Kinondoni: Mwanafunzi apandishwa kizimbani kwa kumpa mimba mwanafunzi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Sekondari ya Mbezi (19), Juma Idd leo Jumatano Septemba 26, 2018 amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la tano mwenye miaka 14.

Mwanafunzi aliyepewa ujauzito wenye miezi mitano sasa anasoma shule ya msingi Kunduchi na tayari ameshaanza kliniki katika zahanati ya Tegeta.

Akisoma shtaka hilo leo mbele ya hakimu Joyce Mushi, wakili wa Serikali Daisy Makakala amedai tarehe tofauti kuanzia Aprili hadi Septemba mshtakiwa alimwingilia kimwili mwanafunzi huyo huku ukijua ni kosa kisheria.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana kosa na wakili Makakala aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika, kumuomba hakimu apange tarehe nyingine.

Hakimu Mushi alimweleza mshtakiwa huyo kuwa dhamana yake iko wazi kwa kuwa shtaka hilo linalomkabili linadhaminika.

Hivyo Hakimu Mushi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa na kila mmoja atasaini bondi ya Sh1 milioni, masharti ambayo mshtakiwa huyo aliyatimiza na kuachiwa huru kwa dhamana.

Akizungumza na MCL Digital nje ya mahakama hiyo, mlezi wa mtoto huyo, Mariam Issack amesema alimpokea mwaka 2016 kama mfanyakazi wa ndani.

Amesema baada ya kumuona kuwa bado ni mdogo aliamua kumtafutia shule na akapata nafasi shule ya Msingi Kunduchi akaanzia darasa la nne.

Baadaye alibaini ni mjamzito ndipo akambana ili amweleze nani aliyempa ujauzito lakini mtoto huyo hakutaka kumweleza ukweli moja kwa moja.

“Nilipoona hivyo nikaamua kwenda shuleni nikaonana na mwalimu mkuu akaitwa na baada ya kumbana ndipo alipomtaja huyo mshtakiwa na kuanza kumfuatilia hadi alipokamatwa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyo mlezi kiherehere sana. We umeletewa house girl, unampeleka shule kivipi?

Alitenda wema kadri nafsi yake ilivyomtuma pia sio vema kuwa na msichana wa kazi Mdogo kiasi hicho.

Kihehere chake ni kupeleleza aliyempa mimba huyo bint, waangalia namna nyingine ya kusolve.
 
Duh.. Asee dogo kakipimia size yake imenasa mambo yamekuw hovyo.

Ila huyo mlezi nae ndio snitch kama vipi angemkabidhi manzi wa wazazi wa dogo wamlelee akizaa aendelee kuwa hausigelo
 
Hakuna kesi hapo, atahukumiwa kwenda jela au faini isiyozidi laki 5 dogo arudi shule akasome
 
Kama wote ni wanafunzi adhabu ni miaka 30?Huyu dogo atakomaa kukimbilia sketi
 
Back
Top Bottom