Kinyago ulichochonga mwenyewe kinapokutisha unafanyaje!?

Kinyago ulichochonga mwenyewe kinapokutisha unafanyaje!?

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,311
Reaction score
12,202
Kuna rafiki yangu mmoja toka chuoni nilikuwa naye, huyu jamaa hakua ile die hard friend but tulikuwa tunajuana sababu alikuwa na akili sana kwenye 'namba' kwahiyo ndio mmoja ya watu waliokuwa wananipa kampani kwenye zile mambo za darasani.

Tulipomaliza kila mtu akaelekea kwao but still niliendelea kuwasiliana nae kama kawaida, then baadae nilijitegemea but mwenzangu hakuweza pata chance akabaki kwao jobless!. Huyu jamaa kwakweli nilikuwa namfahamu tu kama rafiki lakini sikuwa namjua tabia zake kiundani.

Baada ya almost mwaka kuna Biashara flani niliwashauri watu tuifanye, tukafungua kampuni yetu ambayo ilijitegemea na kwa vile ile idea haikuwa yao na me niliiplan ili kuninufaisha 'kiaina' basi nikamkumbuka huyu jamaa 'kichwa' nikamshtua aje then nikamconnect nasi ili awe mhasibu wetu! (kuingia kwake tu nilimuelekeza mambo ya kuja ongea wakati huo nikijifanya simjui ili wasije ogopa washirika).

Lakini kabla ya kumconnect nilimwelekeza kabisa ingawa atakuwa chini yetu sote but kumchagua yeye ni ili anifanyie 'some leverage' mimi hasa tunayejuana bila wenzangu kujua!

Kilichotokea recently nimekuwa nikiona hawa wenzangu tunaoshirikiana kama ile trust ya mwanzo imepungua ikabidi nianze kufuatilia ni kwanini. Wiki iliyopita mmoja ya washirika wenzangu alinitonya yule jamaa (friend yangu) ndio ananichoma kwao ili tuvunje kampuni sababu nawazunguka kupitia yeye!.

Najua wale jamaa hawawezi kuvunja sababu kuna vitu wananitegemea!.
Sasa nabaki njia panda je, nitengeneze plan nimtimue yule mhasibu (friend)?

Najua nitakuwa nimemharibia maisha yake sababu namjua alivyo mpaka kwao (even familia yake as Mzee na Mama, nilikuja kuijua baada ya kuanza fanya nae kazi) au nimkaushie aendelee kutuhudumia ila nikate mawasiliano naye as if sikuwahi mjua kabla?

Ile kitu imeniumiza sana and im way beyond kumsamehe huyu jamaa na kuendelea naye as before!. Mnaofanya biashara na watu msiowaamini mnadecide vipi hizi situation?..
 
Mpuuze msamehe kwa ajili ya familia yake

Punguza ukaribu nae siri zako usimpe

Baada ya muda mpige chini ili asikuharibie hataishia hapo nakwambia atakuchokonoa mpaka ahakikishe umeanguka

Sent using Jamii Forums mobile app
Nachoshindwa elewa anahisi anaweza vipi faidika iwapo mimi na wale jamaa tukiachana!.. Kuna muda nawaza maybe anajiona mfungwa kwa vile nilimleta na kumpangia cha kufanya lakini kwanini asielewe bila mimi hata hicho cha kufanya angekuwa hana!.
Anahisi kwa mimi kuwa nje ya game ataweza limiliki vizuri, asichoelewa nini kilipelekea kuungana sisi!..
 
Ndo maana alikuwa jobless

Masnitch wapo tuko nao tumezaliwa nao na tunaishi nao

Shukuru umemgundua mapema wengine hugundua ikiwa wameshaangushwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunze uandishi ambao Ni rahisi kueleweka kwa watu wote na pia unaweza kutilia mkazo suala la kufupisha habari kwa kutumia maneno muhimu TU.asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani ulifanya vibaya sana kumleta ndani kabla hujam study vizuri. Mtu ni kiumbe hai. Ulivyoamka jana sivyo ulivyo amka leo. Kule poteana naye kwa kitambo kidogo ujue alibadilika kwa kiasi. Pili; Mara nyingi, marafiki huoneana wivu sana pindi mmoja anapokuwa ali fail maisha na wewe ukainuka kiasi kwamba unamleta kwenye mafanikio yako.
Sasa, fanya maamuzi magumu. Mtafutie kosa kwa kuonesha kile alichokifanya kwako tofauti na wenzako. Umu expose kwa wenzako kwamba, kama ameweza kukufanyia hivyo, huenda yeye anajitafunia kiulaini zaidi. Hivyo, show that he is not worthy na umtimue mara moja. Ukisema ni kumvumilia, atakutafutia soft spot akumalize. Mvunja makubaliano yeyote sio mwema. Act ruthlessly tena kwa kushtukiza.
 
