Upotoshaji wa Muungano ni Zanzibar na Tanganyika na wala siyo Tanzania Bara na Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Utawasikia hata waheshimiwa, viongozi wa Taasisi za Serikali na Mashirika wakisema "Tunasherehekea miaka 59 ya Muungano wetu wa Tanzania Bara na Zanzibar

Kilicho wazi ni kwamba Upande wa Bara hawapendi kutaja jina TANGANYIKA, ni kama vile kwa makusudi au wanaona kama ni aibu fulani hivi.

Kwa Upande wa Zanzibar wanaona fahari kutamka TANGANYIKA na ZANZIBAR

Tatizo ni nini?
Jee kunafichwa kwa Makusudi kutamkwa Tanzania Bara badala ya Tanganyika? kwa lengo gani?

Kwani Tanzania Bara ni Nchi? Jina Tanzania limepatikana baada ya tarehe 26 Aprili, 1964, kabla ya hapo na kabla ya Kuungana ilikuwa ni TANGANYIKA. shida ni nini? Huu upotoshaji una maana gani.
 
ikiwa wao wenyewe hawalipendi na wameamua kutolitumia wewe kwanini unateseka ndugu?
 
Tanganyika ilikuwa ni Nchi ya Zanzibar kabla ya uvamizi wa Mjerumani.

Samia uza.
Shogawe Zanzibar ilikuwa ni nchi ya Kilwa Kisiwani miaka 1000 iliopita.
 
Attachments

  • FB_IMG_1686182690771.jpg
    FB_IMG_1686182690771.jpg
    91.2 KB · Views: 7
Mafia ni Kisiwa. Unaana gani unaposema Tanganyika ni Tanzania bara?
Hujui kuwa Tanganyika ilikukuwa na Kisiwa cha Mafia. Mafia sio Zanzibar
 
Kwa maoni yangu,Msingi mkubwa wa Muungano Kwa fikra zangu ni suala la Usalama wa Tanzania Bara na Visiwani na hasa baada ya mapinduzi ..Kama ilivyo Taiwan Kwa China Mainland au Ukraine Kwa Russia..Zanzibar Ina umuhimu strategically Kwa Tanganyika vivyo hivyo Kwa Nchi Za Kiarabu..

Mizizi ya Waarabu wa Oman si ya kufutika leo wala kesho..mwarabu Ana kiu na uchu wa kuirudisha Zanzibar ktk mikono yake kuliko tunavyodhani Kwa sasa kikwazo kikubwa ni Tanganyika au Serikali ya Muungano…

Kwa historia,Utamaduni wa Kiarabu umetamalaki sana ZNZ..Ndugu Zangu wa asili ya Zanzibar ni watu wapole ktk maamuzi ,Wepesi wa kupokea,Wanapenda raha ,Hawana nongwa wakishiba..Hawana hiana wakiwa na raha zao..Wana moyo mizuri wakikirimiwa vema..Ndugu zangu wa Zanzibar wenye asili ya Uarabu wao wapo aggresive kiasi kibiashara na kiutawala (Wana ushawishi)..Japo lengo Lao kuu ni kurudisha utawala wa Kisultani..

Sasa Kwa kuwa Zanzibar ni mlango kwa kuingia bara,Zamani zile masuala ya ulinzi na usalama yalihusisha physical confrontation wakati nyakati hizi (Digital age)..Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yameleta uvumbuzi na mapinduzi ya kiusalama na ulinzi (Air,Sea,Land,Cyber ) kuna cyber attacks,drones,UAV n.k..

On the other hand ,Sio kwamba Wazanzibar wana furaha na Muungano..Wanapenda kujitawala,kuwa na Dola kamili kuwa na uwezo wa kushiriki michakato ya kimataifa (Kisiasa,Kiutamaduni,Kiuchumi,N.K)..Refer michakato mbalimbali ya kujiunga OIC,FIFA,UN,AU,IMO,etc..

Ikitokea leo Kura ya maoni kwamba wachague kujitenga na muungano (JMT) ama Kwa hakika si chini ya asilimia 96 watakubali kujitenga..Though Kwa sasa Wapo kwenye neema kubwa ya kufaidi matunda ya Muungano.. Hivi juzi gawio la fedha (Misaada,Mikopo,Riziki) kwenda Zanzibar toka JMT limeongezwa toka 4.5% mpaka 9% kupitia jitihada Za Mh Rais Samia na Mh Rais Mwinyi..Hongera viongozi Kwa maamuzi thabiti..Neema juu ya Neema.

Hakuna ndoa isiokuwa na changamoto,yapo mazuri Kwa Pande zote lakini zipo changamoto..Penye nia pana njia hivyo Hakuna shida isiotaturika..Tumekuwa familia ,Sisi ni ndugu wa karibu..Linalowezekana kutatuliwa litatuliwe Kwa hekima na busara..
 
kupushana au kugombana Kwa wanandoa ni jambo la kawaida ktk mahusiano ya kiafrika..mke anaweza kufunga vilago leo kesho akarudi maisha yakaendelea
 
Udhaifu wa JK mwaka 2010 Amani Karume pamoja huyo dada yetu na kwa ushirikiano na chama upinzani ambao ni Zambarau (hata Karume na dada sio kijani chama kinachohujumu Zanzibar, ni Zambarau lakini kwa code language) walipitisha katika 2010 ya Zanzibar iliotamka kuwa Zanzibar ni nchi kamili na sio sehemu ya Tanzania. Dada nae kamaliza utata wa mipaka ya baharini, Zanzibar hufika hadi kusini mwa Daressalaam kwa baharini.

Tanganyika ilikuwa ni Nchi ya Zanzibar kabla ya uvamizi wa Mjerumani.

Samia uza.
Huu ujinga ni kwa nini huwa unapewa promo??

ukiuliza lini Tanganyika ilikuwa sehemu ya Zanzibar, unaambiwa enzi za Sultan wa Zanzibar.

Lakini ushahidi unaonesha kuwa Tanganyika haijawahi kuwa sehemu ya Himaya ya Sultan bali maeneo ya Pwani walikuwa wanafanya biashara na maingiliano na washihiri na waarabu wa Oman.

Kinachoshangaza ni kuwa wanaosema Tanganyika ilikuwa sehemu ya Zanzibar ndiyo hao hao ambao walikuwa wanawaita CUF (Ile ya Maalim Seif) kuwa ni vibaraka wa waarabu.

Wana kisebu sebu na kiroho papo!!
 
Back
Top Bottom