hamjui.............swali kwanini shein?

  NAOMBA NIISHIE HAPA KWA LEO HOPE 2SEE U 2MORO


  UKIWA NA MASWALI NIPM

  SENIOR INTELLIGENT OFFICER (CIA)
   
 6. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0

  Kaka unaakili sana natamani nikutane na wewe nibadilishe mawazo hata dakika 10 kama inawezekana . Kunakitu bado Wazanzibari hawaelewi kuhusu muungano.................naomba wale wanaoshabikia kuuvunja muungano wasome kuhusu tiananmen square china

  [​IMG]
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  kulitokea nini? mbona waweka vifaru tena ..let them go hatutaki kuanza kulipuliwa huku bara bure kisa muungano
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Pasco? Who the bloody hell is Pasco? Jamani tuache utani na watu kama Pasco tukae nao chonjo kweli kweli, ni opportunist anaetumika tu kwa malengo anayoyajua yeye. Zanzibar wakitaka kuondoka rukhsa, kinawazuia nini! Wasianze kutuchanganya eti hawakushirikishwa, waache kabisa kutafuta visingizio visivyo na kichwa wala mguu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uhalali wa kutoka kwenye makabrasha ya CIA? tuoneshe uhalali wa kutoka Serikali ya Zanzibar na Tanganyika.

  Kama hauna, kaa kimya. Unajuwa sana kuwa huu ni muungano ulioshadidiwa na Nyerere kwa sababu ya kueneza Ukatoliki Zanzibar.
   
 10. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Asante sana Mwanakijiji kwa document hizo:

  Cha kujiuliza ni kwamba yeyote anayeupinga muungano ni Muhaini maana anayapinga mapinduzi ya Zanzibar.

  Kwanini wanaoupinga muungano wasiyapinge kwanza mapinduzi yaliyomuweka Karume madarakani? Maana serikali inaitwa ya mapinduzi na hata documents inasema revolutionary council wamekubali unanimously... au ni mimi sielewi maana ya neno unanimously? Ina maana wana mapinduzi walipiga kura na kukubali muungano kama documents inavyosema.

  Na kila siku tunasikia kwamba SMZ kazi yake ni kuyalinda mapinduzi hayo, sasa iweje leo UAMSHO walete chokochoko na kusema tujadili muungani bila kwanza kuyajadili mapinduzi yenyewe: Inafaa kwanza wayajadali mapinduzi, na waiondoe madarakani serikali iliyoapa kuyalinda mapinduzi hayo either kwa boz la kura, mtutu au kwa njia nyingine zinazofaa.. wakimaliza hayo ndo sasa waje kujadili muungano...

  Mwisho ningependa kujua tu kwanini hizo documents zilikuwa approved for rease 18.11.1997... je kulikuwa na kesi au nini kilichopelekea kutolewa
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  Acha kuwatukana wazanzibar...ina maana wao mataahira hadi wapelekwe pelekwe kiasi hiko? Nyerere aeneze ukatoliki ili iweje.. Unamfananisha Nyerere na wale wazee wenu wa uamsho? Lini ulimuona anaongelea kusambaa kwa ukatoliki ama ni nyie na imaginations zenu za kipumbavu ambazo hazi exist.. Let em go na najua wakishajitoa na kuanza kupigika wataanza kuilamu Tanganyika kumbe wamefeli wenyewe kimikakati.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nyaraka zote za intelligence na zile ambazo ziko 'classified' zinalindwa kutolewa hadharani kwa muda wa miaka mbalimbali. Kiwango cha chini ni miaka 30 na nadhani kiwango cha juu ni miaka 70 kutegemeana na nchi. Nyaraka hizo zilikuwa classified kwa miaka thelathini naamini. Sasa hivi nyaraka za Tanzania zilizokuwa zimekuwa classified kwa miaka 30 na 40 sasa hizi zinatakiwa ziwekwe wazi - kama wasomi wetu wangeng'ang'ania na waandishi wetu kupigania.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Duu kazi kweli kweli,kuna kitu watanzania wengi hatukijui hapo, kama Bunge halikuwepo na baraza la mapinduzi ndio kila kitu kwa wakati ule,sasa kwa nini Muungano usiwe halali? Na pia kwa nini wasingeuratimisha baada ya kupata bunge?