Ndo maana alikuwa jobless

Masnitch wapo tuko nao tumezaliwa nao na tunaishi nao

Shukuru umemgundua mapema wengine hugundua ikiwa wameshaangushwa

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna hela tulikopeshana, nikampa muda mrefu awe ananirudishia kidogo kidogo sasa nikichukua maamuzi najua nimeipoteza nayo!..
 
kuna hela tulikopeshana, nikampa muda mrefu awe ananirudishia kidogo kidogo sasa nikichukua maamuzi najua nimeipoteza nayo!..
Maamuzi yavutie muda usimfukuze kwa kukurupuka

Adhabu ya kisaikolojia ni nzuri sana unamfukuza kama unampumzisha na harudi tena kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibomoe kabisa...fukuza huyoo!hafai!asije kukuua bure

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitaka kutumia rafiki zetu lakini naona nitakuwa kama mwanamke kufungiana vikao!.. Nikimfata mwenyewe najua kitakachofata ni kugombana au akiwa mpole kazi zitaenda kwa njia ngumu wakati huo nikimtimua tu deni linakufa!.
 
Epuka sana mtu mfitini iwe kwenye kazi majumbani au kokote pale

Unasema unahofia kumfukuza kwa kuogopa deni kutolipwa, je mlivyolipana mliwekeana conditions gani? Mliandikishana??

Kila mtu abebe msalaba wake, ukianza kusaidiana kubeba wa mwenzio wa kwako utakuelemea.
 
Nadhani ulifanya vibaya sana kumleta ndani kabla hujam study vizuri. Mtu ni kiumbe hai. Ulivyoamka jana sivyo ulivyo amka leo. Kule poteana naye kwa kitambo kidogo ujue alibadilika kwa kiasi. Pili; Mara nyingi, marafiki huoneana wivu sana pindi mmoja anapokuwa ali fail maisha na wewe ukainuka kiasi kwamba unamleta kwenye mafanikio yako.
Sasa, fanya maamuzi magumu. Mtafutie kosa kwa kuonesha kile alichokifanya kwako tofauti na wenzako. Umu expose kwa wenzako kwamba, kama ameweza kukufanyia hivyo, huenda yeye anajitafunia kiulaini zaidi. Hivyo, show that he is not worthy na umtimue mara moja. Ukisema ni kumvumilia, atakutafutia soft spot akumalize. Mvunja makubaliano yeyote sio mwema. Act ruthlessly tena kwa kushtukiza.
Mkuu huyu jamaa nilimleta ili aweze nitengenezea mirija ya kutoka ile kampuni ili kuweza fanikisha mambo yangu mengine sasa iwapo nikiamua kumtimua ni kweli sihitaji vitu vingi saana kufanikisha lakini yupo sababu nataka kile 'kitu alichonacho kichwani mwake' halafu itanibidi nikubali kuishi bila kuitegemea ile biashara wakati sole purpose ya kuitengeneza ni ili inifanikishie mambo yangu!.
Nakubali nilichelea 'kumstudy' kabla sijamleta lakini pia nilifanya hivyo sababu wale marafiki naowajua na tunapendana hawana vitu vinavyohitajika na wanajitegemea kivyao pia niliiona hatari kuwaleta kwnye hili dili sababu ninavyopatana nao wangeweza kudai tugawane nusu kwa nusu badala ya huyu ambaye hakua die hard friend ambaye niliweza mpangia kitu cha kufanya!..
Mimi kama mimi siwezi mshirikisha rafiki ninayempenda/kumthamini kwenye dili ambazo ninajua fika zinanipa kitu unless nikimshirikisha aje kama Business Partner awekeze na chake pia!..
 
Back
Top Bottom