  Kama sheria inavyotaka?wakati umefika wananchi kwa maslahi ya nchi zote 2 waamue ila kusiwe na shinikizo la wachache kuamua juu ya wengi!hasa pesa chafu toka nje!!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi hujasikia Shein anaitwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi? au mnafikiria "Baraza la Mapinduzi" halipo? Ndio chombo cha juu Zanzibar - inaitwa "Revolutionary Council". Baraza la Wawakilishi bado haliaminiki kuongoza Zanzibar.
   
 15. m

  mzaire JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Upotoshaji wako usio na mashiko waambie hao hao vilaza wenzako huko Tanganyika.
  Ikiwa mwanasheria wa Z'bar (Wolfred) wakati ule hakuwa na taarifa wala kutia saini yake na hilo alikiri mwenyewe mara kadhaa sasa huo ni uhalali gani? Usikurupuke na kuandika na kutuletea chiti za zisizo na mashiko.

  Kwa mujibu wa Nassor Moyo "huu muungano haukuwa na mashiko yyte isipokuwa ulikuwa wa kulazimishwa kwa njia ya vtisho kutoka kwa Nyerere (LTULLAAh) na hzo union matters zilikuwa 11 tu

  Hata hivo muungano wenyewe ulikuwa wa muda tu wa miaka 10 na ilipokaribia kuisha ndio huyu adui wetu Nyerere aliopomuita Karume akakataa ndio Nyerere akamuuwa Karume"

  Usipotoshe Mwanakijiji ikiwa unataka ushahidi usituletee cjui intelejensia zako nenda kwa Professor Shivji na Mwanasheria Mkuu wa Z'bar utapata kujua kuwa hata huo muelekeo wa muungano Karume aliambiwa na Nyerere kuwa ni Muungano wa Afrika mashariki na sio Tanganyika Na Z'bar.

  Tena unaiscan ili ionekane kuwa ni ya kweli duh! ama ww huna tofauti na yule mwandishi wa habari wa POLISI wa Z'bar alosema kuwa "MUAMSHO wamesambaratika na Muhadhara umehudhuriwa na watu kdogo tena kwa ajili ya swala ya alghaaswir" na hali watu walijaa mpaka uwanja wa Malindi wote ukafurika na wakaibika siku ya Jumapili.
   
 16. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ''wazanzibar wanaoleta fujo kwa kisingizio cha kupinga muungano wamevimbiwa amani,wamevimbiwa raha''
  - Ally Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Tanzania.
   
 17. m

  mzaire JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaonekana huu muungano ulikuwa ni wa Tangayika tu maana kila ushahidi wa muungano uko Tanganyika!!! Basi cjui kama Tanganyika Ulijiunga na kujichukulia kila kitu cha muungano au vp?

  Maana likitokea suala la ushahidi wa muungano Tanganyika ndio hujitutumua kutoa maelezo lakini kule Zenji wanakwambia ss hatuna waraka huo na wala hatuwahi kuuona na wala hatuna uhakiaka na waraka huo kw7bu hakuna maelezo kuhusiana na waraka huo.

  Mfano hakuna mwanasheria hata mmoja wa Z'bar alokiri kuwepo kwa waraka wa muungano alafu leo wee Mwanakijiji watuletea siasa za kizushi kwa kuuhalalisha upuuzi huu naona kwa Wazanzibari huna cha kuwaeleza maana wako tayari kwa llte hata kifo ni bora kuliko kutawaliwa na Watanganyika na soon utasikia khabari mzito wakati hilo Tume la Katiba likijaribu kuingia kule Zenji.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  And this is the moment Mzee maana hawa jamaa wanatupigia kelele tu na kutupotezea muda.
   
 19. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,607
  Likes Received: 6,774
  Trophy Points: 280
  sasa kipi ni kipi mkuu, muungano ulikuwa ni wa miaka 10 au haukutiwa saini kabisa? Last time namsikiliza mzee moyo katika redio moja ya kimataifa akihojiwa alisema wazi kabisa, kwamba yeye kama waziri wa sheria wa wakati huo aliuona mkataba huo!- nenda kwenye archives za mzalendo.net walishaiweka hiyo vidio, kwa hiyo usimsingizie mzee wa watu.
   
 20. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Dunia hii ya ajabu kweli, wengine wakipindua wanaitwa wahaini, wangine wanamapinduzi. Wate halali?
   
Loading...